Tusimuonee Mghwira, kwani wabunge wanatekeleza ilani ya chama gani?!

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Kwanini iwe nongwa kwa Mghwira kukabidhiwa ilani ya chama tawala? Hebu niambieni wabunge bila kujali vyama wanavyotoka wanatekeleza ilani ya chama gani kama siyo chama tawala CCM!

Uchaguzi ukiisha tunabaki na Ilani mona tu ya chama kilichoshinda, ndio maana Rais Magufuli alipotembelea wilaya ya Hai, Mh. Mbowe alikuwepo kuelezea namna ilani ya chama tawala inavyotekelezeka/inavyokwama ili kuangalia namna bora ya kuenenda.

Hata mawaziri vivuli kazi yao ya msingi ni kuelezea changamoto wanazokutana nazo ktk kutekeleza ilani ya chama tawala.

Tumwache mama afanye kazi zake hapo KLM, ahsante.
 
Kwani kuna mtu kamzuia kufanya kazi?, unatoka povu la nini?! Tatizo lake ni unafiki wake, hii nafasi hakuwa anaikubali wakati anatetea katiba mpya (ya wananchi) hizi nafasi zilikuwa hazina kazi yoyote kwa nini leo akubali na kuapa atafanya kazi kwa ilani ya chama cha mapinduzi? Kazi gani hiyo aliyoigundua baada ya yeye kupewa ukuu?! Unafiki wa kina polepole ndio maana tunashauriwa kuweka akiba ya maneno.
 
Wabunge hawatekelezi ilani yoyote bali wanaisimamia serikali na kuhakikisha inatekeleza wajibu wake.

Kwa hiyo wajibu kutekeleza ni wa serikali, ndiyo maana kuna mihimili mitatu bunge na mahakama haitekelezi ilani
 
Hizo kazi anazokwenda kuchapa ni zipi, tofauti na zinazoeleweka na kila mtu!!
 
Wabunge hawatekelezi ilani yoyote bali wanaisimamia serikali na kuhakikisha inatekeleza wajibu wake.

Kwa hiyo wajibu kutekeleza ni wa serikali, ndiyo maana kuna mihimili mitatu bunge na mahakama haitekelezi ilani
Kwa hiyo wakati wa kampeni huwa wanatudanganya?
 
Wabunge hawatekelezi ilani ya chama chochote, wabunge kazi yao ni kuisimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake. Ni vile tu wabunge wa CCM wameharibika kimaadili kiasi hawajui wapo bungeni kwa sababu gani ndio maana na wewe unadhani wanatekeleza ilani.
 
Wabunge wa chama gani?umeona mbunge wa chadema anashiriki kukimbiza Mwenge ulio katika ilani ya CCm?
 
Uongozi wa kweli si kutekeleza ilani Mkuu, Ni kutatua matatizo ya wananchi.

Uongozi makini ni ule unaoongozwa na Mtu anayejitambua.Akiongozwa na Hekima, Busara, Unyenyekevu na Ucha Mungu.

Haya mengine, sijui kuwa na ilani au hata kutokuwa nayo ni extra tu.

Ninasema hivi nikiwa na maana kuwa tulishakuwa na viongozi wengi wenye marundo ya ilani za vyama hadi chumbani mwao ila hali zetu bado ziko vile vile mwaka baada ya mwaka (What ilani means so far if we cant solve problems)?.

Kama wewe ni Mkristu, kasome Uongozi wa Manabii kuanzia Musa, Kalebu, Yusuphu, Daudi, Solomon, Esther na hadi kwa Mtume Paulo then unieleze kuwa walikuwa na Ilani zipi.Hii ndiyo tafsiri ya Uongozi.
 
inabidi uelewe wajibu wa bunge na wabunge,please jisomee kwanza kabla ya kutoa maoni yako,wabunge hawatekelezi ilani ila wapo kuona serikali inasimamia vema kodi zetu katika utekelezaji wa majukumu wa chama tawala,again tunarudi palepale tatizo ni katiba mbovu ambayo imetoa madaraka makubwa mno kwa watawala,ilitakiwa BUNGE ndilo liwe na madaraka hayo.for now ni kuisoma namba hadi generation itakayo fungua macho sie bado usingizini.
 
Kwanini iwe nongwa kwa Mghwira kukabidhiwa ilani ya chama tawala? Hebu niambieni wabunge bila kujali vyama wanavyotoka wanatekeleza ilani ya chama gani kama siyo chama tawala CCM!

Uchaguzi ukiisha tunabaki na Ilani mona tu ya chama kilichoshinda, ndio maana Rais Magufuli alipotembelea wilaya ya Hai, Mh. Mbowe alikuwepo kuelezea namna ilani ya chama tawala inavyotekelezeka/inavyokwama ili kuangalia namna bora ya kuenenda.

Hata mawaziri vivuli kazi yao ya msingi ni kuelezea changamoto wanazokutana nazo ktk kutekeleza ilani ya chama tawala.

Tumwache mama afanye kazi zake hapo KLM, ahsante.
Jina lako halifanani na akili yako mkuu
 
Wabunge hawatekelezi ilani ya chama chochote, wabunge kazi yao ni kuisimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake. Ni vile tu wabunge wa CCM wameharibika kimaadili kiasi hawajui wapo bungeni kwa sababu gani ndio maana na wewe unadhani wanatekeleza ilani.
Kati ya huyu Mbunge aliyeharibika kimaadili kiasi kwamba hajui yupo Bungeni kwa sababu gani, Je tatizo lipo kwake au mpiga kura (Siku hizi wanaita kula)?.

Nimeuliza hivi kwakuwa Watanzania wengi ni hodari sana na tunatumia muda mwingi kumchagua mbuzi au kitoweo cha kumchinja siku ya sherehe kuliko muda wa kumchambua Kiongozi atakayetuongoza kwa takribani muongo mmoja au hata zaidi.

Yaani ukienda mchinjioni na kumkuta mtu akimchagua mbuzi wa kwenda kumchinja kesho (siku ya shughuli) utashangaa kumuona akimkagua kuanzia kwato, macho, pembe nk.Huyu ni mnyama wa kuchinjwa kesho ila tunatumia zaidi ya lisaa kumchambua.

Rudi sasa katika kumchambua kiongozi.Dakika mbili tu, tayari anakuambia "Huyu ndiye anafaa".

Nadhani hapa ndipo ulipo mzizi wa tatizo.
 
Elimu ndio shida. Majority hatujitambui, tupo tupo kama subjects wa dola za kifalme.
 
Wabunge hawatekelezi Ilani. Wabunge huizungumza tu Ilani. Watekeleze wao wana pesa?
Hivi kutekeleza jambo lolote lile ni lazima uwe na pesa?.

Huwezi ku-mobilize wananchi na kutatua tatizo pasina kutumia fedha?.Nb;Kumbuka matumizi ya fedha yameanza kutumika miaka 2000 iliyopita.Je Serikali za kipindi kile hazikuwa zikitekeleza mambo kwakuwa hazikuwa na pesa?.

Karibu.
 
Elimu ndio shida. Majority hatujitambui, tupo tupo kama subjects wa dola za kifalme.
Kuwa na Elimu na kujitambua ni vitu viwili tofauti Mkuu.

Nimekutana na watu (Phd's, Doctrates,Degree's holders) wengi sana ila hawajitambui.Pia nimekutana na wengi mno wasio na Elimu (Japo ya darasa la kwanza) ila wanajitambua mno.

Unadhani Elimu ina-matter katika kuyamtambua mambo?.Au ni sifa tu ya ziada?.
 
Wabunge hawatekelezi ilani yoyote bali wanaisimamia serikali na kuhakikisha inatekeleza wajibu wake.

Kwa hiyo wajibu kutekeleza ni wa serikali, ndiyo maana kuna mihimili mitatu bunge na mahakama haitekelezi ilani
Ndo kutekeleza kwenyewe huko.....unaisimamia serikali yenye ilani yake= kusimamia ilani itekelezwe sawasawa
 
Back
Top Bottom