Tusimlaumu Mwigulu kutaka kutupandishia kodi ya nyumba,tumlaumu anayembeba

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,293
3,965
Ni masikitiko makubwa sasa serikali inataka kutuongezea malipo ya kodi ya nyumba kama walivyokuwa wanafanya madalali wa nyumba.
Sasa serikali inataka kila mwaka iwe inakusanya mapato ya uonevu kwetu maskini

Nalipwa mshahara nakatwa kodi,nikiitoa pesa benki nakatwa,kodi,nikipia umeme nakatwa kodi ya nyumba,nikilipa kodi ya pango,natakiwa nikamlipie kodi mwenye nyumba.Mwenye nyumba akishasema tu nilipe changu,unabaki wewe na deni la kulipa TRA tena!
Kwa kweli ni ukatili sana huu lakini sisi tutamlilia Mungu wetu.Maana hawawezi kutenda haki kwa vile wana nguvu ya dola.
Hatuwezi kuwaondoa kwa kura kwani wana tumia pesa za kodi zetu kutukandamiza.Mungu yupo
 
Pesa za kuwalipa wabrazil na kununua yutong lazima zipatikane kwa namna yeyote ile
 
Kwenye Kodi ya nyumba za kupanga. Hiyo ni biashara. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya 🇹🇿 Kila biashara ni lazima ilipe Kodi. Kama mwenye nyumba atakupangisha nyumba kwa laki Moja Kila mwenzi basi ni lazima atoe %10 vinginevyo huyu mtanzania mwenzetu atakuwa anaishi Bure🇹🇿. Ila kwenye tozo Mimi ndio nawakataa Tena nawakataa mazima.hakuna wa kunishawishi tozo ni salama kwangu
 
Yaani kaaa kwa kutulia mtoto mdooooogoooo, mnuka jasho ,kubwa jinga lisilo na akili a.k.a MNYONGE, sasa kwa taarifa yako kila mwaka v-8 za billions 600 zinaagizwa, V-8 MOJA NI MILLIONS 500 SAWA NA KITUO CHA AFYA

Zinajazwa mafuta full tank, full Ac na hakuna kuzimwa hata kama boss yuko bar na mrembo wa bongo movie wanakula manyama na kushushia na ma wine toka ufaransa

Kaa kwa kutulia weweeeee unalalamika tozo unadhani watoto wako watsomea kwenye nini bila tozo? madarasa yatajengwaje? vituo vya afya vitajengwaje?

Najua mimacho umetolea kwenye v-8 , yees ni lazima kila mwaka model mpya ikitoka waheshimiwa waipate sababu wanaumiza sana vichwa kuwatumikia nyie wanuka jasho msio na shukrani

Mmeletewa hadi wachezaji toka brazil, argentina kwenye team iliyoko singida lakini bado hamna shukrani, hela yenyewe ndogo inayovamiwa kwenye vi account vyenu mnaiona nyiiingi wenyeeewe, LAZIMA MUUMIE LA SIVYO SHULE NA ZAHANATI HAKUNA NAMBA NYINGINE YA KUJENGA

UNAIJUA V-8 WEWEEEEEEEE? MTOOOOTO M-LITTLE, MNUKA JASHO, KUBWA JINGA



v81.JPG



v82.JPG



tozovx.jpg
 
Yeye mbona hanaheshima Nani kamwambia tunataka tozo,wapi wananchi tumetoa maoni yetu juu ya tozo?
Twaweza wamelitafiti Hilo na 64% ya watanzania tumekubaliana na Hilo, Hata bila utafiti huo sisi watanzania tunamuunga mkono mh Rais wetu katika juhudi za kuijenga nchi yetu wenyewe, maana hatutaki mzigo wa madeni utuelemee baadaye, hatutaki tukope kwa kila kitu
 
Twaweza wamelitafiti Hilo na 64% ya watanzania tumekubaliana na Hilo, Hata bila utafiti huo sisi watanzania tunamuunga mkono mh Rais wetu katika juhudi za kuijenga nchi yetu wenyewe, maana hatutaki mzigo wa madeni utuelemee baadaye, hatutaki tukope kwa kila kitu
Wewe unaishi dunia gani?CCM walisema Sisi ni Dona country,tukala tukasaza tukaamka ,tunaambiwa tunafungua nchi Nani alifunga?Hiyo mikataba na mikopo mbona hatuoneshwi kama wenyenchi ambao tunatakiwa kulipa!Mbona raia wasihoji au kuuliza wanapigwa au kufungwa kwenye nchi Yao !Juzi hapa tuliambiwa mama amekwenda kuchukua mikopo huko ulaya hivyo miradi itakwenda vizuri hatujakaa Sawa tunaambiwa tozoooooo Kwa ajili ya madarasa zahanati ,hizo pesa zote mnafanyia nini?Mwisho kabisa kama mnafanya Siri huo ni uzwazwa !narudia tena pesa za maendeleo mumewaachia wazungu watafute!Pesa za kununulia chupi na gagulo za Samia ni tozoooooo
 
Back
Top Bottom