Tusidanganyane, hakuna dawa ya kudumu ya jino bovu! Usiku wa leo nusura nilale uvunguni

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
6,661
20,995
Niliziba jino miaka mitatu iliyopita, kama week tatu hivi zilizopita likaanza tena kumeguka zile sehemu zilizokua zimezibwa, baada ya siku kama tatu likaanza kuuma, nikaanza kutumia dawa za asili ambapo nyingi nilisoma humu.

Nimetumia: Mdarasini, mu alovera, karafuu, majani ya mpera, mu arobaini, tangawizi, dawa zile za wamasai, na nyingne nyingi sana.

Kuna member kama wawili humu walishauri nisukutue mkojo wangu asubuhi, basi nikaamka asubuhi nikaenda uani, kufika nikawazaaa! Mwishowe nikaona huu ni uzwa zwa nikaupiga chini, juzi nikawa na safari, nilikoenda kuna baridii kwa kipind hiki,

Sasa kumbe bwana jino na baridi ndio havipandii kabisa, nilifika jioni, kufika maongezi na wenyeji yakawa mengi, sasa kumbe vile ninavyoongea ndio nazidi kujaza ubaridi kwenye ile sehemu iliyotoboka, muda huo jino lime mute tu, yaan ni kama vile lilisema 'wee bwabwanya tu hapo tutakutana usiku ukiwa mwenyewe' nikala fresh na muda wa kulala ukafika kama saa nne hivi.

Kwanza wakati nipo njiani bi mkubwa alinipigia simu akaniambia 'huko uendako kuna baridi kwa sasa, hilo jino laweza kukusumbua kama umegoma kung'oa beba dawa za mamivu'

Basi kufika nikaenda kununua zile dawa, sasa ule muda wa kulala unafika natoa zile dawa ninywe kucheki ni diclofenac, na si paracetamol, nikatemana nazo (hizi ukitumia kwa muda mrefu husababisha vidonda vya tumbo kwa sababu hukwangua gastroduodenal mucosa na kuharibu ile chemical inayobalance acid inayoingia mwilini)

USHAURI WA BURE
Epuka sana kutumia hizi dawa za kutuliza maumivu/NSAIDs kwa muda mrefu hasa, ibuprofen, diclofenac na asprin, ndio ile unatibu vidonda vya tumbo huponi kumbe wewe unatumia dawa za vidonda vilivyosababishwa na H. Pylori na sio NSAIDs matokeo yake cancer.

Tuendeleee, nikazitupa dirishani nikalala,
imefika saa tano mzigo ukaanza, nikakaza, halafu kukawa na simu nyingi zinaingia ila sikupokea, ikafika saa sita mzigo umepamba moto, nikaaza route pale chumbani, kadiri muda unavyoenda kasi ya routes inaongezeka, nikawa nazunguka pembe kwa pembe kama naagua vile.

Nilipokosa nafuu,
Nikatoka nje kibarazani, kufika napo na maumivu yangu kuna ka mbwa kakawa kana nikoromea, nikakabamiza kopo la maua la tumbo, kakaanza kupiga mayowe mtaa mzima pembeni palikua na kapaka kanajibamiza bamiza kwenye miguu yangu maana kalikimbizwa na yule mbwa kakaja kwangu, kuona vile kakaona napo si salama kakatoka ndukiii, upepo ulivyonipiga ndio nikawa kama nimliechokoza zaidi.

Nikarudi ndani, kufika nikashangaa mama yangu mkubwa ananipigia simu ile saa saba, nikapokea hapo jino linauma sijawah ona, nikajikaza nikaongea kwa uchangamfu ili asijue kama nina shida, sasa kumbe na yeye ananitega kwa kuniongelesha ili nisande niseme ukweli maana nae lilimtesa sana, nikakaza mpaka mwisho mpaka akakata simu,

Kumbe kati ya bi mkubwa au mamkubwa mmoja wapo alipiga simu kwa wenyeji wangu, nikashangaa saa nane nagongewa naletewa chai ya moto iliyojaa tangawizi, wakazuga eti oooh eti tumeona tukuletee chai upashe tumbo moto, nikanywa jino likatulia kabisa kama dk 15-20 baada ya hapo mzigo ukaanza kama ndio limechochewaa, nikawaza nikaokote zile diclofenac?

Nikaona huu ni ujinga, nikawaza niite chai tenaa? Nikaacha maana ni usumbufu kwa watu, sasa hapa ndio zile routes pale chumbani zikaanza tena kama nipo Mandela road, nilikaa kila pozi kuanzia kitandani, mezani, kitini, sakafuni, nayo nikaona najisumbua nikarudi kitandani nikakaza mpaka asubuhi bila kuonja hata tone la usingizi, ni mwendo wa ku guna tu!

Asubuhi na mapemaa nikawaomba wenyeji wangu wanielekeze hospital ilipo, nikaenda kufika huko nako nikakutana na mapicha picha, kufika kwenye benchi nakutana na njemba inanguruma huku imefumba mdomo, mkononi kashika meno mawili kumbe yamong'olewa kimakosa, amepigwa ganzi anasubiria la tatu (alikua anaelekeza yatolewe ambayo hayaumi bila kujua),

Pembeni kuna mshkaji mwingine analalamika ganzi imesanda mara tatu, kucheki kwenye kioo kule ndani naona masululu ya maana mezani na mayoe juu, hapa sasa kajasho kakaanza kunitokaa, maana langu ni gego la juu mwisho na limemeguka kiasi kwamba limefunikwa na ufizi, nikaingia, kufika tu docta kuliona akamuomba mwenzake aje amsaidie, kumbe anaogopa lilivyokaa litamsumbua,

Nikalala kwenye kiti nikamuonesha, anamikwara si ya nchi hii yaani alichukua zana kama tisa hivi au zaidi, mkasi, koleo mbili, vile vioo vya kuangalizia, kijifaa cha kuchokonolea, kajimsumeno, dude fulani hivi sijui ni sululu ile na vifaa vingine halafu akavibwaga vyote kwenye yale makalai yao ya bati kwa nguvu, yaani jino tu lakini kana kwamba unatolewa kichwa halafu ukimcheki usoni anasura chafu hatari hata tabasamu au kumfariji mgonjwa hakuna, nikajiuliza hivi kweli huyu amesomea hii fani?

Akaanza kunipiga ganzi, nikamuuliza mbona anapiga ganzi jino jingne, akasema nimekosea linalouma ni hilo alilopiga, nikamwambia tena lakini akawa anasisitiza hivyo hivyo, anataka kupiga ya pili nikamshika mkono, nikamwambia usinipangie jino la kung'oa au unataka unifanyie kama mlivyomfanyia huyo hapo nje?

Basi Nikagundua hawa hawataweza kabisa lile jino langu maana lilivyo na lilipo ni mtihani, nikaamka nikatoka na ganzi yangu nikarudi, ilitakiwa nikae week ila kufika nikawaambia mi narudi, hapa lengo langu ni kuwahi na kumbuka muda huu jino haliumi sababu ya ganzi, nikaondoka, nikawa nimepanda na ka sista duu, ila nikasema hapa navunga nisije nikaanzisha route humu tena na safari ni almost 9hrs, nikakapa tu hi nikakaa zangu.

Nikawaza, nikikaa kimya sana bacteria wakijaa nitaharibu hali ya hewa, nikiongea jino litauma, usingizi ninao ila kila nikijaribu kulala nashindwa, tukabadilishana mawazo kidogo, baadae alivyoona response ndogo akakaa kimya then baada ya muda akaniuliza kaka umepata matatizo? nikamjibu, 'hapana' ila mwishowe akajua maana utulivu ulikua ziro pale kwenye kiti maana ilifka hatua nataka niingize kichwa kwenye begi.

Liliniuma sana sanaa lakini nikakaza watu wengi wasijenishangaa, nilikua hoi yule dada mpaka akawa kama anaogopa hivi akasema mjulishe mtu wa karibu au nipe namba namba nimpigie, nikamwambia usijali, kufika akanisindkza mpaka hospital, nako kufika wakaniuliza unataka tulizibe tena?

Nikamuuliza unasema nini? siitaki hata kusikia hilo neno tena wewe toa jino lolote unaloona halijakaa sawa huko mdomoni, akatabasamu, Nikamwambia sitaki dr mwingne zaidi ya ...... basi akaja yule Dr. Akanipiga ganzi za kutosha, mdomo unaona kama kapu akacheza nalo mpaka likatoka baada ya kama dk 5 tu hivi, alivyoliangalia akasema 'dogo una roho ngumu sana' baada ya pale sikuhisi maumivu yoyote mpaka sasa,

Wakati tunaondoka yule dada akaniambia 'kuna muda kule kwenye gari ulilala kwenye beg ukatulia sana nikajua umezimia', nikajiongeza kwa kuwaza kimoyo moyo huyu alijua nimevuta maana kila saa nikitulia sana ananishtua 'weee kaka?' mpaka nikamwona kero tena.

Wakati naumwa ilikua nikiona mtu anacheka namuona kama ni malaika halafu nasema hivi huyu anamkumbuka Mungu kwa uzima alionao?

Nikakumbuka ule usemi tunao utamkaga kirahisi na kumbe una uzito mkubwa
'kikubwa uzima'

jino haliponi, ni suala la muda tu,
Leo bisha ila kuna siku utakuja hapa.
 
Pole jino bwana halina adabu ......niliumwa jino ndani ya dakika kumi tu nilikua nimeshaondoka home na sikujua kama natembea uzuri lilipoanza kuuma nilimeza mifupen ...nilienda kugundua sipo home baada ya ile dawa kufanya kazi dakika 20+ ....kesho yake nilienda kung'oa kabisa ....

Nimeshatoa meno mawili naomba mungu asubuhi mchana nisiumwe tena jino maana Yale masindano ya ganzi yalivyo makubwa then unachomwa mdomoni daaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu
asantee nishapoa na gego langu,
Dawa ya jino ni kung'oa tu.
hilo ndio suluhisho la kweli
Mtu akiniambia anaumwa jino halafu analeta blah blah sijui nimeziba,siling'oi huwa namwambia 'HUJAWAHI KUUMWA JINO,SIKU UKIUMWA UTAAMKA ASUBUHI NA KWENDA KULING'OA'
na hua likikuuma vizuri, ukipewa mawazo ya kuzîba unaona ni uchawi
pole sana...lkn asante kwa elimu juu ya dawa za kutuliza maumivu na vidonda vya tumbo.Nasumbuliwa sana na uclers na huwa natumia sana hizo pain killers
hii ishike sana , hapa daŵa za kutumia ni kama omeprazole,
Mbona mnanitisha jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
hapana ,ni vizuri ukawa na checkup ya kinyŵa na meno mapema
 
Pole kwa mkasa huo ndugu. Hofu yangu, ni huyo daktari aliyekuziba mwanzoni kutolichokonoa vizuri kuhakikisha sehemu yote iliyoathirika imeondolewa kabla ya kuliziba. Vinginevyo atawafunika bakteria ambao wataendelea kulichimba ndani kwa ndani.

Binafsi niliziba jino tangu 2005. Mpaka leo halijawahi kuuma kabisa. Lilivyouma mwazoni na mateso niliyoyapata, niliazimia kuling'oa kabisa. Nilivyoenda kwa daktari yeye akashauri lizibwe. Nikakubaliana naye, hivyo mpaka leo napeta.
 
Back
Top Bottom