Uchaguzi 2020 Tusidanganyane: Kwa mtindo huu sioni hata Mkurugenzi mmoja atayeweza kutangaza ushindi kwa upinzani abadani

Louis II

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,030
4,645
Kuna mambo hayahitaji akili kubwa sana kuyaelewa namna yanavyoenda/endeshwa.

Hii kauli mmeisahau? "Nikuteuwe mimi kuwa Mkurugenzi, nikupe gari, nikupe nyumba, nikupe mshahara na posho halafu umtangaze mpinzani mshindi!!". Maneno hayo ni mazito sana na yanatanabaisha namna mambo yanavyoanza kuwaendea kombo wapinzani hata kabla ya kuanzwa kwa kampeni.

NEC sio wenzetu, Polisi vivyo hivyo! Mahakama nazo zimekosa weledi wa namna ya kuzisimamia sheria. Upinzani usitegemee muujiza kwani hakuna Mkurugenzi ambaye atakubali kupoteza 'ugali' wake kwa kumtangaza mpinzani kuwa mshindi.

Kwa hali ilivyo sasa, "Wananchi tutachagua, NEC watateuwa".
 
Resistance ya Hali ya juu inatakiwa kuanzia sasa kabla hata ya kampeni kuanza
Mkuu hiyo resistance imeshashindwa kabla ya kuanza. Wabunge zaidi ya 50 wa CDM wameenguliwa kwa sababu ambazo ni za kijinga sana, na raia wako kimyaaa kama vile hakuna kilichotokea. Tunaaza kampeni wabunge wote hao wameenguliwa, maana yake tumekubali matokeo. Na kwenye uchaguzi watafanya hivyo hivyo na maisha yataendelea. Watz bado sana, maji bado hayajafika shingoni. Siku yakifika ambayo haijulikani ni lini...!!!
 
Ndugu ndugu wapinzani,
Mumeona jinsi munavyo enguliwa na hao NEC bila sababu za msingi.
Mumeona jinsi haki yenu ya uchauguzi isivyopatikana kwa watu wetu kuengulia kwa sababu ya msingi (Breaches of Fundamental rights)
Mumeona jinsi mapingamizi yenu yanatupwa bila sababu za msisngi.
Hivi kweli mnavyoona mtapa haki sawa huko mbeleni? Thubutu

Kwa nini msiwafunguliwe kesi ya ubaguzi hao NEC na muiombe mahakama iistopishe NEC kuendesha au kusimamia zoezi zima la uchaguzi huu?

Kuendelea nayo hii NEC ya sasa maana yake ni kwamba :
1. Mumekubaliana na figisu zote za NEC za sasa
2. Mumekubali kwamba wakisha tangaza matokeo (Uraisi) hamtaweza kuyapinga au kuyahoji mahala popote Tanzania maana ni kinyume na sheria
3. Mumekubali kwamba uchaguzi utakuwa free na fair ingawaje yale yale yaliyotokea serikali za mitaa yanajirudia.
4. Mkiishitaki NEC kwa certificate of urgent (breaches of fundamental rights ) kwa kuwapendelea CCM au kwa kutofuata sheria za uchaguzi na kanuni zake kinachoweza kufanyika ni kati ya haya yafuatayo:

1. Mahakama kuwarudisha wagombea wote walionguliwa kwa sababu za magumashi
2. Mahakakam kuisimamisha NEC kuendela na zoezi zima la uchaguzi mpaka hapa watakopo kuwa wameonyesha kwamba wao sio biased
3. Mahakama kuagiza tume huru itayounda na watu huru.

Hii ndio njia pekee iliyobakia kwa sasa hadi 28 October.
Tarehe nyingine ya uchaguzi inaweza kupangwa (kama itakavuo amuliwa na mahakama) ili kurekebisha dosari zote za uchaguzi kurekebishwa.
Hamuwezi kuendelea na ushaguzi huu ili hali ubaguzi wa haki zenu za msingio ziko wazi referee wenu- NEC- hana uwe3zo tena wa kusimamia zoezi zima la uchaguzi utao kuwa free an fair maana tayari amekwisha onesha uwezo wake - hana uwezo huo kwa kuusimamia

Ni ushauri tu na maoni yangu binafsi si lazima mmchukue... msipotaka hivyo, hakuna njia ya kuyahoji matokeo wala ukiukwaj wa taratibu maana mtakuwa mmekubaliana na yote NEC iliyowafanyia.
 
Kuna mambo hayahitaji akili kubwa sana kuyaelewa namna yanavyoenda/endeshwa.

Hii kauli mmeisahau? "Nikuteuwe mimi kuwa Mkurugenzi, nikupe gari, nikupe nyumba, nikupe mshahara na posho halafu umtangaze mpinzani mshindi!!". Maneno hayo ni mazito sana na yanatanabaisha namna mambo yanavyoanza kuwaendea kombo wapinzani hata kabla ya kuanzwa kwa kampeni.

NEC sio wenzetu, Polisi vivyo hivyo! Mahakama nazo zimekosa weledi wa namna ya kuzisimamia sheria. Upinzani usitegemee muujiza kwani hakuna Mkurugenzi ambaye atakubali kupoteza 'ugali' wake kwa kumtangaza mpinzani kuwa mshindi.

Kwa hali ilivyo sasa, "Wananchi tutachagua, NEC watateuwa".
Labda kinukishwe mahali akili iwarudie
 
Nchi inaweza kuingia kwenye machafuko na wote pamoja na buku saba, wateuliwa, wachumia tumbo na wenye mamlaka tukajuta na kuona jinsi ujinga, ulimbukeni , ushamba na unafiki ulivyo na madhara.
 
Back
Top Bottom