Tusidanganyane hata Lowassa au Sumaye wenu wakiteuliwa hawawezi kataa!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Leo hii Rais Magufuli akimteiua Lowassa au Sumaye kushika wadhifa wowote ule, hawawezi kukataa na hawana jeuri ya kukataa, na wala hili halihusiani na kuwa na fedha au kutokuwa na fedha, wengi wao wanaopiga kelele ni kwamba hawajapata Bahati ya kuteuliwa!

Tumeona Tundu Lissu baada ya kuteuliwa na law firms kuwa Kiongozi wa TLS, amepoa na hajawatibua Askari wetu kwa makusudi na kujipeleka Dodoma huku akijua atashikwa na kusafirishwa, hivyo tuache kudanganyana hapa, kila mtu anaangalia maslahi yake na tunaongelea mambo ya Chama pale ambapo hatujapata nafasi ya kupewa nyadhifa, hata Mbatia Ubunge wake aliupata tu kwa sababu ya Kiongozi wa CCM kumteua, kwa nini hamkumuita Msaliti? Sasa mnazijua sababu za Mwenyekiti wa CCM kumpa Ubunge Mbatia? Acheni kudanganyana, ...

Tundu Lisu kabla ya Ulaji!
maxresdefault.jpg


Tundu Lissu baada ya kupewa ulaji!

A-4-18.jpg


603b58264a60fb295385fec65738e30a.jpg
 
Unataka kusemaje?

Na Mecky Sadick akiteuliwa kesho atakwenda mbio kuapa, hana jeuri ya kukataa!
 
Ndugu una jitahidi kusafisha uchafu sio?
usipoteze muda uchafu ni uchafu tu ata usafishe unabaki kuwa uchafu tu!!
 
Hili siyo swala la fedha ndugu, ni swala la kufungua Milango zaidi au kuifunga, ni swala la kibinafsi zaidi, na Lowasa anajali maisha yake na familia yake zaidi anavyojali maisha yako na chadema!
HUNA HOJA, KJIPANGE TENA.
 
Mtoa mada hunakumbukumbu nzuri
Naomba nikukumbushe kuwa si kila anayeteuliwa anakubali

Unakumbuka mke wa lowasa alivyoteuliwa na chadema kuwa mwakilishi bungeni majibu yake yalikuwaje?

Sio kila mtu unadhani ni mwepesi hivyo.

Unakumbuka kuna mkurugenzi aliteuliwa akakataa na akaona kazi ktk kampuni ya tigo inathamani kuliko uo nafasi aliyopewa na magu?

Panua mawazo yako mkuu
 
Mtoa mada hunakumbukumbu nzuri
Naomba nikukumbushe kuwa si kila anayeteuliwa anakubali

Unakumbuka mke wa lowasa alivyoteuliwa na chadema kuwa mwakilishi bungeni majibu yake yalikuwaje?

Sio kila mtu unadhani ni mwepesi hivyo.

Unakumbuka kuna mkurugenzi aliteuliwa akakataa na akaona kazi ktk kampuni ya tigo inathamani kuliko uo nafasi aliyopewa na magu?

Panua mawazo yako mkuu


Aliteuliwa na chadema, sasa chadema wana Dola? Chadema wana nguvu gani nchi hii? Kumbuka siyo swala la fedha, ni zaidi ya hapo, ingekuwa hivyo akina Shabiby, Abood, &Co. wasingekimbilia kuwa Wabunge wa CCM, CCM ni Chama Dola kuna sababu kwa nini kinaitwa hivyo, sasa uteuzi wa chadema utakufikisha wapi nchi hii?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom