Tusidanganyane, hakuna dawa ya kudumu ya jino bovu! Usiku wa leo nusura nilale uvunguni

Kuna watu watabisha hiyo nina caninr ya kulia imeharibika kufika kwa mtaalam akaniambia ili tunali scrap yaan wakalikwangua mpe ndani likajazwa sasa ni mwaka wa nne ila wameliua si hisi kitu hala limefanya colour blackish hiv natafuna kama sina akilo nzuri .
Na nina mengine mawili ya kusagia nayo vile vile haya nikayapeleka kwa wale cheaper dentist wameniziba hata miezi sita haija fika juzi nimetoka kutoa ujinga wao nimewekwa tena upya .
Akikuambia mtu anaziba jino kwa 50k kimbia .
Toa mpunga kwa hospital eleweka utaenjoy na meno yako nusu au robo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo njia ipo na ni nzuri kwa jina ambalo halijatoboka. Lililotoboka shida yake linahifadhi uchafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah umenikumbusha mbali

Kuna jamaa yangu mmoja nilikuaga nampitia kwao daily asubuhi tunaenda skuli

Sasa siku moja nimempitia nikamkuta yupo chini ya mti, analia kabisa na machozi yanamtoka

Mimi kwa haraka haraka nikajua amefiwa na mshua wake mana kipindi hicho mshua wake alikuwa anaumwa

Nikamuuliza vipi bwashee akaniambia jino linauma toka usiku yupo hapo chini ya mti hakulala

Nilikuja kuyaelewa maumivu yake pale alipoumwaga bimkubwa, aisee japo sijawahi kusumbuliwa na jino lakini namna bimkubwa alivyokuwa anahangaika sebleni ilinipa picha halisi ya maumivu anayopitia.

Suluhisho la kudumu ni kuling'oa tu japo wakikosea kung'oa inaweza kusababisha matatizo mengine ikiwemo kifo
 
JINO LINAUMA!
Liliuma lakwanza nkatoa.likahamia kwingine nkatoa...
Baada ya miezi sita likaanza kuvimba lajuu!!!!
Nkawa naambiw kutoa la juu Ni noma ,afu limetoboka na linatoa harufu

Siku nahamishiwa wilayani nkapiga hesabu ,,,,hivi haya meno huko si yataniuwa!!
Nkainuka nkaenda mackdonia nkatoa yote mawiliii
Hadi leo fresh ila mapengo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami mwaka jana nilipata shida ya jino...nilijikuta napata maumivu makali ya jino la mwisho na nilihisi jino litakuwa limetoboka, baada ya kwenda hospitali, Dr aligundua kumbe kuna jino lilikuwa linaota mwisho kabisa likielekea horizontally ikiwa inamsukuma yule wa pembeni yake...ikabidi kwenda kwaajili ya x-ray then ktk kuling'oa sijawahi kupata maumivu makali maishani kama yale coz ilibidi nichomwe ganzi kama 3 hivi na utaratibu uliofanyika ni wa kuliondoa lile jino lililokuwa la pembeni ambalo ni zima, dah! MaDr walikuwa wawili lakini zile nguvu walizozitumia kuling'oa hilo jina zilikuwa kubwa kinoma na still maumivu yalikuwa makali sana japo ganzi nilipigwa, sijui ingekuwaje bila ya ganzi...maumivu yalitumia muda wa kama wiki 1 na nusu hivi.

Ulikua unasikia maumivu huku umepigwa ganzi? Si nasikia dawa ya ganzi ni kuzuia maumivu?

Ulilia? Ulikua unakulaje chakula?
Ulikua unatembea na pamba muda wote? Kutematema mate je?

Mie Nina gego linanisumbua sana, naogopa kwenda hospital kung'oa
 
Kwanza polee....
Hii utaipata supermarkets au kwenye maduka makubwa ya dawa, zipo za aina mbali mbali kulingana na flavour, mfano hio uliyoona hapo juu iliisha asaivi natumia hii..View attachment 1448589
Sijawahi simbuliwa na jino tena, na sitokuja kuacha hii dawa kamwe, siku nikiikosa kwa bahati mbaya basi nitatumia Colgate OG.
Ina sukari sukari?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia mafuta ya Tini,weka kwenye pamba,then bandika kwenye jino linalouma,haitapita nusu saa,maumivu yote yanakata...
 
Mkuu ni kweli.Hiyo ni root canal ndio bei zake.Wanalichimba jino katikati kutoa mizizi,hiyo ndiyo inasababisha bacteria kuozesha jino na maumivu(mishipa ya fahamu).Hivyo huondoa hiyo na kisha kuliçhonga vizuuri kama seremala halafu wanatia dawa na ile material yao gani sijui kuziba pale kwenye shimo.Siku hizi wanaweka kitu kama chuma halafu wanasakafia jino lote na material fulani nyeupe ukipewa kioo ukaambiwa uonyeshe jino lililokuwa limeoza na kutoboka unaanza kulitafuta hulioni!yote meupee pee!😊

Wewe ushawahi kufanyiwa root canal?
inachukua muda gan, masaa manne?
Maumivu yake je... Ukimaliza hapo unaweza kula baada ya muda gan
 
Mkuu naskiaga hizo bei ndo unakaa mwaka linaanza kuuma tena.jino kuziba wanasema ni gharama kidogo sio kwa alfu 20 au 30,na nimefatilia walioziba meno wengi ambao wakiziba yanarudia ni hao wa alfu 30 30

Asalam aleykum ustaadh...
Ulifanikiwa kufanya root canal?
Gharama, wapi, muda uliotumia? Changamoto zipi ulipata wakati na baada ya operation
 
Daah aise ngoja nifanye tafiti kwa zenji wapi wanaziba vizuri jino.

Mana wengine ukienda wanakuziba leo mwakani limetoka

Kumbe wewe ni mzanzibari?
Ndio maana unachangiaga sana mada za uislamu... Niambie basi ulifanikiwa kufanya root canal? Kuziba jino? Shingapi? Changamoto?
 
Jino mzee baba lisikie tu kwa mwingine halafu sijui kwa nini linapenda kuuma usiku ila nimegundua vinywaji kama energy na soda vinasababibisha meno kuharibika au kwa Yale mabovu kuuma
 
Ulikua unasikia maumivu huku umepigwa ganzi? Si nasikia dawa ya ganzi ni kuzuia maumivu?

Ulilia? Ulikua unakulaje chakula?
Ulikua unatembea na pamba muda wote? Kutematema mate je?

Mie Nina gego linanisumbua sana, naogopa kwenda hospital kung'oa
Nilichomwa sindano zaidi ya moja kwaajili ya ganzi, lakini kwakuwa mpango mzima ni kuliondoa jino zima, ganzi haikusaidia kabisa japo nilikuwa kama nimeparalyse upande mmoja wa uso kwaajili ya ganzi na kwa yale maumivu nilitamani hata kuwasukuma wale madr waniache niende zangu tu...na siku nzima nilikuwa siwezi ongea kabisa na muda wote nilikuwa nikitema damu. Ilinichukua kama wiki 1 na nusu kwa maumivu kupungua.
 
Mara nyingi nanunua Sensodyne kwenye maduka ya CH Amon.pale Hakuna bidhaa feki hata moja. na uzuri bei Za Sensodyne Zinafanana pote. Maduka ya CH Amon kariakoo au mlimani city, phamarcy kubwa Kama za JD phamarcy mlimani city na pharmacy nyingine kubwa kubwa huwezi kukuta Feki

Hiyo JD Pharmacy naingia mule Mliman city ndan kabisa Shoprite?
 
Back
Top Bottom