Tusikubali misaada ya uingereza kama kigezo ni kuhalilisha laana ushoga Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusikubali misaada ya uingereza kama kigezo ni kuhalilisha laana ushoga Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchakachuaji, Nov 3, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. m

  mchakachuaji Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UZEMBE NA UFISADI wa viongozi wetu ulichukua mimba na umezaa umaskini mkubwa nchini, nao umaskini ukakomaa ukachukua mimba unataka kilizalia taifa letu mtoto aitwae ushoga nao ushoga utalliua taifa na kulipeleka jehanamu. Watanzania wenzangu tusikubali ndoa za jinsa moja kwani vitabu vitakatifu vinaukataza badala yake tupambane na ufisadi na uzembe wa viongozi wetu ili rasilimali zetu zitusapoti la sivyo ADHABU KALI zaidi ya ILE YA SODOMA NA GOMORA inakuja. naomba kuwasilisha
   
 2. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Masharti ya kupata Misaada yaliyotolewa na David Cameroon Mkuu wa Uingereza yamenisikitisha sana,kunihuzunisha sana na kunifedhesha sana!
  Haiwezekani Tulazimishwe kuidhinisha USHOGA!Ushoga si kitu cha kuruhusu kwani ni Kinyume na Mpango wa MUNGU!
  "Misaada yote yenye masharti ya Kijinga tuikatae ikiwa tu misaada hiyo inatishia Heshima,Haiba,Utu na Hadhi ya Mtanzania"
  Turudishe Siasa ya Ujamaa na Kujitegema!Uwezo wa Kujitegemea na kutegemewa tunao
  Bora tumkaribie mungu kuliko Kumpromoti Shetani!
  Kamerooni Alaaniwe
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unaposema 'tuikatae' unamaanisha wewe na nani? Labda kama na wewe huwa unafaidika na hiyo misaada lakini ukweli unabaki kuwa mwenye maamuzi ya kukataa misaada ni yule 'anayefaidika' nayo.
   
 4. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Na Watanzania wazalendo kasoro Mwita 25!
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  beggars cant be choosers! tunatakiwa tukatae kuwa beggars, na uamuzi uko mikononi mwetu!
   
 6. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NICE PUNCH Mr. Mwita
   
 7. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 280
  Kwanza tukatae kuwa omba omba kabisa. Huku ni kudhalilishana؛
   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Dawa sio kukataa misaada yenye masharti ya kukubali ushoga. Tukatae kabisa misaada yoyote toka nje. Uwezo Tunao
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Waikubari tuu hiyo misaada maana mpaka sasa Ushoga unachukiwa sana lakini still unafanyika, na hata wakiikataa misaada ushoga utaendelea tuu.
   
 10. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Smart move son.. Thats de facto.
   
 11. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Na ww ni shoga nn? Tanzania hatutaki uendelee! ww unasema uendelee! Tabia mbaya hiyo!
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,119
  Trophy Points: 280
  Si ndio hivyo Labda huyu jamaaa anataka atufanye mashoga au kaona labda baadhi ya akina fulani wana vi-element vya ushoga.....
   
 13. Dogo Lao

  Dogo Lao Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Tutake tusitake, hakuna msaada unaotolewa kwa waafrika wenye lengo la kumwendeleza mtu mweusi. Kila misaada inalenga kuwanufaisha wao, kumpumbaza mwafrika na kumnyonya, kumtawala kifikra, kiuchumi, na hata kisiasa. Na hiz ndizo hasara kutegemea misaada! Suala hapa ni kuboresha uhusiano wa jumuiya za afrika, tusimame sisi kama sisi na kuwa na afrika moja, tunaweza kuinua uchumi na kuepukana na misaada yenye masharti haramu kama hayo.
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  afadhali tu nchi iongozwe na mapunga tujue moja kuliko sasa
   
 15. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Msije kushangaa ukipitishwa muswada kuhusu kutambua haki sawa kwa wote na hata makongamano yakafanyika kuwafundisha wananchi umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu (mashoga)!
   
 16. haggai32

  haggai32 Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Achaneni na Uingereza , acha kuwa omba omba....tuko waafrika zaidi ya bilioni moja sasa hivi hilo pekee ni mtaji tosha...we have to draw a line somewhere..
   
 17. f

  firehim Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi ni technique wanayoitumia Waingereza kupunguza misaada Afrika ili wajenge uchumi wa kwao. Dunia inaelekea pabaya watanzania tuliozoea kuomba hela ya matumizi itakula kwetu. Na bado. Watanzania tuamke tudai kodi zetu zinapotea bure kwa ufisadi.

  TIENI TIENI KWA MOYO MMOJA NAMBARI ONE NI CCM.
   
 18. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Swala la haki sawa ni kitu ambacho hakipo. Makowadi wa hiyo kauli mbiu ya haki sawa wamebadilisha msemo sasa wanasema ''haki ya ushiriki sawa''
  Halafu inaonekana nchi za ulaya kutaka kuyavuruga maumbile pesa zao nyingi wamekuwa wakizipitishia kwenye NGO's wanaojificha kwenye kivuli cha wanaharakati. Sasa tunawaomba wale wote wanaopigania haki za *******, waonyeshe mfano kwa kuwashawishi wana wao wa kiume kuwaliwaza mashoga walioko karibu nao.
  .
   
 19. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Binafsi nampongeza sana Cameron.Unajua tumekuwa tukilidhalilisha sana na misaaada, mfano net, kufadhiliwa kunawa mikono, yaani utadhani hatuna akili. Tunavokimbilia misaaada mpaka akili sasa haina ubunifu. Naomba Cameron asiishie tu maneno afanye kweli ili ituingie akilini na tuwasikilize wanao tukumbusha bila kuchoka kuwa hakuna maendeleo kupitia misaaada ispokuwa kudharilika na kudumaza akili ya kuendelea. Naomba wafadhiri wote waweke vipengele vya udharirishaji kwa waafrika kama kigezo kikuu cha misaaada. Kwanza tunawezaje kuikosoa uingereza. Kwanza tunajua nini? Maaana kama Uingereza tunamuona hayawani eti kwa kuuukubali ushoga je, sie wenye akili timamu mbona tunatembeza bakuli kwake? Sasa mtu anaye mpigia magoti hayawani si ndo hayawani mkubwa?. CAMWRON ASIYE KUBALI USHOGA MWACHE ALE JEURI YAK. Hivi hamjui misaada ya uingerza ni kodi ya ho mashoga mnao wapinga au yale yale ya Baniaan mbaya kiatu chake dawa.
   
 20. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tumelipuka kwa jaziba kuhusiana na pendekezo la Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron la kutaka nchi omba omba shart ziukubali ushoga kama kigezo cha kupewa misaada. Kinadharia ni udharirishaji. Lakini hebu tusumbue bongo zetu kiddoogo. Misaada tunayo ipata kutoka Uingereza si ni kodi za waingereza? Na mashoga si ni raia wa Uingereza? Kwa hiyo ni hivi; mashoga wa Uingereza wanatupatia misaada. Yaani misaaada ni mizuri ila mtowaji ni mbaya. Huu ndo upofu. Na tunapodai Uingereza inatudhalilisha, mbona yenyewe imehalalisha.

  Tunao uchaguzi mmoja ama kuacha kuwa omba omba kabla ya mengine makubwa hayajatukuta au tuufyate tudhalilike. Nakumbuka sana vitabu vya siaasa ya wakati ule vikiandikwa na Halimoja. Tangu shule ya msingi tulifundishwa kuwa misaaad ni hatari, kwa uhuru wetu, usalama wetu, akili zetu, maendeleo yetu na muhimi zaidi UTU wetu. Wakati tukifundishwa hivo tulihimizwa kujinyima anasa nakufanya kazi kwa bidii tukizingatia vipaumbele vya kutukomboa kiuchumi hadi tujitegemee. Shule ikawa lazima na bure, Sasaleo hii mnao ishangaa Uingereza nina swali moja kwenu; mlidhani waliotuasa kuwa misaaada inamadhara walikuwa waongo? Kama tunafika hatua ya viongozi kusimama na kuda bila aibu kuwa tumefanikiwa katika uongozi kwa kupata misaada zaidi. Eti tunaaminiwa ndo maaana tunasaidiwa. Haya bwana mashart ndo hayo na urafiki na wazungu ndio huo. Unavuna unacho panda ndugu zangu katika dunia hii. Hiyo ndo kanuni ya asili.

  Tunahitaji akina Cameron wengi maana dharau zao zaweza kutuzingua. Hebu ona, tunatenga hela kununua mashsngingi kila mwaka afu tunaomba neti za mbu. Tunafuta masoma ya afya (sayansi kimu) shuleni tunafundishwa na wazungu kunawa mikono. Afu tunasema tusidaririshwe. Tunajidharirisha wenyewe. Tumechagua misaada tutulia tuvune dharau na bado.Nyerere aliesema adhabu nyingine zimo ndani tendo lenyewe. Tuache kuangalia matokeo bila kuangalia chanzo. Tuimeze dawa chungu ya somo la Cmeron
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...