Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Nimesoma mada ya ndugu na Rafiki yangu Molemo inayodai kuwa maelfu ya wanachama wa CHADEMA wamejitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya kumchukulia na kumpelekea fomu ya kugombea Uenyekiti wa Taifa Mwenyekiti wa sasa Mhe. Freeman A. Mbowe. Fomu husika, kwa uchaguzi wa Disemba, inagharimu shilingi milioni moja za kitanzania.
Mkuu Molemo anajaribu kuonyesha kuwa wanachama wa CHADEMA kwa maelfu bado wanamtaka Mbowe ili 'awavushe'. Mbowe amekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka kumi akichukua uongozi baada ya Hayati Bob Makani. Sikubaliani na hoja kuwa Mbowe analazimishwa na wanachama kugombea Uenyekiti.
Ingawa mimi si mwanasiasa, ufuatiliaji wangu wa siasa katika vyama vyote umenifahamisha kuwa siasa ni mkusanyiko wa maigizo, ulaghai na utapeli ulio na chembechembe ndogo za ukweli. Kwenye siasa, 9 husemwa 6 na sifuri na o zaweza kutotofautishwa kirahisi. Kwenye siasa, ambamo Mbowe yumo, kunaweza kuigizwa jambo hadi watu wakaamini.
Nasema kuwa Mbowe (kama itaonekana amechangiwa na kupelekewa fomu) anataka mwenyewe kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Haya maigizo ya kuchangiwa na kubembelezwa kugombea nayakataa. Walishawahi kuwepo wanasiasa waliotembelewa na kuombwa kugombea katika aina hii hii ya maigizo.
Mbowe amefanya mengi na makubwa. Anapaswa kukaa benchi la washauri wa chama na kuachia wengine wakiongoze chama. Aliyoyafanya wakati wa uongozi wake yatamfanya akumbukwe na kuheshimika kuliko aendelee na kundelea kusemwa kama mlafi wa madaraka kwenye chama chake.