Tusidanganyane Hakuna Kiongozi asiyelipa Fadhila Dunia Hii!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Nawashangaa baadhi ya watu kumrushia Raisi Magufuli madongo kwenye baadhi ya teuzi zake kama vile Nape, Makamba na sasa Mama Migiro na wengineo kwamba ni wale wale lkn wanachosahau ni kwamba hawa wote wametoa mchango mkubwa sana kufanikisha ushindi wa Magufuli mtu kama Nape unawezaje kumtenganisha na Uraisi wa Magufuli?
Hivyo ni jambo la kawaida sana hapa Duniani kwamba huwezi kuwasahau hata iweje, cha muhimu hapa ni kwamba wanaolipwa fadhila wasigeuke kuwa mzigo kwa Raisi yaani kuharibu kazi lkn kama wanachapa mzigo kama vile Nape anavyochapa sasa hivi hakuna tatizo hapo!

Hata kama ukipindua nchi kijeshi ni lazima kuna watu ambao wamekuwa na wewe tangu siku ya kwanza na kamwe huwezi kuwatupa hata Raisi Obama tutaona wale wote waliomsaidia kushinda uchaguzi hakuwatupa kama akina Rahm Manuel ambao ndiyo waliomwingiza Obama Ikulu na alivyoshinda Manuel akateuliwa kuwa white house chief of staff na wengine wengi achilia mbali mabankers waliomchangia fedha hivyo ni jambo la kawaida sana kwani msisahau pia Raisi Magufuli pmj na uzuri wake wote kama Raisi wetu bado pia ni Mwanasiasa au niseme ni lazima wakati fulani pia afanye maamuzi ya kisiasa!

Hivyo msishtuke hii ni kawaida sana, na inafanyika Dunia nzima!
 
YES. Mkuu umeongea kama msomi, nimependa. Hata kwenye Global Financial Crisis 2008 kuna makampuni yali receive bail out money in the US na mengine yakawachwa yajifie kwa sababu kama hizi.

Hizi issue zipo sanaa tu.
 
mbn hata CDM walimchagua yule reporter wa itv devota minja kuwa mbunge wa viti maalum et kisa tu alikua anaripoti vzur habar zao wakati wa kampen za uchaguzi, siku zote unampendelea anayekusaidia, mm sion tatzo kwa maguful kuwateua watu waliomsaidia katka safari yake. haya mapnzani asiyasikilize, kelele zao ni kama za mbwa mlinzi
 
Buhohela naye jpm kamkumbuka
 
Shida Ni kwamba jamaa anasema Hakuna aliemsaidia kuingia madaraka.. Na Kama Ni fadhila angeanza na wale 46 wa Baba Mwanaasha.
 
mbn hata CDM walimchagua yule reporter wa itv devota minja kuwa mbunge wa viti maalum et kisa tu alikua anaripoti vzur habar zao wakati wa kampen za uchaguzi, siku zote unampendelea anayekusaidia, mm sion tatzo kwa maguful kuwateua watu waliomsaidia katka safari yake. haya mapnzani asiyasikilize, kelele zao ni kama za mbwa mlinzi
Kwa huyo bint kuna zaidi ya hayo Mkuu.
 
Kweli mkuu buhohela simuoni baada ya uchaguzi haunekani yuko wapi Mzee wa kipindi cha dakika 45?
Kwa habari zilizopo na zenye aslimia kubwa ya ukweli ni kwamba wakati wa kampeni mwajiri wake alimwita arudi ofcn na badala yake saro akachukue nafas yake, ndipo jpm aligoma akasema haondoki m2 hapa, so ikwa ndo mwisho w jamaa itv japo huenda mara chache kwa masuala binafsi. Anasubiri kupangiwa kazi
 
Back
Top Bottom