Tusiiangalie pesa kwa tarakimu zake bali kwa PURCHASING POWER yake – Money Redefined! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiiangalie pesa kwa tarakimu zake bali kwa PURCHASING POWER yake – Money Redefined!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Revolutionary, Feb 26, 2011.

 1. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Part 2

  Shukrani kwa wanajamii ambao mlichukua adha ya muda wenu kusoma sehemeu ya kwanza ya topic hii (https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/112091-tusiiangalie-pesa-kwa-tarakimu-zake-bali-kwa-purchasing-power-yake-%96-money-redefined.html).

  Kwa wale wanajamii wenzangu ambao mlikua mnasubiria sehemu ya pili ya topic hiyo leo nitawaletea kwenu sehemu hiyo ya pili ambayo inakwenda kama ifuatavyo;

  ......Kuna watu ambao kutwa kucha kazi yao ni kufuatilia matukio mbali mbali duniani na namna matukio haya yanavokuwa na uhusiano (implication) na kupanda au kushuka kwa thamani ya fedha katika wakati huo.

  Mfano leo wakiona maandamano Misri au haya yanayoendelea Libya wanajua mandamano hayo yana faida au hasara gani kifedha na hivyo huweza kuitumia fursa hiyo kuchukua hatua madhubuti kujizalishia pesa, kujiimarisha kifedha na kujikinga wasipate matoke hasi kutokana na matukio hayo.

  Taasisi mbalimbali za kifedha kama benki hufanya haya pia kwa kuwatumia wataalam wa mambo ya fedha na uchumi.

  Wenzangu na mimi tusiokuwa na ufahamu katika mambo haya ndio tuliwao, kwani tupo wengi tusiokuwa na maamuzi sahihi katika fedha zetu na hivyo siku zote huwa inakula kwetu.

  Kwa mfano mdogo tu, unapoweka shilingi 1,000,000 zako katika akaunti yako ya akiba (savings account) katika benki inayotoa riba ya aslilimia tano (5%) kwa mwaka. Mwishoni mwa mwaka utakuwa na faida ya Shilingi 50,000 zaidi katika akaunti na kufanya uwe na jumla ya shilingi 1,050,000 (yaani kianzio 1,000,000 + Faida 50,000 = 1,050,000).

  Kwa kuwa kuna aina kadhaa za riba, nahii ya 5% hapo juu ni ‘NOMINAL RATE’ na ndio ambazo hutolewa na benki nyingi kama riba ya faida ili kukuvutia uweke fedha zako kwao. Kumbe basi kama kiwango cha mfumuko wa bei (Inflation rate) mwaka huo ni asilimia mbili (2%) Ingawa kiwango chako cha fedha katika akaunti yako kitakuwa kimeongezeka kwa 5% kama nilivyoeleza hapo juu lakini ki ukweli kwamba pia thamani ya pesa yako imeshuka kwa 2% interms of its PURCHASING POWER kutokana na mfumuko huo wa bei (inflation).

  Kwa hivyo katika lugha rahisi ni kusema ingawa Pesa yako ndio imeongezeka kwa 5% lakini thamani yake imeshuka kwa 2% na hivyo riba halisi uliyopata ni 3% tu na sio 5% kama unavyoambiwa na benki. Hapa hii 3% huitwa ‘REAL RATE’
  Faida halisi unayoipata benki ni 1,000,000 x 3% = 30,000 (elfu thelathini tu).

  Ingawa hii faida ya 3% uliyoipata si haba na ndio maana ukaiweka pesa yako benki ili iweze kubakia na PURCHASING POWER kubwa maana bila hivyo kama ile 1,000,000 usingeipeleka benki kiuhalisia ingeshuka thamani kwa 2% yaani 1,000,000 x (1-2%) = 980,000 kutokana na mfumuko wa bei (INFLATION) na thamani halisi ya hiyo 1,000,000 sasa itakuwa ni 980,000 (ukilinganisha na PURCHASING POWER kwa sasa).

  Kwa kuwa hakika hatuwezi kutabiri hali ya uchumi na wakati mwingine kama kunatokea anguko kubwa la uchumi (RAPID INFLATION) kama ilivyotokea hivi karibuni duniani kote na hupelekea kupungua kwa kiasi kikubwa kwa uwezo wa mtu kufanya manunuzi (PERSON’S PURCHASING POWER) ingawa au hata kama riba inayotolewa na benki ni nzuri kiasi gani.

  Misamiati hii ya riba (NOMINAL & REAL RATES) hutumika katika maeneo mbali mbali kiuchumi kama kulipa mishahara, matumizi ya serikali, riba za benki, mikopo nk kwa uchache......
   
 2. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  mkuu endelea kushusha nondo ili tupate maarifa .asante
   
 3. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante Miundo Mbinu tujaliane afya ili tuendelee kujuzana!
  Ukweli ni kwamba nawashauri muwekeze fedha zenu sio tu kuziweka benki. kwa kuwa tunapoweka fedha zetu benki kwa wingi wetu tunawapa hao benki investment power kubwa, wanatumia wingi wa fedha zetu kuwekeza, wanapata faida kubwa na wanatugawia sisi faida kidogo ambayo ni sawa na bure (binafsi sijawahi hata kuhisi kama kuna faida huwa inawekwa kwenye akaunti yangu). na juu ya hayo wanatuchaji na service/ledger fee kila mwezi (benki yangu wanachaji 5000, kwa mwaka yaani 5000x12=60,000, si haba).
  kuweka hela benki bila mantiki ni upunguani na upom pom po mtupu!
   
Loading...