UTANGULIZI
Pamekuwa na mijadala na minong’ono mingi juu ya kuporomoka kwa uelewa wa lugha ya kiingereza. Tafiti mbalimbali zimefanywa na watu pamoja na taasisi mbalimbali zikionyesha kushuka kwa umahiri wa kuzaungumzwa kwa lugha ya kiingereza. Na sababu kubwa kabisa ambayo imekuwa ikitajwa ni msingi mbaya wa elimu katika kumfanya mtoto kuwa mahiri katika lugha hii maarufu duniani.
Sababu hii ya msingi mbaya wa lugha katika mfumo wetu wa elimu pia ndio sababu inayotajwa kusababisha wanafunzi wengi kufanya vibaya lakini pia kutumia muda mwingi kukariri kuliko kuelewa. Na kwasababu kukariri ni kwingi kuliko kuelewa matokeo yake tunapata wahitimu wasio na ujuzi unaokusudiwa.
Hii inaonyesha kuwa wanafunzi wengi wanaofanikiwa kufaulu kidato cha nne na sita haina maana kuwa wanauwezo sana kuliko waliofeli isipokuwa wengi hufaulu kutokana na uwezo mkubwa walionao wa kukariri na sio kuelewa.
Wanafunzi mwenye msingi mzuri walugha ya kiingereza hatumii nguvu kubwa sana katika kujisomea kwasababu anasoma kwa kuelewa na si kukariri.
Tusikikimbie kiingereza tuwe wazi na tukubali tumekosea tujirekebishe ikiwezekana tukope ujuzi kwa waliotuzidi.
MSINGI MBAYA WA LUGHA YA KIINGEREZA NI SABABU YA AFYA DUNI YA AKILI YA WATOTO WETU
Kitendo cha mwanafunzi kutoka shule ya msingi na kuingia sekondari hajui kiingereza huwasababisha wanafunzi wengi kuwa na msongo wa mawazo unaowasababishia afya duni ya akili .Unaweza kuona mwanafunzi kabla ya kuingia sekondari anajiamini, amechangamka lakini ghafla anapoingia sekondari anabadilika,kujiamini kunaondoka na baadhi huchukia shule kabisa na kukata tamaa.Walimu wanapoingia madarasani uchangamfu wa waanafunzi hupotea. Tusione haya kukubali kuwa kiingereza kimetuacha,Tusifumbe macho kwakukwepa wajibu wetu na kujificha kwenye uzalendo .
UWEZO MDOGO WA LUGHA YA KIINGEREZA CHANZO CHA WENGI KUKIMBIA MAARIFA.
Umuhimu wa lugha ya kiingereza upo katika kupata maarifa mbalimbali.Maarifa mbalimbali duniani yapo katika lugha ya kiingereza.Huwezi kuwa mahiri katika fani mbalimbali kama hujajizoeza kusoma na kutafuta maarifa katika dunia ya wanaotumia kiingereza.Chanzo kikuu cha wasomi wetu kushindwa kujinoa katika maarifa mbalimbali ,tatizo ni uwelewa mdogo wa lugha ya kiingereza kwasababu maarifa mengi yamefichwa kwenye kimombo ambacho leo hii tunashawishiwa tukiache libaki tu kama somo.Swali la kujiuliza ikiwa sasa tunasomo la kiingereza kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba lakini bado kiingereza kinatupiga chenga ? Vile vile tunajifunza masomo yote ya sekondari kwa kiingereza isipokuwa Kiswahili inakuwaje bado kiingereza ni tatizo kwa watoto wetu? Bilashaka kwa maswali haya mawili utagundua tatizo lipo katika msingi wa lugha yenyewe inayochangiwa na mfumo mbaya wa elimu. Tusione haya kukubali kuwa kiingereza kimetuacha,Tusifumbe macho kwakukwepa wajibu wetu na kujificha kwenye uzalendo .
UWEZO MDOGO WA LUGHA YA KIINGEREZA UMETUFANYA TUSIJIAMINI KIMATAIFA
Pasipo kufahamu lugha kuu za kimataifa ni vigumu hata kufikiria kutafuta fursa nje ya nchi yako.Serikali inaposema itaongeza ajira kwa watanzania inapaswa kuangalia na uwezekano wa mtanzania kuajiriwa nje ya nchi yake anapokosa fursa hapa nchini.Kwasababu ya kutokujua vizuri lugha hii ya kimombo tumejikuta wengi tumejifungia hapa hapa ndani kwakukosa ujasiri wakutafuta ajira au fursa nje ya nchi yetu.Zinapotangazwa fursa mbalimbali ajira katika jumuya zetu kama EAC na SADC ni watanzania wachache sana wenye uthubutu wakuomba kwasababu tunajijua wenyewe shida ilipo.Kwa mfano hata kwenye fursa za kufundisha Kiswahili nje ya nchi bado kigezo namba moja uwe unauwezo wakuzungumza na kuandika kiingereza na wenzetu wakenya wanafaidi hiyo fursa kwasababu ya umahiri wao katika hiyo lugha. Tusione haya kukubali kuwa kiingereza kimetuacha,Tusifumbe macho kwakukwepa wajibu wetu na kujificha kwenye uzalendo .
HALI YA KIINGEREZA KATIKA SHULE ZA SERIKALI
Walimu wanashindwa kuhusiana vizuri na wanafunzi wakati wa ufundishaji .Unakuta mwalimu anashindwa kuwashirikisha vizuri wanafunzi kwasababu akiuliza swali kwa kiingereza wachache ndio wanaojibu.Akiruhusu mwanafunzi aulize swali wachache ndio wanaouliza.Hali kama hii huondoa hari ya mwalimu kufundisha na kuwasaidia wanafunzi.Walimu wengi wanauliza maswali mengi ya kutaja(mention na definition) kuliko ya kujieleza wakati wa kufundisha kwasababu wanaelewa watoto wetu hawawezi kujieleza kwasababu ya uelewa mdogo wa lugha ya kiingereza.
Pia baadhi ya walimu wanachangamoto ya umahiri katika kutumia lugha ya kiingereza katika ufundishaji.Hatuwezi kushangaa kwa hilo kwasababu walimu ni zao la mfumo wetu wa elimu hii inayozalisha walimu.Kiingereza ni tatatizo hadi vyuo vikuu.Wahadhiri baadhi lugha kwao ni tatizo kama ilivyo kwa walimu katika shule zetu. Tusione haya kukubali kuwa kiingereza kimetuacha,Tusifumbe macho kwakukwepa wajibu wetu na kujificha kwenye uzalendo .
TAFITI ZINASEMA NINI?
Tafiti mbalimbali zilizofanywa nchini Tanzania (Mlama na Matteru, 1978; Mvungi 1982; Tume ya Rais, 1982, 1983; Criper na Dodd, 1984; Roy-Campbell na Qorro, 1987; Simmonds na wenzie, 1991; Kadeghe, 2000, 2003; Brock-Utne, 2004, 2005, 2007; Galabawa na Lwaitama, 2005; Galabawa na Senkoro, 2006; 2003, 2007; Qorro, 1999, 2005; Vuzo, 2002, 2005, 2007; kwa kutaja chache tu), zote zimebainisha kuwa kiwango cha ufahamu wa wanafunzi katika lugha ya Kiingereza kwa shule za sekondari nchini Tanzania ‘hakifai kabisa kwa ufundishaji na ujifunzaji wa masomo mengine...’ (yaani, kama lugha ya kufundishia) ‘... kiasi kwamba suala hili halina budi kushughulikiwa haraka’ (Criper na Dodd, 1984: 72).. Hali hii inaonyesha kwamba kuna haja ya kufanya mapitio ya tafiti muhimu katika eneo hili ili kupata uelewa wa jumla wa matokeo na mapendekezo ya tafiti mbalimbali; na kuangalia uzito wa njia mbalimbali zilizopendekezwa katika kutatua tatizo hili.
NAMNA YA KUKUZA KIINGEREZA
Kiingereza na lugha zingine za kimataifa bado ni ajira kwa vijana wetu hata kama ni kidato cha nne.Kupitia mitandao kama utube na kozi za online kijana anaweza kujifunza mambo mazuri na kujiajiri kama atakuwa anauelewa mzuri wa lugha ya kiingereza.Kijana ambaye amemaliza kidato cha nne na anajua lugha ya kiingereza vizuri ,si rahisi kumkuta hana ajira labda awe na matatizo yake mengine.Binafsi nazishukuru shule za michipuo ya kiingereza nazile za kibinafsi kwakufanya kazi kubwa yakuokoa jahazi kwasababu vinginevyo hali ingekuwa mbaya sana.
Serikali ifanye nini kutatua tatizo hili la vijana wetu kutojua vizuri lugha ya kiingereza.
TUSIKITUPE KIINGEREZA KWA SABABU TUMESHINDWA KUKIFUNDISHA NA KUJIFICHA KWENYE UZALENDO WA LUGHA.Pamekuwa na mijadala na minong’ono mingi juu ya kuporomoka kwa uelewa wa lugha ya kiingereza. Tafiti mbalimbali zimefanywa na watu pamoja na taasisi mbalimbali zikionyesha kushuka kwa umahiri wa kuzaungumzwa kwa lugha ya kiingereza. Na sababu kubwa kabisa ambayo imekuwa ikitajwa ni msingi mbaya wa elimu katika kumfanya mtoto kuwa mahiri katika lugha hii maarufu duniani.

- Serikali ikiri bado tuna upungufu wa walimu wazuri wa lugha ya kiingereza. Ninaposikia serikali inadai ina walimu wa kutosha wa masomo ya sanaa binafsi huwa sikubaliani na jambo hilo kwasababu ni ukweli kwamba walimu ni wengi lakini umahiri katika kuzungumza kiingereza ni mdogo.Kwa hiyo serikaliinapaswa kuanza kuajiri walimu wa lugha ya kiingereza kwa kufanya usahili utakao zingatia uwezo wa mtu kimatamshi(pronunciation ) ,mtiririko katika kuzungumza(fluently) , misamiati inayoeleweka katika kuzungumza na kuandika pia.
- Walimu wa masomo mengine ya sekondari isipokuwa kiswahili nao inafaa sana wakifanyiwa usahili kujua uwezo wao katika kufundisha kwa kutumia kiingereza.Mwalimu mwenyewe akiwa na kiingereza kizuri na rahisi wanafunzi kujifunza kwake kwa njia ya kusikia lakini kitawavutia pia wanafunzi kuongea kiiingereza tofauti na sasa ambapo baadhi ya walimu wanamatamshi yasiyovutia hata kumsikiliza lakini hawawezi kuongea kiingereza kwa kutiririka hata dakika moja.
- Tukiona ni vigumu kuwapata walimu wenye sifa za kuongea kiingereza vizuri basis i vibaya tukiamua kuomba walimu kutoka mataifa mengine ambao wanaweza kufundisha na kuongea vizuri lugha ya kiingereza.
- Tunaweza kubadilisha utaratibu.kwamba wanafunzi wasome mpaka darasa la sita alafu darasa la saba liwe darasa maalumu kwa mwanafunzi kujiandaa na sekondari ,kwamba kwa mwaka mzima atakuwa anajifunza kiingereza tu na serikali iajiri waalimu maalumu mahiri na wenye ujuzi wakufundisha kiingereza kuanzia chini (bigginners) na kuendelea.Serikali ijenge madarasa ya kisasa kama Lab za lugha ambayo inaweza ikawa na vifaa vya kujifunzia lugha kama computer zenye software au video maalumu kwaajili ya kufanyia mazoezi ya kusikia na kuongea kiingereza.
- Tutafute waandishi wazuri au vitabu vizuri vya kujifunzia lugha ya kiingereza mashuleni tofauti na hivi vya sasa ambavyo vinaonekana ni vigumu kwa mtu anayeanza kujifunza lugha na hasa shule ya msingi kwasababu ya misamiati migumu na wakati mwingine mwanafunzi mwenyewe ni wa darasa la tatu au la nne.Kitabu kinapaswa kuwa na stori au hadithi chache na mazoezi mengi ya kuongea na kuandika kiingereza.
- Changamoto ya mtaala wetu wa shule za msingi ni kujikita kwenye sheria nyingi za lugha.Wanafunzi wanakazaniwa sana kujua grammer,tenses,structure na wakati hata lugha ya kunywea maji hata hajaijua bado.Kwa nini tusijikite kwenye kumfundisha mwanafunzi kujua kuongea kiingereza hata kama ni broken English alafu madarasa ya juu ndipo aanze kujifunza namna ya mpangilio ,sarufi n.k?Lugha yoyote watu huanza kujifunza kwa kukosea kosea ndipo hufuata ya kujifunza sheria na kanuni ya lugha husika,
- Watunga sera hawana budi kuchunguza upya malengo ya kufundisha lugha ya Kiingereza nchini Tanzania na kuyatofautisha na matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia. Wanapaswa kutangamanisha malengo hayo na sera ya lugha na mpango lugha ili sera na malengo hayo yaendane na ufundishaji madarasani