Tusimchague Jakaya Kikwete na tusiichague CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusimchague Jakaya Kikwete na tusiichague CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by sifdav, Oct 4, 2010.

 1. s

  sifdav New Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kutoa uchambuzi wangu kwa watanzania nikiwasihi kutomchagua Jakaya Kikwete na kutoichagua CCM.Kuna sababu 16 zinazohalalisha watanzania kutomchagua Kikwete na CCM,nazo ni;

  1.Embu kumbuka ilani ya CCM ilivyokuwa ya kisanii,2005 alisema atashughulikia mahakama ya KADHI wakati safari hii amefuta kabisa kipengele hicho katika ilani yake bila hata kufikiri IMPACT yake.

  2.Aliunda baraza la mawaziri na kulichakachua randomly na alipoulizwa kwanini unalichakachua baraza kwa kubadilishabadi lisha mawaziri alisema UWAZIRI hausomewi.

  3.Alipotajwa mkapa katika ufisadi alimkingia kifua kwa kumtetea kuwa sio vizuri kumchambua kiongozi alimaliza mda wake.

  4.Kuhusu suala na malipo ya wazee East Africa JK serikali yake ya CCM waliwarushia mabomu na maji ya kuwasha wazee hao bila kuwajali halafu leo hii wanadai eti wanawajali wastaafu.

  5.JK anapenda kushiriki vitu ambavyo hatakiwi hata kidogo kwa wadhifa alionao kufanya hivyo(anahulka ya kutaka aonekane mtendaji sana);kumbuka suala zima la kutoa ambulance moja tu ikulu eti iliandaliwa tafrija kubwa katika suala hilo wakati hata mkuu wa mkoa angemwakilisha katika hilo sehemu husika.na mungu alivyo mkubwa aliumbuka baada ya kudanganywa katika utaratibu mzima wa
  kugawa gari hilo.
  6.Embu kumbuka suala zima la wafanyakazi TUCTA alivyojibu kuwa hataki KURA za wafanyakazi na baadae akashindwa kuyameza maneno yake mwenyewe eti kasema hakukataa kura za wafanyakazi.

  7.Embu angalia suala zima la EPA na richmond alivyolipiga chenga eti akaamuru wale wote waliochukua fedha za EPA warudishe haraka sana bila hata kutajwa.

  8.Embu kumbuka alijinadi kwenye media na kusema wala rushwa na wauza madawa ya kulevya ana majina yao yote na akaahidi kuwashighulikia ;hajatekeleza ahadi yake hiyo.YAANI wewe acha tu.

  9.Eti anasema bila kwenda nje tungekufa njaa.huu ni UGANDIFU WA UBONGO.
  10.Eti anadai kuwa ahadi zake katika ilani ya CCM amazitekeleza kwa kiasi kikubwa na akataja asilimia 99.EEEhh hapo ndo nilichoka kabisaaa.
  11.Eti anasema akiondoka 2015 akumbukwe kwa mambo 10 alipoorodhesha inaonekana kuwa mambo yenyewe yanalenga KILIMO tu vipi kuhusu Elimu,afya,miundominu,ajira n.k);hapo nadhani munanielewa vizuri naposema JK ana matatizo ya akili.

  12.Alipoingia madarakani JK alingia na amendesha NCHI kwa VISASI na kwa vitisho na wale wote ambao hawakumdhamini katika fomu yake ya URAIS walikiona kwaniwengi wao waliachishwa kazi,walishushw a vyeo,walikosa ubalozi n.k mtawakumbuka akina Stephen Mashishanga,Nic odemus Banduka,Philip mangula na wengine wengi tu.

  13:pia angalia namna alivyodanganywa katika sheria ya gharama za uchaguzi ilivyosainiwa kwa mbwembwe mpaka Dr SLAA alipokosoa makosa ya muswada huo na ukarudishwa bungeni kupitishwa tena.Hajui alitendalo na hayuko makini kabisa.

  14:Kumbuka mswada wa kuunda baraza la usalama lilivyorudishwa mara mbili bungeni wakati yeye ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri.Inaonyesha JK anamatatizo ya UBONGO.

  15.Embu angalia wakati huu wa kampeni jinsi Tanzania ilivyobadilishwa kuwa nchi ya kifalme kwa wakuu wa wilaya wanavyopiga saluti kwa mke wa Rais na mtoto wa Rais(Ridhiwani).Je unajiuliza kuwa Salma na Ridhiwani wanachokitafuta ni nini? wakiingia madarakani si wataitafuta nchi.

  16. Kumbukeni Raisi Kikwete alipokuwa ziarani Ufaransa na akaulizwa kwa nini nchi yake ya Tanzania ni masikini na akajibu kuwa hajui.

  Na kwa kuliona tatizo hilo CCM wakakaa wakachambua na wakaona mbali kuwa JK hana ubunifu wa aina yeyote katika kujibu hoja mbalimbali nzito(kichwa maji-kilaza)na ndio maana Makamba na Kinana wakaamua KUKACHA MDAHALO.
  Na nina wasi wasi kuwa akipita JK(kwa wizi wa kura)sitashangaa nikisikia wale wote waliotajwa katika kesi ya EPA na RICHMOND wameshinda kesi na wanaidai fidia ya kudhalilishwa serikali ya JK.

  TUSIMCHAGUE KIKWETE.TUMCHAGUE DR.SLAA hapo OKTOBA 31,2010 KUWA RAISI WA TANZANIA
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Yapo mambo ambayo ni makosa yake ya wazi na mengine inawezekana yapo nje ya uwezo wake. Lets not be so much optimistic, manake tukiwa hivyo basi hata akiingia Dr. Slaa tutamchoka baada ya siku chache, maana yumkini atakutana na mambo ambayo yatakuwa nje ya uwezo wake wa kibinadamu.
   
Loading...