Tusiichukie Tanzania bali tuwachukie viongozi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiichukie Tanzania bali tuwachukie viongozi wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KiuyaJibu, Jan 16, 2012.

 1. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Hebu tafakari kuhusu baadhi ya matukio yaliyotokea kuhusiana na matumizi ya raslimali za taifa changa kiuchumi duniani (Tanzania)
  Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru Tanzania bara (Tanganyika) zimetumika Tshs 57 billioni;
  Maadhimisho ya miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar (Tanzania visiwani) zimetumika Tshs 700 millioni;
  Kuuzwa kwa Celtel Tanzania Limited chini ya Celtel Tanzania B.V. Tanzania kama nchi imepoteza/ilipoteza kiasi cha kodi ambacho kilipaswa kuchukuliwa kutokana na mauzo hayo (capital gain) ya dola za kimarekani million 300.Wakati wenzetu Kenya, Zambia, na Nigeria wao walisimama kidete na kuhakikisha mwekezaji analipa hiyo fedha na walifanikiwa ila kwa Tanzania, akaendelea kuwa mnyonge na kupoteza hiyo fedha bila hata kujiuliza wenzetu waliokuwa na mwekezaji huyohuyo wanafanya nini katika uuzwaji wa kampuni.
  Kwa wakati huo, hiyo fedha ingechululiwa na kuipeleka labda katika kutatua tatizo la umeme basi Tanzania isingekumbwa na tatizo la mgao wa umeme.
  Au kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami,kwa kipindi hicho kilometa 1 ilikuwa ni Tshs 1 billioni; japo baada ya kuingia Dr.Magufuli akashtukia janja ya makandarasi na akashusha gharama mpaka Tshs 800 millioni kwa kilometa moja ya kiwango cha lami.
  Mchezo wenye uko hivi: Celtel Afica→Celtel Tanzania B.V. →Celtel Tanzania Ltd→Zain→Airtel; hili ni suala off-shore companies. Zinafanya sana usanii na hasa ikikuta sehemu ambayo sheria zake ziko legelege na hakuna uwajibikaji wa kweli; hapo lazima mapato yapotee kwa njia moja ama nyingine.

  Mengineyo:
  Kupanda kwa posho za wabunge kwa kigezo cha gharama na ugumu wa maisha katika mji wa Dodoma;

  Kupanda kwa gharama za umeme;

  Kupanda kwa gharama za kivuko cha Kigamboni kutoka Tshs 100 hadi 200/=;ferry(kivuko) katika nchi nyingi ni huduma inayotolewa bure mfano ni Afrika ya Kusini.

  Tatizo letu kubwa watanzania ni hatuna uwajibikaji wa kweli kuanzia juu hadi chini na ufuatiliaji duni wa masuala yenyewe maslahi kwa taifa.

  Kwa mambo kama haya hivi ni kweli tuna viongozi ambao wanataka maendeleo ya kweli au ni kuongea tu majukwaani na vyombo vya habari.
   
Loading...