Elections 2010 Tusikubali kushindwa, ila tukubali matokeo

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Natoa maoni kama mpenda mabadiliko na mwanachama wa CHADEMA. Matokeo ya uchaguzi yametolewa, lakini katika hali inayoashiria kuwa hatukupata kile tulichostahili kupata.

Pamoja na hujuma tulizofanyiwa, nawaomba wanaCHADEMA wenzangu, tukubaliane na matokeo haya, lakini tusikubaliane na kushindwa kwetu. Ni dhahiri kuwa hata kwa upande wetu tulikuwa dhaifu katika kujipanga, kuhakikisha tunapata kile tulichostahili.

Binafsi naamini kweli tumeibiwa, lakini tukumbuke kuwa sehemu nyingi tuliacha milango ya nyumba zetu wazi, kibaka kapita kachukua bila hata mtu kumwona. Tujipange sasa ili next time, milango yetu iwe ya grill kiasi kwamba atakayetaka kutuibia, atafanya kazi kubwa, na uwezekano wa kupiga mayowe akakamatwa utakuwepo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom