GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,542
- 108,846
Kwa takribani karibia siku 40 zinatimia sasa za Mfungo wa Kwaresma ambapo tunakaribia pia kusheherekea Sikuu ya Pasaka hapo Keshokutwa ila kwa Wakristo wenzangu wengi niliokuwa nao na matendo ambayo wamefanya nitakayoyaorodhesha hapa ukweli ni kwamba waliofunga hasa Kwaresma hawazidi Watatu na tuliobaki wote tumetenda dhambi nyingi sana.
Nawasilisha.
- Nimepishana sana na Wake za Watu Gesti Kwaresma hii
- Nimeshuhudia Wakristo wengi sana wakiwateta wenzao Kwaresma hii
- Nimekutana na Vijana kadhaa wa Kikristo wakipanga njama ya kuiba Ofisini Kwao Kwaresma hii
- Nimeshuhudia Wanaume wengi sana wa Kikristo wakitembea na Watoto wa Shule
- Nimeshuhudia Wakristo wengi sana wakidhulumu wenzao
- Nimeshuhudia Wakristo wengi mno wakidanganya tena bila woga wala aibu
- Nimeshuhudia Wakristo wengi sana wakitega kwenda Makanisani japo Ijumaa Kuu hadi Jumapili na Jumatatu ya Pasaka watafurika / watajazana sana
Nawasilisha.