Ndugu zangu tusije tukajisahau na kujiziuka kwa sababu ya itikadi ya kisiasa. Kwa uzoefu wa miaka hii mitano. Hakuna mbunge wa CCM ambaye ataupinga mswada wa sheria kandamizi ulioletwa au utakaoletwa na serikali bungeni. HAKUNA.
Tumeona haya kwenye bunge la Ndugai na Tulia. Tumeona sheria nyingi kandamizi zikipitishwa na wabunge "Ndiyoooooo".
Tumeshuhudia marekebisho ya sheria ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu ikipitishwa kwa mbwembwe na ilivyokuwa kitanzi kwa watanzania.
Tumeshuhudia mjadala wa mabadiliko ya kikokotoo cha pensheni jinsi wabunge wa CCM walivyoitikia 'Ndiyooo' na kugonga meza. Kikototoo kandamizi kilisitishwa na rais mpaka 2023 ( watumishi wa kuelewa wataelewa)
Tumeshuhudia jinsi wabunge wa CCM walivyofurahia kuondoa FAO la kujitoa kwa kuitikia "Ndiyooo" huku wakipiga vigelegele, vifijo na kugonga meza. Mabadiliko haya yamekuwa ni kitanzi cha vijana kushindwa kujiajiri na kuajiri wengine.
Tumeshuhudia sheria mbalimbali kandamizi zikishangiliwa na wabunge wa CCM na kupitishwa kwa mbwembwe, bashasha, na furaha kama vile wapo kitchen party.
Sheria hizi zimekuwa ni vifungo na kuleta mateso makubwa kwa watanzania waliowachagua hawa wabunge kwa upendo mkubwa.
Bahati mbaya wabunge hawa wanakitumikia zaidi chama na serikali kuliko kuwatumikia wananchi.
Hivyo ndugu zangu, tusijisahau na kujiziuka. Hawa wabunge wa CCM watatuongezea mateso yetu kwa kusema Ndiyooooo pale serikali itakapopeleka mswada kandamizi na wa kuwatesa watanzania.
Tusijisahau, tusijiziuke. CCM ni ile ile, na wabunge wa CCM ni wale wale.