Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Siku zote wahenga wanasema usiache mbachao kwa msala upitao. Pia wahenga wanasema usitupe jongoo na mti wake.
Kwa sasa wafuasi wa CHADEMA mitandaoni tumeanza kampeni tuliyoipa jina la TUNDU LISSU FOR PRESIDENCY 2020. Kampeni hii inalenga kumjenga TUNDU LISU kisiasa ili awe mgombea Urais kwa tiketi ya chama chetu Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa kuamini kuwa ni mtu pekee ndani ya chama anayeweza kumudu Rais Magufuli. Mkakati huo pia unalenga kumjenga Tundu Lissu kisiasa ili awe Mwenyekiti wa chama kwenye uchaguzi wa ndani unaotarajiwa kufanyika 2019. Binafsi sioni tabu ya Lissu kugombea kwani ni haki yake kidemokrasia na ana sifa. Tabu ninayoiona ndani ya CHADEMA ni pale tunaposahau wapi tumetoka.
Kwa sasa hatima ya Edward Lowasa kisiasa haijulikani ingawa ni yeye ndiye aliyetupa mtaji mkubwa wa wabunge tunaotamba nao kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Tusidanganyane, Lissu anaweza kuwa maarufu kwa upande mmoja ila si kwa nafasi ya Urais. Mimi nikiwa mfuasi na mwanachama makini wa CDM, nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Lissu atatuvusha salama 2020.
Nikija kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama, Kamanda Mbowe ameitendea haki nafasi hiyo. sioni mbadala wake ndani ya chama. Tusijidanganye kufanya majaribio ya nafasi hiyo kwa kumpa mtu wa kutoka Ikungi. Atakiharibu chama chetu na kitapotea kisiasa. Wapi ilipo NCCR Mageuzi ya Augustino Lyatonga Mrema? Mnataka CHADEMA iwe kama NCCR ya James Mbatia? Ni Mbowe pekee ndiye anayefaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ya sasa na natamani aendelee kuwa kwenye nafasi hiyo hadi umauti wake au atakapoamua yeye mwenyewe kuacha. Hivi mnajua kwa nini tulibadili katiba ya chama mwaka 2004 kinyemela ili Mbowe awe Mwenyekiti wa kudumu? Mnajua? Tulifanya vile kimya kimya kwa maslahi mapana ya chama. Matunda yake yanaonekana sasa
Niwasihi makamanda popote mlipo. Sumu haionjwi kwa kulambwa. Tutaangamia