Tusidanganyane: Mbowe bado anataka kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,221
25,691
Nimesoma mada ya ndugu na Rafiki yangu Molemo inayodai kuwa maelfu ya wanachama wa CHADEMA wamejitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya kumchukulia na kumpelekea fomu ya kugombea Uenyekiti wa Taifa Mwenyekiti wa sasa Mhe. Freeman A. Mbowe. Fomu husika, kwa uchaguzi wa Disemba, inagharimu shilingi milioni moja za kitanzania.

Mkuu Molemo anajaribu kuonyesha kuwa wanachama wa CHADEMA kwa maelfu bado wanamtaka Mbowe ili 'awavushe'. Mbowe amekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka kumi akichukua uongozi baada ya Hayati Bob Makani. Sikubaliani na hoja kuwa Mbowe analazimishwa na wanachama kugombea Uenyekiti.

Ingawa mimi si mwanasiasa, ufuatiliaji wangu wa siasa katika vyama vyote umenifahamisha kuwa siasa ni mkusanyiko wa maigizo, ulaghai na utapeli ulio na chembechembe ndogo za ukweli. Kwenye siasa, 9 husemwa 6 na sifuri na o zaweza kutotofautishwa kirahisi. Kwenye siasa, ambamo Mbowe yumo, kunaweza kuigizwa jambo hadi watu wakaamini.

Nasema kuwa Mbowe (kama itaonekana amechangiwa na kupelekewa fomu) anataka mwenyewe kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Haya maigizo ya kuchangiwa na kubembelezwa kugombea nayakataa. Walishawahi kuwepo wanasiasa waliotembelewa na kuombwa kugombea katika aina hii hii ya maigizo.

Mbowe amefanya mengi na makubwa. Anapaswa kukaa benchi la washauri wa chama na kuachia wengine wakiongoze chama. Aliyoyafanya wakati wa uongozi wake yatamfanya akumbukwe na kuheshimika kuliko aendelee na kundelea kusemwa kama mlafi wa madaraka kwenye chama chake.
 
Mbowe ni dictator hawezi kuachia hiyo nafasi kwasababu anajua kuna ruzuku. Eti mnataka tuwape nchi! Kweli! Si watang'ang'ania milele,? Waendelee tu kuwa wapinza maana uroho wao wa madaraka hautaicha nchi salama!
 
Viongozi hawako tayari kupoteza uongozi wao

Jiulize wanag'ang'ania nini kwenye uongozi

Je hatuna mwingne anae weza kuwa kiongozi

Je wanaanda vipi viongozi makini kama wao wanavyo jijua kuwa wako makini

Tujiulize Kwanin watu tunamwona kiongozi tulie nae ni bora


Kuna wakati viongozi makini huandaa viongozi makini

Ila tunapo pata kiongozi mbovu husimama na kuonekana bila yeye hakuna kitu

Mbowe alipaswa kuachia kiti akiwa bado na nguvu awacoach vijana kama mzee wa chama
 
Halafu mkuu kama issue ni ku over stay kwemye uongozi wa siasa. Kuna majina tunasikia toka tukiwa watoto wa shule za msingi enzi hizo tukilazimishwa kukipenda chama, mpaka leo hao watu wapo na ni viongozi.

Wachache wao ni Mangula na Wasira. Jeeee huko hakuna watu wengine wa kushika hivyo vyeo vyao
Kuna mtu anaitwa Mrema, mbona humuongelei

Kuna Lipumba, mbona humuongelei

Tunataka maendeleo na uhuru wa kuelezea mawazo yetu hata kama ni ya hovyo. Tusikilizeni na mtujibu
 
Back
Top Bottom