Tusichoshane 'Hotuba' imeshatolewa jana na leo ni Siku tu ya Kuwashangaa 'Makomandoo' wetu na Rais 'Genius' Afrika Paul Kagame

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,518
108,793
Mmeshaambiwa jana kuwa mpaka sasa kuna Vyuo Vikuu 30 badala ya Chuo Kikuu Kimoja ( 1 ) tu wakati wa Uhuru. Watanzania mnataka nini tena? Hebu acheni Nongwa!

Mmeshaambiwa jana kuwa sasa tuna Balozi 44 na baadae akasema tuna Balozi nchi zote duniani. Watanzania mnataka nini tena? Hebu acheni Nongwa!

Mmeshaambiwa jana kuwa mpaka tuna jumla ya Ndege zetu 12 na nyingine 5 zimeshalipiwa ziko Angani zinakuja kuendelea Kupaki tu pale Terminal 1,2 na 3 zikioza na Twiga wake wakati tulipopata Uhuru tulikuwa na Ndege 1 tu. Watanzania mnataka tena? Hebu acheni Nongwa!

Mmeshaambiwa jana kuwa idadi ya Madaktari imeongezeka nchini hivyo Watanzania hatuugui tena hovyo, Dawa ni za Kumwaga Mahospitalini na hata ukishindwa Kugomboa Maiti yako unapewa tu bure na bila Usumbufu ( Ngendembwe ) ukazike. Wakati wa Uhuru hali haikuwa hivyo. Watanzania mnataka nini tena? Hebu acheni Nongwa!

Kitu pekee tu na cha 'Kitakwimu' ambacho GENTAMYCINE nilikuwa nakisubiri kwa hamu Kukisikia ni wakati wa Uhuru Tanzania kulikuwa na Malaya na Waiba Waume za Watu wangapi, Walevi ( hasa wa Wine ) na Wasagaji wangapi na hii leo wamefikia wangapi?

Tafadhali leo tusichoshane wala tusisumbuane Hotuba ya Sikukuu imetolewa Saa 3 Usiku jana na leo ni Siku 'Maalum' tu ya Kuwakodolea ( Kuwashangaa ) Makomandoo ( na najua Rafiki yangu Komandoo Switibeti ) atakuwepo kama hakuwepo katika lile 'Bogi' la walioenda Ntwara na Nchumbiji kisha Kumshangaa Rais 'Genius' Afrika mwenye Kuongoza kwa Vitendo na siyo maneno mengi na Uwongo mwingi Mheshimiwa Paul Kagame.

Ushauri pekee na wa bure kwa wale mtakaoketi nae jirani ( karibu ) Rais Kagame wa Rwanda jaribuni kumuuliza mbona Yeye anaongoza kwa Vitendo zaidi na Maendeleo yanaonekana haraka halafu hana maneno mengi, hazuruli hovyo Angani na nchini Kwake Rushwa imedhibitiwa, Uzalendo ni wa hali ya Juu na Wananchi ( Raia ) wake wana Akili sana kama Wayahudi na Warusi tofauti na maeneo yenu?

Karibu sana pia Rais Uhuru Kenyatta na naamini kabisa hii Ziara yako ( japo ni ya Siku Mbili tu ) itawanufaisha mno Wauza 'Ulaibu' wa Mirungi ( Khat ) na Bangi ( Marijuana ) hapa Tanzania na Ndege yako itakuwa na nafasi Kubwa na ya Kutosha kubeba Shehena za bidhaa hizo ( hizi ) ili kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani ambapo Wewe, Makamu wako Ruto na ' Political Opportunist' Raila Odinga mmepanga Kuiingiza Kenya yenu katika 'Machafuko' ya Kisiasa hivyo Wananchi wenu ( Wakenya ) watazitumia sana ili 'Wauwane' vizuri.

Happy Independence Day Watanzania!!!
 
Barua
FB_IMG_16379028893410562.jpg
 
Back
Top Bottom