DaveSave
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 440
- 637
Tujiulize, Magufuli aliyekwenda kwa Kagame kwa barabara akirudi atakuwaje?
Ndugu zangu,
Wahenga walisema, tembea ujionee, ina maana tembea ukijifunza. John Magufuli anajenga ubia na Paul Kagame. Urafiki wa John na Paul, na atakayojifunza John kwa rafiki yake Paul, yamkini yataongeza maradufu kasi ya John Magufuli kutumbua majipu.
Kagame pamoja na kuitwa dikteta, lakini ameibadilisha Rwanda na inaelekea kuwa nchi ya kisasa zaidi. Siri kubwa ya mafanikio ya Rwanda ni kwa Kagame kuwafanya Wanyarwanda kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za nchi. Kujenga misingi ya uadilifu na kuisimamia. Na wenye kukiuka kuadhibiwa. Ni kwa viongozi na raia.
John Magufuli ameanza kuijenga misingi hiyo hapa nyumbani, na kwa atakayoyaona kwa rafiki yake mpya Paul Kagame kule Kigali, basi, John Magufuli njiani akirudi nyumbani atakuwa akijisemea.
Yaani, kanchi kadogo aka ka Rwanda, hakina hata bandari wala migodi ya madini katupite hivi hivi kwa vile sisi tumekubali kuyafuga mafisadi...uwiii!"
Goodmorning.
Maggid.