Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,862
- 5,680
Miaka 20 iliyopita tarehe 14 Oktoba 1999 Taifa lilikuwa katika majonzi mazito. Kipindi hicho nikiwa na miaka 20 hivi namaliza kidato cha nne mkoani Mbeya.
Tangazo la Mh. Benjamin W. Mkapa kuwa Baba wa Taifa Mwl. J.K.Nyerere hatunaye tena ilikuwa kama ni ndoto za alinacha na hakuna raia aliyetaka kuzikubali taarifa zile kupitia ITV.
Wakati Mh. Mkapa anasisitiza wananchi kuwa watulivu amani itadumu na kila kitu kiko under control nilikuwa natamani asiendelee kutupa habari hizo maana ananipa woga na simanzi zaidi. Sikuwa naona kitu mbele zaidi ya Giza na hofu.
Nyerere hakuwa Rais, ila uwepo wake, ushauri wake, Matendo yake Uzalendo wake na Maono yake, kwa taifa yalikuwa ni zaidi ya kuwa kiongozi wa taifa.
Maswali yalikuwa mengi kuliko majibu.
Tutampata wapi mtu kama Nyerere atakaye weza kushauri, kukosoa kuonya na kutupa matumani mahali ambapo tumekosa Matumaini?
Nyerere alikuwa na kipaji cha kipekee sana. Hii iliwafanya watu wengi tuamini maisha bila Nyerere ilikuwa haiwezekani. Matendo yake na maneno yake yalifanana hasa anapozungumzia maendeleo, utu haki na usawa.
Giza lile nililokuwa nikiliona na kulihofu miaka ishirini iliyopita sasa linaonekana dhahiri kutamalaki katika nchi yetu ya Tanzania. Utu umetoweka na umebakia unyama unyama tuu.
Taratibu taifa letu limeanza kufurahia unyama na matendo ya uovu kwa binadamu wenzetu. Amepigwa Risasi Tundu Lissu kinyama sana wapo watu walioshangilia unyama huo. Na hakuna hata Nzi aliye kamatwa mpaka sasa kuhusika na tukio hilo. Ametenguliwa ubunge Tundu Lissu pia wapo watu wameshangilia haki yake hiyo kupotea.
Juzi na jana zilizuka taarifa ya hali ya afya ya kiongozi wa nchi kuwa mbaya. Wapo watu walidiriki kuombea kusikia amekufa tena wakishangilia na kusubiria kwa haamu kupewa uhakika wa tukio.
Hili sio jambo la kawaida katika siasa za Dunia ya ustaarabu na utu. Kuna nyufa zimeonekana na tukiendelea kuzitikisa sisi sote tupo hatarini hakuna wa kupona.
Hii ina maana sasa hivi watu wakisikia ikulu imelipuliwa hawatajali kabisa zaidi watauliza tuu fulani kafa? Ni kwa nini tumefika hapa?
Tusijidanganye kuwa chuki hii inatokana na wahujumu uchumi au sijui mafisadi ambao taifa linapambana nao. Huo ni uongo na unafiki uliutukuka.
Hakuna kiongozi aliye pambana na mafisadi kama Nyerere mpaka kuweka Azimio la Arusha. Kwa miaka mingi aliyo ongoza Nyerere angepaswa kuwa na Maadui wananchi wengi kuliko kiongozi yeyote yule hapa Tanzania. Hakuna wa kujifananisha na Nyerere na hata kumfikia kwa robo tuu.
Viongozi wa sasa wanahamasisha chuki na ubaguzi miongoni mwetu raia na Matunda ya chuki hiyo tumeanza kuyachuma na kuyala sasa.
Tutampata wapi Nyerere kwa sasa aweze kutuonya, kutukaripia, kutusahihisha? Nyerere alikuwa na Kariba ya kipekee ya kiuongozi.
Kikwete alijaribu kuongea kidogo tu hivi karibuni katika Nyerere Day alicho kipata anakijua. Mtu kama Ally Hapi anajitutumua na kutaka kujibizana na Rais mstaafu huku akijiapiza kuwa yupo tayari kupambana na kiongozi mkuu wa nchi aliyestaafu.
Tusipo ziba ufa tutajenga ukuta.