Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,185
- 18,513
Kundi ambalo hadi Leo bado linaiabudu CCM ni kina mama, na wazee karibia wote, ukimwona kijana yuko na CCM ujue akili zilishachotwa.
Wazee utakuta analalamika lakini mwisho hataki kukubali kuwa matatizo yote haya yanatokana na CCM, nguo na T-shirt wanazo pewa basi wanaona inatosha.
Vijana sasa ni wakati wa kuwaelimisha na kuwahamisha hawa kina mama na wazee kifikra waachane na chama fisadi hiki.
Naamini kama kila kijana akimhamisha mzee mmoja hadi 2020 CCM itabaki tupu.
Kazi imeanza, nyumba kwa nyumba.