Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,615
zITTO AMEDHIHIRISHA WAISLAM TUNAWEZA
Ugonvi wote wa Mhando na Maswi ni nani apewe tender ya ku supply mafuta IPTL..haya mengine ni kachumbari na Mazingaombwe kama alivyosema Mwanakijiji..
Kwanini kuna sheria? Sheria ipo ili kulinda masilahi ya watu na Taifa. Iweje sasa kama hiyo sheria hailindi masilahi mapana ya jamii iendelee kuwa cover kwa wale wanaolihujumu Taifa? Ni wazi kabisa above sheria kuna kitu kinachoitwa dhamira njema (Social capital) ambayo kama sote tungekuwa nayo hizo sheria zisingetungwa maana kila kitu kingefanywa inavyotakiwa. Huwezi kusema eti polisi akikamata mhalifu wa kubambikiza huku akiwa kafuata taratibu zote na sheria zote basi anahaki ya kufanya hivyo kwakua ana dhamana ya kipolisi kufanya hayo. Ndivyo ilivyo hata katika sheria kama sheria imetumiwa kihalifu basi hiyo sheria imeshindwa kulinda haki ya jamii na hivyo kama kuna mtu ameonekana kukiuka sheria ili kuilinda hiyo haki basi huyo eti awe ndiye wa kuadhibiwa na yule aliye tumia sheria kuhujumu eti yeye aachwe; hicho ni kituko ambacho kinaweza kufanywa na jamii isiyojitambua.
Sheria ipo kulinda haki za raia na jamii nzima lakini sheria inaposhindwa kuzilinda haki hizo hiyo sheria inakosa uhalali kwa hiyo specific case na katu hili lisiwe kisingizio eti wengine watafanya hivyo hivyo wakati mwingine maana sheria haitumiwi bila context ndiyo maana kuna watafsiri wa sheria ambao hawapo kama kasuku kuhukumu bila kuangalia context na mazingira halisi ya tukio husika.
Watu katu wasihusishe mazingira ya Richmond na haya ya wakati huu kwani sote tunazo akili na ufahamu wa kutosha kujua ni uamuzi upi umelinda haki na upi unahujumu taifa pale ambapo sheria imetokea kutumiwa kufanya uhalifu badala ya kulinda maslahi. Cha msingi ni case zote kuwa tabled kwa uwazi naiweke wazi ni maslahi yapi yalikuwa yanalindwa na nani kwa faida gani then ukweli utajiweka wazi na haki itatendeka.
Ninachosisitiza ni kuwa sheria pekee hata siku mmoja haitajisimamia kulinda haki kama wanaozitumia hizo sheria hawatakuwa na high social capital na ndiyo maana si wote wanapewa dhamana ya kuongoza bali wale tu wenye maadili mema walio fanyiwa vetting na vyombo husika (Kama hili linafanyika ama la wakati huu ni discussion nyingine). Hivyo watu wasijifiche kwenye kichaka cha sheria na kanuni kutenda na kuficha maovu yao kwani sheria yaweza ama kulinda au kuhujumu maslahi mapana ya raia na jamii kama itatumiwa tofauti na malengo yaliyokusudiwa.
Wengi tunaweza kusoma,
lakini hatuwezi kuchambua,
na kujua maana ya kilicho,
andikwa kwa undani.
Kuna haja ya kujielimisha,
zaidi katika uwanja wa,
kuchambua hoja kwa,
kwa umakini mkubwa,
na kuuliza maswali ya,
udadisi na kutaka kujua zaidi.
Mkuu chuki na hasira kwa sababu anahusika Zitto zisisababishe uandike vitu ambavyo unajua siyo sahihi lakini unatetea uwongo! Amka kijana. Udhaifu wa watawala usikupofushe kushabikia watu wasioheshimu sheria na taratibu tulizojiwekea.