Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,339
- 45,659
Wiki hii na mwaka huu vimetia fora kuhusu habari za wamchinga. Bungeni wamejadiliwa, Ofisi namba moja imezungumza kuwahusu na leo Morogoro watu wametumbuliwa kwa sababu yao, RC wa Dar bado anagugumia na kiswahili kingi cha kuwapanga wasizibe mitaro iweze kufanyiwa usafi.
Hizi ni sehemu tu suala hili lilipopata nafasi sehemu ya mbele ya vyombo vya habari lakini kupo kwingi ambapo hapajaweza kumulikwa.
Kuzidi kushamiri kwa wamachinga na zaidi sana wakiwa wanauza bidhaa za Wachina ni dalali mbaya ya uchumi dhaifu na usio endelevu.
Wanapozidi kuongezeka wamachinga ndivyo ndoto za uchumi wa viwanda zinazikwa taratibu, ndivyo mifumo ya biashara rasmi inazidi kuparanganyika, ndivyo ukusanyaji wa kodi utakuwa mgumu zaidi na ndivyo mazingira ya miji yataharabiwa kabisa.
Ili nchi iwe na uchumi imara na endelevu sehemu kubwa ya raia nchi inahatajika wawe wanafanya kazi katika sekta za uzalishaji kama viwanda, madini, ujenzi na huduma kama utalii sio kuchuuza bidhaa hafifu za nchi nyingine barabarani na kuuza malighafi.
Watunga sera wanaolipwa kwa kodi za wananchi wanao wajibu mkubwa na wa haraka kulikwamua taifa kutoka katika mtego huu mbaya wa umaskini na uharibifu kwa taifa. Watimize wajibu wao kabla maji hayajakorogeka zaidi.