Tusiilaumu tu CHADEMA!! Tuweni sehemu ya mabadiliko tunayoyataka!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiilaumu tu CHADEMA!! Tuweni sehemu ya mabadiliko tunayoyataka!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Moseley, Nov 16, 2010.

 1. Moseley

  Moseley Senior Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kama kuna kitu kinanisikitisha, ni kuona wana-JF wanaotupia lawama kwa CHADEMA kwa kutomtambua Rais. Wengine wakidai, kama CHADEMA haimtambui Rais, basi haina haja ya wao kuruhusu wabunge wao kuhudhuria vikao bungeni..

  Wengine wanailaumu kuwa kwanini wametoa tamko hilo kwenye tafrija?? Wakimaanisha kuwa mantiki ya tamko hilo imeharibiwa, kutolewa katika tafrija

  Wengine wakisema Doctor wa Mezani kawa Rais kihalali maana wananchi wamekaa kimya wamemkubali. Wengine wakidai kuwa kama watu hawamkubali Rais, wangeandamana kupinga (Wakati huo huo wanasahau yaliyotokea Kenya)

  Kuna mifano mingi naweza kuitaja, Ila napenda kuwauliza wanaJF, kwanini tunatupa lawama kiasi hicho kwa CHADEMA? Why??

  Cha msingi tulitakiwa kuwa sehemu ya mabadiliko. Swala la Uchaguzi huru na wa haki si la Mbowe wala Slaa wala si swala la CHADEMA, ni swala linalotugusa sote..

  Kama unaona ya kuwa CHADEMA wanacheza katika maamuzi yao, acha lawama, ingia ulingoni na tetea haki ya wanyonge..

  Haya maswala ya kufikiria kuwa CHADEMA ndio pekee italeta mabadiliko yanaweza yasitufikishe popote, maana sisi tunabaki kubwabwaja tu bila kuiunga mkono, au kuchukua hatua thabiti pale tunapoona nguvu yetu inahtajika..

  Tuache lawama, tuingieni katika kudai haki zetu. Sio kutupa lawama tu hapa JF..

  Tuache mawazo hasi, CHADEMA imeonesha njia.. Sie twahitajika kufanya sehemu yetu, lawama hazitatufikisha popote!!!!
   
 2. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii inaonyesha jinsi gani watanzania tulivyo longo longo,inapofikia kwenye utekelezaji wa mambo ya msingi kama hili watu wanaingia mitini.Sasa hapa tunawakatisha tamaa hata wenye mwamko wa kweli pale wanapojikuta wako wenyewe.Hili wazo la Moseley ni zuri jamani tulipe uzito,tunaomba fikra zenu na support wanaJF.
   
 3. l

  len Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mosleley kasema kweli kabisa, Chadema wameonyesha njia na kama walivyosema jana mapambano yanaendelea. Sisi wenyewe tuwe sehemu ya mapambano hayo tukijiandaa kwa uchaguzi ujao. Wananchi tuamke tudai katiba mpya ili uchaguzi ujao uwe kweli huru. Tutafakari kwa nini watanzania wengi hawakujitokeza kupiga kura na nini kifanyike. Tudai tume huru ya uchaguzi ambaya pamoja na mambo mengine itaweka utaratibu rahisi wa watanzania kujiandikisha / kupata shahada walizopoteza, kuabadilisha vituo cya kupiga kura n.k
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Labda sisi wapenda mabadiliko tunapaswa kufahamu ya kuwa hawa wakina Dr. Slaa na wenzake ni waongoza mapambano ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kimfumo na kiutawala tunayoyatarajia na sio kweli kwamba wao wenyewe watafanikiwa katika hili. K

  WA KWELI NAUNGA MKONO HOJA na kuwaomba wana-CDM wote na wale wapenda mabadiliko. Cha kufanya kwa sasa ni kutoa ushauri wa msingi na wenye kujenga kwa viongozi wetu hawa na naamini kwa kuwa wametoa kipaumbele kwa nguvu ya umma basi watatusikiliza na mapambano yatakuwa kwenye mstari.

  Mosley umetoa ushauri muhimu na mimi niko njiani kutoa mchango wangu wa kuchangia mabadiliko tunayoyataka. JE WEWE MWANA JF Mpenda mabadiliko uko tayari??? na uko tayari kwa kiasi gani kujitolea katika kuleta mabadiliko haya??

  Mabadiliko ni gharama, tujiandae kuilipa kwa faida ya vizazi vyetu vya sasa na pia baadae na sio CHADEMA
   
 5. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwana JF na wengine kazi ndio inaanza, kuna njia mbili tu

  1. Uunge mkono mabadiliko na kusonga mbele kufikia mabadiliko
  2. Uache kuunga mkono na uende upande wa pili (old and conservative)

  Note: usiwe vuguvugu (katikati), na kama upo hapo waaache waliodhamiria wasonge mbele
   
 6. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Message sent to Rev Kishoka and co!
   
Loading...