Tusiache kuiombea Zanzibar na Wazanzibari kwenye Corona

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Ni kweli kuwa Zanzibar ni Tanzania lakini kuna utofauti kidogo kama ifuatavyo:

1. Zanzibar ni ndogo
2. Zanzibar ina watu wachache sana kuliko Bara, yaani ratio ya 1:50, yaani kila watanzania 50 mtu 1 ni Mzanzibar, hivyo kama akifa mzanzibar mmoja ni sawa na kufa watanganyika 50.
3. Zanzibar kiuchumi inategemea zaidi utalii
4. Zanzibar ina Rais ambaye ni Daktari wa magonjwa ya binadamu.

Maana yake Wazanzibar lazima wawe makini mara 50 zaidi ya watanganyika katika kufikiria, kujikinga na magonjwa na hata kuchukua maamuzi yoyote yanayohusisha Tanzania nzima.

Uzembe kidogo tu utaighalimu Zanzibar kiuchumi, kijamii na kiafya, maana wakifa Wazanzibar 2 tu kwa kitu chochote kile ni sawa na kufa Watanganyika 100 kwa kitu hicho.
 
Umechanganya mambo mengi wakati mmoja
Sio mambo mengi kaka, jitihada za wazanzibar kwenye corona kwamfano zinatakiwa ziwe na hadhi ya kimataifa, maana zanzibar inategemea wageni kutoka mataifa mbalimbali
 
Rate uliyotoa haikidhi
Haijakidhi vipi? Population ya Zanzibar ni watu kama 1.5 mil. na ile ya Tanganyika ni kama 50.2 ml. haya Fanya hesabu hapo ya uwiano ili kufahamu ratio ya Tanganyika: Zanzibar. Hii ndio maana wapalestina wakimuua myahudi mmoja Israeli itawaua waarabu 10 kulipiza kisasi. Kama Zanzibar watajifanya kuwa na wao hawana corona kisha wakafa ovyo iko siku visiwa hivyo vitageuka vya watu wa bara. Maana hata wakifa 10 tu hiyo ni % kubwa sana kwao.
 
Back
Top Bottom