Elections 2010 TUSIFURAHIE KIUINGIZA WABUNGE WENGI WA UPINZANI (tafakari)

Kiherehere

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,807
621
Baada ya kufanikisha uchaguzi uchwara na kupelekea wabunge wa CHAMA MAKINI (chadema) kuingia kwa idadi kubwa wengi wao wakiwa wabunge wadadisi na shupavu, CCM sasa walivyo na fikra za kishenzi wanataka kuhakikisha speaker SITA harudi kwenye kiti chake.
Tutakubaliana wote kuwa SAMWELI ndo alifanya bunge la tisa kwenda kwa viwango kwa kuruhusu mijadala, CCM wanataka kumuweka SPEAKER ATAKAYE ZUIA MIJADALA ILI FISADI KIKWETE ATAWALE ANAVYOTAKA.
Tuombane kwa kushirikiana SITA ARUDI KWENYE KITI CHAKE kinyume cha hapo, miaka mitano ijayo hutamsikia,Shibuda,Lisu,Kabwe,Mnyika,Mbowe,Mdee na wengineo ikiwa ni kampeni ya kutowapa fursa nzuri ya kujadili hoja tata.
Tafakari iwapo Chenge akashika uspika afu hoja ya rada iingie!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
78
nadhani bungeni kuna kanuni na sheria za mijadala hivyo basi akikaa mtu yoyote ili mradi kanuni na sheria zinafuatwa mambo yote yatakwenda sawa!
 
Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
Wasiwasi wa bure. Tuna imanii wabunge wetu, watatuchagulia Spika makini.
 
Oct 29, 2010
25
7
Wabunge gani hao ulio na imani nao? Ni hao wa CCM ambao wengi wao ubunge wameupata baada ya uchakachuaji wa kura? Nakubaliana na mtoa hoja, kwamba kuna umuhimu wa kuhamasisha wananchi ili achaguliwe spika mwenye nia njema na muelekeo wa nchi hii na si "kibaraka" wa chama tawala. Wengi tunafahamu jinsi Mhe Sitta (CCM) alivyoweka hatarini nafasi yake katika chama, kwa uendeshaji wake mzuri wa bunge, na faida yake leo hii wapinzani tunaiona. Sitoshangaa kama vigogo wa CCM wakimuweka "kibaraka" ambaye atakuwa akifuata maelekezo ya chama badala ya matakwa ya wananchi.
Jamani, kuna umuhimu wa kuhamasishana na hili jambo la spika wa bunge lina umuhimu wake, kwani hata katika uchaguzi wa Rais kanuni za kufuatwa zilikuwepo, na uchakachuaji ukafanyika, leo hii iweje tuseme hayo matunda ya uchakachuaji, yatafuata kanuni yatakapofika bungeni? Tusipokuwa makini nguvu zetu zitapotea bure.
 
kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
360
wasipochagua spika mzuri na wakachagua asiyefaa kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wa Sita,, basi ittakuwa kiama chao na wapinzani watachekelea zaidi 2015
 
kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,216
4,838
Sisi CHADEMA tumejipanga yeyote atakaekuja tutapambana nae tu. usicheze na peoples power wewe.
Tena akija speaker dhaifu ndo atauona moto hadi atalikimbia bunge usilete mchezo na timu ya CHADEMA iliyoingia sasa tena ina hasira na uchakachuaji wa kura we acha tu. Na kwenye viti maalumu tutaingiza wanawake wa kazi kama akina Suzan Lyimo, Lucy Owenya na wengine kibao hakuna kulala bunge la mwaka huu. We are ready for any speaker kwani sheria na kanuni za bunge tunazifahamu ndo maana ni chama cha wasomi chini ya ushauri wa prof Baregu na wala sio makamba mwalimu wa UPE
 
Kiherehere

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,807
621
kimtazamo ni kwamba spika anao uwezo wa KURUHUSU HOJA IJADILIWE au KUIZIMA KABISA, ni kama ulivyosikia katika moja ya mahojianao ya Raisi Wa JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. Dr, Peter Wilbroad Slaa alipokuwa akitoa hoja baada ya Uhasama(usalama) wa Taifa kujibu madai yake. Yeye alisema kuwa usalama ulijaribu kuzuia hoja ya EPA isiingizwe bungeni kwa kupitia Dr. Slaa, lakini spika makini aliruhusu.So mtu kama Chenge sina uhakika nae... au Lowasa au vibaraka wengine..
 
mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Kama wabunge wawe wa CCM hata misukule watamchagua huyu fisadi nao moja kwa moja watakuwa wamejigeuza nepi ya mafisadi. Si haba idadi ya wabunge wa upinzani wanaweza kusaidia kuzuia huyu habithi kuwa spika.
 
Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
225
Baada ya kufanikisha uchaguzi uchwara na kupelekea wabunge wa CHAMA MAKINI (chadema) kuingia kwa idadi kubwa wengi wao wakiwa wabunge wadadisi na shupavu, CCM sasa walivyo na fikra za kishenzi wanataka kuhakikisha speaker SITA harudi kwenye kiti chake.
Tutakubaliana wote kuwa SAMWELI ndo alifanya bunge la tisa kwenda kwa viwango kwa kuruhusu mijadala, CCM wanataka kumuweka SPEAKER ATAKAYE ZUIA MIJADALA ILI FISADI KIKWETE ATAWALE ANAVYOTAKA.
Tuombane kwa kushirikiana SITA ARUDI KWENYE KITI CHAKE kinyume cha hapo, miaka mitano ijayo hutamsikia,Shibuda,Lisu,Kabwe,Mnyika,Mbowe,Mdee na wengineo ikiwa ni kampeni ya kutowapa fursa nzuri ya kujadili hoja tata.
Tafakari iwapo Chenge akashika uspika afu hoja ya rada iingie!!!!!!!!!!!!!!!!!

Chenge akipewa uspika hii nchi hii itatengwa na EU mara moja!!!!! pengine hata na USA! Navyowafahamu, hawawezi kuubali kitu kama hicho kutokea hapa -- mtuhumiwa wa rada, ambao wao kule wana ushahidi kamili-- katika suala lililojadiliwa Bungeni hapa -- na Bunge la Uingereza pia --AWE SPIKA wa Tanzania?

CCM wala wasijaribu hivyo. Najua yeye Chenge anataka uspika ili azidi kujijengea kichaka cha kujifichia. Mamlaka za wenzetu kule siyo wa hovyo vovyo kama wa kwetu hapa.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Bila spika makini imekula ndugu zangu, la msingi tumwombe mungu atusaidie apite mtu makini kama vile Samwel Sitta au Harrison Mwakyembe.
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
12,619
11,297
Wananchi wahamasishwe ili wawalazimishe wabunge wao wachague Spika atakayeweka maslahi ya Taifa mbele na sio yA CHAMA!! Sitta angefaa ingawa alikuwa na mapungufu yake kipindi kilichopita; hayo safari hii nadhani atayarekebisha!!
 
tripojo

Member
Jan 4, 2008
61
6
nadhani bungeni kuna kanuni na sheria za mijadala hivyo basi akikaa mtu yoyote ili mradi kanuni na sheria zinafuatwa mambo yote yatakwenda sawa!

Mafisadi wanajua cha kanuni basi! Mbona sheria zimekuwapo siku zote lakini mafisadi wanakiuka na hawachukuliwi hatua zozote! I can't imagine mzee wa vijisenti kuwa spika....nahisi nitasahau kuangalia kipindi cha bunge kwa miaka yote mitano!!
 
Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,325
64
Tanzania kila kitu si kinachakachuliwa..
hata spika atapatikana baada ya uchakachuzi.
Tusitegemee jipya, system yote imeoza, thanks God tuna watu makini kama Dr Slaa anaetamka maovu yao mengi bila kumung'unya maneno.
Big up Dr Slaa, Mungu ukupe nguvu na hekima zaidi
 
rmashauri

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
3,011
448
Nafikiri CCM na ubovu wao hawataruhusu fisadi Chenge achaguliwe kuwa spika. Tusubiri Jumatatu tuone kama watampitisha.
 
superfisadi

JF-Expert Member
May 22, 2009
553
51
mi nadhani suala la msingi ni kwa wabunge wa ccm kuombewa mungu wasikubali kurubuniwa hasa kipindi hiki walichochoka mifukoni kutokana na kumalizia hela kwenye majimbo yao kwa kuhonga hivyo nao wanahamu ya kuhongwa na kutoa kura kwa mafisadi ambao fedha zao hazikauki kwa kuwa hakuna upishi spika atakayepita ni yule anayetakiwa na CCM kwani wao ndio wengi bungeni na ndiyo wenye maamuzi:nono:
 
Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
297
kimtazamo ni kwamba spika anao uwezo wa KURUHUSU HOJA IJADILIWE au KUIZIMA KABISA, ni kama ulivyosikia katika moja ya mahojianao ya Raisi Wa JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. Dr, Peter Wilbroad Slaa alipokuwa akitoa hoja baada ya Uhasama(usalama) wa Taifa kujibu madai yake. Yeye alisema kuwa usalama ulijaribu kuzuia hoja ya EPA isiingizwe bungeni kwa kupitia Dr. Slaa, lakini spika makini aliruhusu.So mtu kama Chenge sina uhakika nae... au Lowasa au vibaraka wengine..

Hapo kwenye red, Sitta alimkatalia Dr Slaa then aliamua kupeleka hoja kwa wananchi.

Sitta na hao kina chenge hawana tofauti sana, namwona Sitta kama mnafiki vile na geugeu.
 
Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
297
CCM hawawezi kumchagua spika makini, kwani wanataka spika atakayeweka maslahi ya CCM kwanza; hivyo Chenge kwa CCM ndiye atakayewafaa zaidi. CCM ni wahuni. hata Sitta na kina Kilango wanamtaka atakayeweka maslahi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom