Tusiende mbali kuhusu hisa

Richardbr

Senior Member
May 29, 2011
110
25
Kwanza tuambiane kwa mliokwisha wahi kufanya biashara ya hisa na hasa tunapozungumzia faida,hivi tuwe wakweli ili hatimae tupime wenyewe na tuamue na sisi ambao tunafikiria kuhusu hisa tufanye maamuzi sahihi,swali linakuja kama ifutavyo.

Hivi faida itokanayo na uwekezaji katika hisa inavutia? coz naogopa kuweka huku vimayai vyangu ambavyo pengine ningeuza voucher vingeleta faida kubwa kuliko kupeleka huko so please wataalamu na wenye uzoefu tunawaheshimu sana na tunajivunia kuwa nanyi kwenye hilijukwaa tupeni darasa.

Pili, hivi tunaweza tukafanya comparison kati ya kuwekeza kwenye saccos na kununua hisa kama za NMB,hapa panatofauti gani wakuu?
 
Kwanza kuna makampuni yamespecialize kama brokers wa stock exchange market mfano orbit wapo twiga house. Wao ni maconsultant na wanatoa maelezo mazuri kuhusu hisa.

Kununua hisa maana yake unaweka mtaji wako katika kampuni nawewe unakuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni. Sasa unapotaka kununua hisa ni muhimu ukanunua hisa za kampuni ambayo inafanya vizuri. Kampuni ikishapata faida mwisho wa mwaka inabakisha sehemu ya faida kwa ajili ya kujiendeleza na sehemu nyingine inatoa gawiwo/dividend kwa owners/wanahisa.
Na kampuni inavyozidi kufanya vema ndivyo thamani ya hisa zake zinazidi kuongezeka.

Saccos ni kama unaweka hela yako na ikifika amount fulani unakuwa na fursa za kukopa na mtaji wako ulioweka unabaki palepale na kama ukijitoa unaondoka na pesa uliyo weka.

Swali jingine.
 
Maelezo yako ni sawa kabisa!
Kwa kusaidia zaidi weka makampuni ambayo tayari yameshafloat hisa zake, na bei approximate ya hizo hisa!
Nilisoma hapa juzi kuwa Precision wanataka pia ku-flaot hisa, je hii ni kweli?
 
maelezo yako ni sawa kabisa!
Kinachonitatiza ni kwamba sijaelewa unatakaje sasa baada ya hayo maelezo?...sioni cha kudiscuss zaidi!

mimi nimejaribu kumjibu mtuma thread. Hebu soma vema maswali yake hapo juu. Thread yake inahitaji majibu
 
Kwanza kuna makampuni yamespecialize kama brokers wa stock exchange market mfano orbit wapo twiga house. Wao ni maconsultant na wanatoa maelezo mazuri kuhusu hisa.

Kununua hisa maana yake unaweka mtaji wako katika kampuni nawewe unakuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni. Sasa unapotaka kununua hisa ni muhimu ukanunua hisa za kampuni ambayo inafanya vizuri. Kampuni ikishapata faida mwisho wa mwaka inabakisha sehemu ya faida kwa ajili ya kujiendeleza na sehemu nyingine inatoa gawiwo/dividend kwa owners/wanahisa.
Na kampuni inavyozidi kufanya vema ndivyo thamani ya hisa zake zinazidi kuongezeka.

Saccos ni kama unaweka hela yako na ikifika amount fulani unakuwa na fursa za kukopa na mtaji wako ulioweka unabaki palepale na kama ukijitoa unaondoka na pesa uliyo weka.

Swali jingine.

Kabla ya swali jingine labda tu niseme kuwa maelezo yako yamekaa vizuri sema kuhusu ile issue yafaida itokanayo na uwekezaji wa hizo hisa ndo hujagusia kabisa kama zina mvuto ama vp?itakuwa poa kama utatujuza na hilo Mkuu
 
Swali lako ali-make sense kwa sababu inategemea unanunua hisa na kampuni gani?

1...Kama ni kampuni changa uenda usipate dividend for a long time mpaka kampuni itakapoanza pata faida na hata wakianza kutoa dividend pato lako litatokana na thamani ya hisa ulizonazo in percentage na mgao wako utakuwa in percentage of what is being offered. And if the company ever goes bankruptcy you'll be the last person to be paid. Investors wa makampuni machanga mara nyingi huwa ni watu wanaoelewa potential ya hilo soko wanalowekeza or rich gamblers like Warren Buffet.

2...Ukinunua hisa katika already established company by law haya makampuni yanatakiwa kutoa financial reports hili kuwapa picha potential and already committed investors how the company is performing. Read the financial report of the company you need to invest in and find out what sort of dividend they have been paying and how often.

Mwisho remember kama jamaa alivyokuonya hapo juu companies are not obliged to pay dividends if they feel their not in a good financial position. There are also other little technicalities as an investor you'd need to know but then hii si shule ya bure ebu nenda kidogo hata uka-google after all its your money your going to risk.
 
Nikiamua kucheza nazo hisa kibiashara zaidi, yaani nanunua kwa bei poa leo na kesho nauza kwenda kununua kampuni nyingine inawezekana au ni mpaka muda fulani upite ndipo naruhusiwa?
 
Kama ujui sheria za kununua na kuhuza hisa, kwanza nashauri ungejifunza kanuni zinazofanya hisa kupanda na kushuka. Hila hapa kinachoshangaza wewe ujue kuna uwezekano wa kununua na kuuza kibiashara halafu unashindwa kujua kama kuna time limit, aint that pathetic.
 
Nikiamua kucheza nazo hisa kibiashara zaidi, yaani nanunua kwa bei poa leo na kesho nauza kwenda kununua kampuni nyingine inawezekana au ni mpaka muda fulani upite ndipo naruhusiwa?

Mkuu wewe unachoongelea ni stock trading; tena karne hii ya internet unaweza ukafanya trading sio kwa siku hata kwa dakika au sekunde na kwenye masoko makubwa yaani Marekani; UK n.k. Pia unaweza ukawa unafanya Currency Trading as well... unachofanya unakuwa na Account unaweka pesa alafu unaanza kazi....

Word of Caution hii inaweza ikawa njia ya kujipatia pressure au ugonjwa wa moyo (kama hujui unalolifanya...) just imagine umeweka pesa zako kwa kununua stock fulani au currency fulani asubuhi by saa nne hiyo stock imeshuka units chache (this can translate in a lot of money..) by saa sita unawea kujikuta umekuwa wiped out... (ingawa huwa kuna vitu vinaitwa stock stop au stock limit..., kwamba labda stock ikishuka units mbili basi ile trading iishe na ujitoe ili usipate hasara zaidi ila sasa huenda ikashuka unit tatu alafu ikapanda unit mia moja (sasa unaona hii emotion rollercoster unaweza ukajikuta ume-sweat jasho mpaka damu au umekonda kwa siku moja..., kumbuka hivi vitu vinamove within seconds unaweza ukamake au kuloose any amount of money within seconds
 
Mkuu kwa ujumla kwenye hisa si mahali pa kupategemea kutengeneza faida ya kukufanya uishi kwayo au kukuinua kiuchumi haraka na kufanya mambo yako ya mendeleoa labda kama umewekeza mamilioni. Nikupe tu mfano, mimi nilinunua hisa za Twiga wakati huo ( kama sikosei ilikuwa 2006) zikiuzwa kwa Tshs 435 na sasa zimefikia Tshs 2,080 kwa hisa. Kwahiyo kama ningekuwa nimenunua assume hisa za milioni kumi (hisa 22,988) na nikaziuza leo hii ningepata jumla ya Tshs. mil 47.8. Faida ni 37.8 mil. Tatizo lililopo kwenye kampuni nzuri ni demand kuwa kubwa kuliko supply (yaani hisa floated in the market ni chache kulingana na wahitaji). Nilitaka kununua hisa za kama mil 5 hivi nikajikuta napata za around mil 1.26 tu pesa zingine zikarudishwa. Kwahiyo mwaka wa kwanza nilipata gawio la around TSh. 87,000 mwaka wa pili around 100K. Mwaka jana kidogo imeongezeka sana na kufikia above 400K. Kwa mantiki hiyo gawio si pesa nyingi za kukuza mtaji wako kama umewekeza pesa kidogo. Kwa kifupi ni kwamba unaweka pesa yako huko kama unaweka kwenye fixed akaunti ya benki na kama ni kampuni nzuri basi huko utapata faida zaidi kuliko benki.
Asante.
 
Kabla ya swali jingine labda tu niseme kuwa maelezo yako yamekaa vizuri sema kuhusu ile issue yafaida itokanayo na uwekezaji wa hizo hisa ndo hujagusia kabisa kama zina mvuto ama vp?itakuwa poa kama utatujuza na hilo Mkuu

Mkuu faida siyo constant kwa kila mwaka kwa sababu gawiwo huwa linaamuliwa na board of directors wa kampuni husika. Kampuni inaweza kutengeneza faida kubwa sana mwaka fulani mkashangaa mnapata gawio kidogo kutoka na maamuzi ya board of direcotors. Maana wanaweza kuamua kuwa faida iliyopatikana kiasi kikubwa kiongezwe kwenye mtaji wa upanuzi wa kampuni na sehemu kidogo ndo mkagawiwa. Kwa mfano mwaka 2008/2009 Twiga Cement walitengeneza faida kubwa sana kutokana na mauzo huko Afrika ya kusini kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya mpira wakati wa maandalizi ya World cup lakini tualiambulia gawiiwo kidogo sana ukilinganisha na mwaka jana. Na faida pia inategemea na kampuni yenyewe. Kwa mfano kama mtu alinunua hisa za Nicol au TOL basi leo hii anasikilizia maumivu tu.
 
kama unataka kupata faida kupitia hisa, na hata uwekezaji mwingine, principle ni moja tu i.e diversification. Unatakiwa kutengeneza kitu kinaitwa portfolio. Alaf unanunua hisa za kampuni kutokana na objectives umejiwekea. Kuna aina tatu za wawekazaji kutokana na risk tolerance

1. Aggressive investment strategy- huyu ni risk taker ambaye anatafuta faida kubwa, ana upto date information za kampuni alizoweka, pia anauelewa mkubwa soko linavyojiendesha mfano Warren Buffet na wengine.

2.Moderate investment strategy. Huyu ni muwekezaji mwenye nia ya kuweka mtaji wake katika portfolio yenye mchanganyiko wa risky asset na fixed income asset kama T-Bills etc. Huyu uwekezaji wake ni kulinda mtaji kutokana na kushuka thamani ya fedha na inflation.

3. Conservative investment strategy.
Huyu hataki risk kabisa katika mtaji wake. mara nyingi hupendelea kuweka mtaji katika fixed income assets, kama fixed deposit, T-bills, debentures na zingine. Faida yake ni ndogo ukilinganisha na wote niliowataja hapo juu.

Huo ni mwanzo tu wa mambo unayotakiwa kujua kuhusu soko la fedha, mengine inabidi kuwaona consultants wenye ujuzi zaidi na soko letu.
 
Yap! hapa sasa ninapata Idea

Mkuu faida siyo constant kwa kila mwaka kwa sababu gawiwo huwa linaamuliwa na board of directors wa kampuni husika. Kampuni inaweza kutengeneza faida kubwa sana mwaka fulani mkashangaa mnapata gawio kidogo kutoka na maamuzi ya board of direcotors. Maana wanaweza kuamua kuwa faida iliyopatikana kiasi kikubwa kiongezwe kwenye mtaji wa upanuzi wa kampuni na sehemu kidogo ndo mkagawiwa. Kwa mfano mwaka 2008/2009 Twiga Cement walitengeneza faida kubwa sana kutokana na mauzo huko Afrika ya kusini kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya mpira wakati wa maandalizi ya World cup lakini tualiambulia gawiiwo kidogo sana ukilinganisha na mwaka jana. Na faida pia inategemea na kampuni yenyewe. Kwa mfano kama mtu alinunua hisa za Nicol au TOL basi leo hii anasikilizia maumivu tu.
 
Kwanza kuna makampuni yamespecialize kama brokers wa stock exchange market mfano orbit wapo twiga house. Wao ni maconsultant na wanatoa maelezo mazuri kuhusu hisa.

Kununua hisa maana yake unaweka mtaji wako katika kampuni nawewe unakuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni. Sasa unapotaka kununua hisa ni muhimu ukanunua hisa za kampuni ambayo inafanya vizuri. Kampuni ikishapata faida mwisho wa mwaka inabakisha sehemu ya faida kwa ajili ya kujiendeleza na sehemu nyingine inatoa gawiwo/dividend kwa owners/wanahisa.
Na kampuni inavyozidi kufanya vema ndivyo thamani ya hisa zake zinazidi kuongezeka.

Saccos ni kama unaweka hela yako na ikifika amount fulani unakuwa na fursa za kukopa na mtaji wako ulioweka unabaki palepale na kama ukijitoa unaondoka na pesa uliyo weka.

Swali jingine.

Labda niongezee kidogo, hakuna ulazima wa kampuni kutoa dividends hata kama imepata faida kubwa hayo ni maamuzi ya kampuni yenyewe.

So kuna njia kadhaa za kupata "profit" kutoka hisa moja ni hiyo ya dividends kama kampuni ikiamua kutoa na pili ni kununua hisa kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu so unatakiwa ununue hisa za kampuni ambayo unategemea thamani ya hisa zake itapanda. Hakuna maana ya kununua hisa za kampuni ambayo inafanya vizuri lakini thamani ya hisa zake hazitapanda au zitashuka.

Labda niseme tu kuwa pia unaweza kuprofit kama hisa za kampuni zikishuka hii inaitwa short selling na complicated kidogo na sina uhakika sheria za bongo zinasemaje kuhusu hilo.
 
Nikiamua kucheza nazo hisa kibiashara zaidi, yaani nanunua kwa bei poa leo na kesho nauza kwenda kununua kampuni nyingine inawezekana au ni mpaka muda fulani upite ndipo naruhusiwa?

Hapo utakuwa unafanya gambling na nimesoma sehemu nyingi kuwa statistically always utapoteza in the long run. Sio idea nzuri hii.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom