Tusimame na Iran na Qatar

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,879
Tunasimama na Iran na Qatar, Uonevu Dhidi Yao Si Sawa - Tanzania Tusaidie Amani ya Ulimwengu.

[Sehemu ya Nne na ya Mwisho ya Hotuba ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (MB) Juu ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2018/19]

Mheshimiwa Spika

Jambo la mwisho kwenye mchango wangu ni juu ya hali ya ulinzi na usalama duniani. Usiku wa kuamkia Disemba 9, 2017, tulipoteza askari wetu 14 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa huko DRC Congo, wakiwa kwenye Jeshi la kulinda Amani la Umoja wa Mataifa. Nachukua nafasi hii kuwaombea kwa Mola awalaze pema, pamoja na kutoa pole kwa familia zao na kwa Jeshi zima la JWTZ. Hawa ni wazalendo waliokufa wakibeba bendera yetu ya amani ulimwenguni.

Taifa letu linachangia pakubwa katika kulinda amani ya ulimwengu, wanajeshi wetu wakiwa karibu katika nchi nane duniani. Naamini tunao wajibu kama Taifa kusaidia uwepo wa amani Ulimwenguni ili kuzuia nchi zilizo kwenye machafuko kama DRC Congo kuongezeka na askari wetu wa kulinda amani kupotea.

Tayari, katika siku za karibuni, dunia imeshughudia maafa makubwa ya vita nchini Libya (ambako Rais Kikwete ni msuluhishi), Iraq, Afghanistan, Somalia, Syria, Sudan Kusini na Yemen. Mwenendo wa migogoro na uonevu unofanyika Qatar na unaotaka kufanyika Iran unapaswa kukemewa mapema ili kuchochea amani ulimwenguni, hasa eneo la mashariki ya kati ambalo tayari limeharibiwa na vita.

Hotuba ya Waziri ya Bajeti ya Wizara hii kwa mwaka 2016/17 ilibeba pongezi kwa nchi za Iran, Marekani, China, Urusi, UN na Umoja wa Ulaya (hasa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani) kwa makubaliano ya Nyuklia yaliyoiondolea vikwazo Iran kwa masharti ya kutoendeleza urutubishaji wa nyuklia. Makubaliano yale ni muhimu kwa kuwa yaliondoa hali ya mashaka iliyokuwa imetanda duniani.

Tumeona Marekani imejitoa kwenye makubaliano hayo, na kutishia kuweka vikwazo vipya kwa Iran. Huku wajumbe wengine wa makubaliano hayo wakiendelea kubaki, kwa kuwa bado Iran imeendelea kutekeleza makubaliano hayo, na kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA ni kuwa bado Iran inafuata masharti ya makubaliano husika.

Uamuzi huu wa Marekani si mzuri, unarudisha hali ya mashaka kwenye eneo la mashariki ya kati, ni uonevu dhidi ya Iran, hasa kwa kuwa IAEA imethibitisha kuwa Iran haina makosa. Ni uamuzi wa uonevu tu na usiochochea amani, ni uamuzi unaopaswa kupingwa. Serikali yetu iitumie nafasi yake kule UN kupinga uamuzi huu, na kuitaka Marekani kurudi kwenye makubaliano haya ili kudumisha amani.

Pia, Julai 26, 2017 Wizara hii ilitoa taarifa yake juu ya mgogoro wa nchi za Ghuba (GCC), baada ya hatua ya nchi nne za Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri za kuiwekea vikwazo vya anga, bahari na ardhini nchi jirani ya Qatar. Msimamo wa Serikali yetu ni kuunga mkono upatanishi unaongozwa na Amir wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Jaber, sisi ACT Wazalendo tunaunga mkono msimamo huo.

Lakini bado pia sisi ACT Wazalendo tunasimamia tamko letu la kupinga uonevu dhidi ya Qatar tulilolitoa July 24, 2017. Kwa karibu miezi 10 sasa watu wa Qatar wamewekewa vikwazo vya kiuchumi na kiusafiri, kwenye anga, ardhi na bahari na nchi hizo nne jirani, jambo hilo si sawa, hasa kwa kuwa masharti yaliyotolewa ili kuondoa vikwazo hivyo yanaingilia uhuru wa nchi hiyo.

Tunaitaka Serikali yetu, pamoja na kusapoti usuluhishi huu wa Kuwait, itumie nafasi yake pia kule UN kuhakikisha inachangia usuluhishi wa jambo hili ili mashaka yaliyoko na vikwazo kwa Qatar viondoshwe, ni wajibu wetu huo kama taifa kusaidia amani ya dunia na hivyo askari wetu kutokupoteza maisha wakiwa wanalinda amani kwenye maeneo mbalimbali yaliyo na vita na migogoro.

Ahsanteni kwa Kunisikiliza. Naomba Kuwasilisha

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bungeni Dodoma
Mei 23, 2018
 
Trump alisema tokea siku anaapishwa kushika wadhifa wa urais. From now onward, it is America first.
Hao jamaa wakishaamua jambo watalifanya tu, bado hatujafikia hatua za kutumia ipasavyo vyombo kama UN, AU na vinginecyo kupaza sauti zitakazo leta tija na kubadili maamuzi ya hawa mabepari. UN kimsingi nayo ni kama ipo kuhakikisha maslhai yao yanatekelezwa lakini ni chombo zaifu sana chenye jina kubwa.
 
rais mwenyewe hata somalia hajawahi kufika,nani atamsikiliza!!!!
halafu hao waarabu wenzao wamewasaliti waarabu wenzao inabidi tujiulize kwanini
 
NOO ZITO TUSIMAME NA MASLAHI YETU KAMA TAIFA, TUMESHASIAMAMA NA WATU SANA HUKO NYUMA, JE NI NANI ANASIMAMA NA SISI.
Hiyo point,tuna mind mambo ya watu miaka yote mpaka tukuwa fukara,
Acha mbwa ale mbwa
Kama taifa tumegawanyika na hakuna hatua zinazochukuliwa,
Bunge na mahakama zimewekwa mfukon,democracy ipo mashakani,uchumi unayumba,tumekua marafik wa madikteta badala ya Tawala Bora
Watu wanatekwa,wanauwa,polis wanauwa raia hakuna hatua,Rais anatoa kauli za kibaguz na tata hakuna wa kuongea
Tutibu Tz kwanza
 
Hao Iran wanacheza na moto haiwezekani wawatishe wayahudi kwamba watawafuta kwenye ramani ya dunia alafu hii ACT wasilaani lakini hao mbari nyingine ya wayahudi.

Zito unasahau tena Kush Timbuktu wairan walichofanya pale africa magheribi alafu bado unawatetea.

Mimi naomba Mungu Iraq nyingine izaliwe iran maana wanaunda silaha za rocket alafu wanataka kuzipeleka Israel

Go to hell Iran
 
Hao Iran wanacheza na moto haiwezekani wawatishe wayahudi kwamba watawafuta kwenye ramani ya dunia alafu hii ACT wasilaani lakini hao mbari nyingine ya wayahudi.

Zito unasahau tena Kush Timbuktu wairan walichofanya pale africa magheribi alafu bado unawatetea.

Mimi naomba Mungu Iraq nyingine izaliwe iran maana wanaunda silaha za rocket alafu wanataka kuzipeleka Israel

Go to hell Iran

Mh. Magufuli na Wananchi wetu ni wapenda amani. Tutawasuport tu kama ni wajenga amani Duniani. Kwanza hawawezi kuifuta ISRAEL, wasahau hilo.
 
Wanasapoti ugaidi duniani, tutakosa misaada
Hizo ni chai tu mkuu...Iran anapigana vita ya kiuchumi sawa na Qatar so Wazungu lazma wamchukie. Ogopa sana mtu anayeikataa Dolar kama base curency kwenye uchumi wake kitu ambacho China na Urusi wanakifanya.
Wamepinga matumizi ya Dollar kwenye biashara zao, na ndo hicho hicho kilichomuondoa Gaddafi Libya.
 
Hizo ni chai tu mkuu...Iran anapigana vita ya kiuchumi sawa na Qatar so Wazungu lazma wamchukie. Ogopa sana mtu anayeikataa Dolar kama base curency kwenye uchumi wake kitu ambacho China na Urusi wanakifanya.
Wamepinga matumizi ya Dollar kwenye biashara zao, na ndo hicho hicho kilichomuondoa Gaddafi Libya.
Fuatilia vizuri kama unajua uchumi, nchi yeyote yenye watu siriazi haiwezi kuacha kushirikiana na US na EU
 
Rais Kikwete aje asuruhishe na humu ndani... (Japo sijui ni rais wa nini? au kikwete foundation)
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom