Tusibaguane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusibaguane

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Dec 28, 2010.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  "KATIKA NCHI HII HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUSHINDA UCHAGUZI KWA KURA ZA WAISLAM PEKEE AU WAKRISTO PEKEE" Hii ni kauli maridhawa ya Mh Mbowe. Nawaombeni ndugu zanguni, TUISHI BILA KUBAGUANA KIDINI. Turuhusu tofauti ya mawazo miongoni mwetu. Sisi sote ni ndudu, hata mapacha waliokaa tumboni miezi 9 pamoja wanawaza tofauti. Tupendane, tusaidiane na tuombeane mema. Hasani akimuona Rozi amuone kama dada yake na Masanja akimuona Patel ampende vilevile(Vicious circle). Sisi sote ni ndugu, watoto wa Tanzania. Kupishana mawazo, ndo ubinadamu
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Pishana mawazo na JK uone kama kesho kuna uhai tena Tanzania hii. Walioondoa UDUGU wetu wa Ki-Tanzania hao hapo ...

  Prof Mwaikusa alifikiria mgombea binafsi safi kwetu yuko wapi, Prof Chacha kapigia kilele rasilmali za taifa; siku hizi unamuona, Prof Haroub Othman na tofauti za kimawazo juu ya katika ya jamhuri ya muungano tanzania; yuko wapi.

  Akina kabwela waliotofautiana kitu kidogo basi tena ndio usiseme. Mahubiri haya ni mazuri lakini fikiria tena, nani kalazimisha tufike hapa na huko tuendako safari ni salama kiasi gani bila UDUGU wa Ki-Tanzania na utaifa katika kweli bila kuona wengine ni mabwege tu???????
   
 3. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hakuna udini wa la ubaguzi tz. nafikiri mboe anakosea anaposema tusbaguane
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hata siku moja usikubali kuficha kaa la moto mfukoni mwako!!!!
   
 5. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  maaskofu wamesema anaesema kuna udini afukuzwe tz. sasa ,mboe anapingana na baba askofu?
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Nenda chuo kikuu chochote kilichoko karibu yako wewe kisha ukawaombe kuonana na mwalimu wao wa FALSAFA ili aweze kukurahishishi UJUMBE uliobebwa ndani ya kauli za hao maaskofu.

  Usipende sana kulambala kidonge cha hospitali kionyeshacho utamu wa asali mgongoni, pindi uamuapo kuendelea na lambalamba yako zaidi na zaidi basi huna budi pia kujiandaa na ukanda wenye ladha chungu zaidi ya subili. Tupo pamoja???????

  Viongozi wa dini hasa hao unaowaona ujumbe wao haung'amuliki kihivyo kama gumzo sokoni, bali ni kwamba maana yao ni sharti umenywe kama chenza ndani ya gamba lake.

  Hakika maana yao viongozi wa dini yapatikana zaidi kwenye kile unachokitafakari na wala si kile unachokisikia.
   
 7. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dk slaa alisema alisema wanaosema kuna udini wanafanya business, sasa mboe anakuja na hili mbona?
   
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Ni lazima wakatae kuwepo kwa tatizo kwa kuwa mission yao haijawa complete.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sina jibu la swali lako hili hapa, kamuone Mhe Mbowe kwa wakati wako.
   
 10. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  inamaana mwenyekiti/katibu different vission?
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii nafsi katika sentensi yako unamzungumzia nani hasa hapa, Mhe Mbowe na Dr Slaa au Maaskofu wawili waliozungumzia udini hivi karibuni???
   
 12. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Ni mawazo mazuri kinadharia............. KIMATENDO JARIBU UONE ............. Fikiri kuhusu hawa...........

  Amina Chifupa
  Edawrd Moringe Sokoine
  Horace Korimba
  etc .......... etc...........

  Walijionyesha kuwa na matendo yaliyobebwa na ujumbe uliouandika.......lakini mwisho wao ulikuwa ni nini.........??? Viongozi wetu huwa wanadhani USAWA ni pale tu wanapofaidika wao............... Watafanya lolote, watamhifadhi au kumtosa yeyote ilimradi tu yao yasijurikane

  Mwangalie Sitta, hebu mcheki Tido Mhando ndo utajuwa uwezo wa hawa watu............ Ukiwa sehemu ni lazima utekeleze ya kwao, vinginevyo utakiona cha mtema kuni
   
 13. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yaani hawa wote watatu: chadema. maaskofu isipokuwa Jk alisema kuna udini. sasa kauli hii mbona inakwenda kinyume na chama chao?
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakati swali lako la hapo juu lilionekana kuwa ni la Mhe Mbowe zaidi, nafikiri hili la sasa ni la kutafutia msaada kiofisi zaidi pale makao makuu ya CHADEMA. Naamini watakusikiliza katika hilo.
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha nini na hii phrase 'chama chao'? Chama cha Maaskofu au cha JK uliemtaja hapo juu?????
   
 16. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe si unatetea? nadhani utakuwa na jibu
   
 17. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  safi sana,mawazo mazuri hayo
   
 18. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Annuur na Alhuda yanamilikiwa na nani? Ni swali tu wakuu
   
 19. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  msemakweli na kiongozi ?
   
 20. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  udini upo,ulikuwepo na utaendelea kuwepo.na miongoni mwa mafunzo ya dini yana chochea ubaguzi, Tatizo wengi wanakariri matukio na tarehe za kihistoria lakini hawajishughulishi kujua phyilosophical consepts za historia.tokaa karne ya 8 kulikua na vita za jihads,karne ya 11 vita ya crusade.sasa alshabab, alqaeda,hizbulah, hamas na makundi mengine yanaendesha mapambano ya kiimani. Mkristo na mwislam hawapikwi chungu kimoja wanatofauti kubwa za misingi ya imani zao. Asanteni sana nawasilisha.
   
Loading...