May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Siku hizi imekuwa kama sifa kumsikia Mtu akijinadi kuwa yeye ni bingwa wa kuagiza bidhaa kutoka China au sehemu nyingine ya Dunia.
Kwa vyovyote Mtu kama huyu hawezi kufurahi akisikia mipango yoyote ya Nchi kutengeneza bidhaa zake yenyewe, na atafanya kila linalowezekana kuhujumu juhudi kama hizo.
Kama nchi ni lazima kuwe na mikakati mahsusi kuhakikisha nasi tunakuwa Watengenezaji maana ni hakika nguvu ya kupinga inaweza kuzidi nguvu ya kutekeleza.
Inasikitisha ukipita Mtaani unakuta 99% ya bidhaa alizobeba Mmachinga ni bidhaa kutoka nje ya nchi.
Hivi kweli bidhaa kama Soksi, Nguo za ndani, mikanda ya kiunoni, vifaa vya usafi n.k vyote ni mpaka tutengenezewe na Wengine?
Mbali na kutatua tatizo la ajira na uchumi pia ni heshima kwa nchi kama tukijitengenezea bidhaa zetu wenyewe.