Mkakati wa Chato kuwa mkoa wapingwa rasmi na RCC ya mkoa wa Kagera

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
55,792
90,594
Anaandika Askofu Bagoza PhD.

TUNAHITAJI HALMASHAURI NYINGI KULIKO MIKOA NA WILAYA MPYA

Kamati ya Maendeleo ya Mkoa wa Kagera (RCC) imemaliza kujadili mapendekezo ya kuundwa kwa Mkoa mpya wa Chato. Wengi wanakataa mapendekezo hayo. Niliwaunga mkono mapema.

Natamani Taifa lihitimishe uundwaji wa MIKOA na Wilaya mpya. Badala yake, jopo la wataalam wa kada mbalimbali, wajikite katika kupendekeza uundwaji wa HALMASHAURI mpya. Kwa Nini tunahitaji zaidi HALMASHAURI kuliko MIKOA na Wilaya?

1. Masuala karibu yote ya Maendeleo yako TAMISEMI.

2. Halmashauri ni kitovu cha mamlaka ya wananchi kujipanga na kusimamia mambo yao.

3. Tuachane na "developmentalism" (U-maendeleo) na kuingia katika "transformation"(Mabadiliko).

4. Maendeleo endelevu hayahitaji "Uimra" (top to down) bali "uasi Mtakatifu" (bottom up). Ma RC na Ma DC ni alama za unyapara. Wanatupeleka mtoni lakini hawawezi kutulazimisha kunywa maji hata kama tuna kiu.

5. Inawezekana kuwa na Halmashauri hata 5 katika Wilaya moja wakati kwa mtindo wa sasa kuna hatari ya Wilaya 2 kugombania Halmashauri Moja.

6. Jopo la wataalam lizame kutafuta namna nyepesi ya wateule wa Rais kufanya kazi na wateule wa wananchi pasipo mgongano wala kutambiana. Siku hizi wateule wa Rais wanawanyanyasa wateule wa wananchi wakati Rais naye ni Mteule wa wananchi.

Ili haya yafanikiwe, semina elekezi zinatakiwa na zisiendeshwe na Rais. Wateule wengi wamejipa haki ya kumdanganya Rais kwa kusifia, kujipendekeza na kumhakikishia Rais kuwa anajua kila kitu.

Hatukuchagua malaika kuwa RAIS wetu. Na hatukuchagua RAIS ili ageuke malaika. Tunamnyima Rais fursa ya kunyenyekea.

KAZI IENDELEE
 
Hizo ndizo sababu za hiyo RCC au ni maoni yako mleta uzi?
Mleta hoja badala ya kuleta yaliyojiri RCC Kagera, kaja na mtazamo wa Askofu. Ingekuwa na uzito sana hoja yake kama ingesema nini RCC ya Kagera imeamua then tusikie nini Askofu Bagonza anashauri/ana-challenge.
 
Anaandika Askofu Bagoza PhD.

TUNAHITAJI HALMASHAURI NYINGI KULIKO MIKOA NA WILAYA MPYA

Kamati ya Maendeleo ya Mkoa wa Kagera (RCC) imemaliza kujadili mapendekezo ya kuundwa kwa Mkoa mpya wa Chato. Wengi wanakataa mapendekezo hayo. Niliwaunga mkono mapema.

Natamani Taifa lihitimishe uundwaji wa MIKOA na Wilaya mpya. Badala yake, jopo la wataalam wa kada mbalimbali, wajikite katika kupendekeza uundwaji wa HALMASHAURI mpya. Kwa Nini tunahitaji zaidi HALMASHAURI kuliko MIKOA na Wilaya?

1. Masuala karibu yote ya Maendeleo yako TAMISEMI.

2. Halmashauri ni kitovu cha mamlaka ya wananchi kujipanga na kusimamia mambo yao.

3. Tuachane na "developmentalism" (U-maendeleo) na kuingia katika "transformation"(Mabadiliko).

4. Maendeleo endelevu hayahitaji "Uimra" (top to down) bali "uasi Mtakatifu" (bottom up). Ma RC na Ma DC ni alama za unyapara. Wanatupeleka mtoni lakini hawawezi kutulazimisha kunywa maji hata kama tuna kiu.

5. Inawezekana kuwa na Halmashauri hata 5 katika Wilaya moja wakati kwa mtindo wa sasa kuna hatari ya Wilaya 2 kugombania Halmashauri Moja.

6. Jopo la wataalam lizame kutafuta namna nyepesi ya wateule wa Rais kufanya kazi na wateule wa wananchi pasipo mgongano wala kutambiana. Siku hizi wateule wa Rais wanawanyanyasa wateule wa wananchi wakati Rais naye ni Mteule wa wananchi.

Ili haya yafanikiwe, semina elekezi zinatakiwa na zisiendeshwe na Rais. Wateule wengi wamejipa haki ya kumdanganya Rais kwa kusifia, kujipendekeza na kumhakikishia Rais kuwa anajua kila kitu.

Hatukuchagua malaika kuwa RAIS wetu. Na hatukuchagua RAIS ili ageuke malaika. Tunamnyima Rais fursa ya kunyenyekea.

KAZI IENDELEE
Asante bishop mungu akutunze ili waje watawala wema wakutumie.naomba nama Samia akutumie Kwa manufaa ya taifa tz
 
mawazo ya kitaalamu sana haya ila yatapigwa na waroho wa madaraka. ie halmashauri=kusogeza maendeleo kwa watu kupitia madiwani na Mikoa/Wilaya=kusogeza utawala kwa watu kupitia Rcs/Dcs
kiujumla wananchi tunahitaji maendeleo kuliko utawala ambao hauna matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi🙌🙌
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom