Tushirikishane: Uliwezaje kupambana na fikra za uoga ama kushindwa ili kupambana na umaskini, Ni hatua zipi ulizopitia mpaka ukawa vizuri kiuchumi

Cavill

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
249
847
Salaam Ndugu zangu,
Kama title inavyojieleza hapo Juu, hebu tusaidiane kwa Mawazo maana humu Kuna juniors ambao wanaanza game na seniors ambao tayari wameshakutana na changamoto mbalimbali, tuna Wazee wetu humu ndani na Vijana kutoka sehemu mbalimbali ambao kwa pamoja tukichanganya Mawazo yetu tunaweza saidiana kujikwamua mahala tulipo.

Binafsi napitia kipindi Cha mpito, Nina bahati Sana kuanza harakati tangu Raisi Wangu kikwete anamalizia miaka yake ya Mwisho, na Nina bahati zaidi ya kuanza na Raisi wangu wa Sasa ambae Kama mnavyoelewa mambo kidogo yamebadirika.

Nina Elimu ya Chuo Kikuu na mpaka Sasa sijabahatika kupata Ajira Serikalini na Kwa fani niliyosomea Ni rahisi Sana kupata Ajira Sector binafsi Ila malipo ndo hua changamoto. Japo nimeajiriwa Ila bado mambo sio rahisi maana majukumu Ni mengi na Kama unavyoelewa familia zetu hizi ukishasoma wanategemea uwe msaada kwao na kwa nia njema unaweza ukawa unapambana Ila ndio hivyo Hali Ni Tete.

Lengo kuu la Uzi huu Ni Tushirikishane Ni Mbinu gani ulizotumia kukutoa kwenye Maisha ya wasiwasi mpaka hapo ulipo ambapo ishu Kama Kodi ya nyumba, hela ya kula na kuhudumia familia hazisumbui sana.

Tafadhali, Uzi huu unaweza kuwa msaada kwa Vijana wengi haswaa wa kiume maana wengi wao wanakua bila father figure ama mtu wa kuwaongoza kiushauri na kimawazo Nini Cha kufanya na kwa wakati gani, unapochangia jaribu kuwa na hofu ya Mungu ili usije potosha na uwe na Nia thabiti ya kutoa msaada, Asante.
 
Tunapambana na fikira za uoga hapo hapo unasemasema tuchagie tukiwa na hofu ya Mungu. Kuna tofauti gani kati ya fikira za uoga na hofu ya Mungu?
 
Kama una elimu ya chuo halafu ndo unavyojieleza hv kazi ipo?
Mzee uko vizuri kichwani kweli? Kwanza mimi sio mleta uzi nimesema kile ninachokijua kwenye hizi ajira za Sasa.

Pia punguza ujuaji, watu Kama nyie ndio mara nyingi mnakuaga hamjui kitu, ungeweza kumsahihisha kwa hekima na ukaeleweka sio kuanzisha mada nyingine yenye mlengo wa kejeli, haya basi tufanye muanzishe uzi hajafika chuo elimu yake ni darasa la 4B ... Endelea kuchangia mjadala sasa wewe uliyefika chuo

Msomi tunasubiri nondo😀
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mbinu tunazopeana humu ni za kula bata tu zakutafuta pesa ni siri ya kila mtu

Sent using IPhone X
 
Tunapambana na fikira za uoga hapo hapo unasemasema tuchagie tukiwa na hofu ya Mungu. Kuna tofauti gani kati ya fikira za uoga na hofu ya Mungu?

Naamanisha uende moja kwa Moja kwenye point usiweke taarifa za kubuni au uongo, kiufupi uelezee uhalisia ambao wewe umepitia sio hadithi za kina Chris mauki kaka
 
Mzee uko vizuri kichwani kweli? Kwanza mimi sio mleta uzi nimesema kile ninachokijua kwenye hizi ajira za Sasa.

Pia punguza ujuaji, watu Kama nyie ndio mara nyingi mnakuaga hamjui kitu, ungeweza kumsahihisha kwa hekima na ukaeleweka sio kuanzisha mada nyingine yenye mlengo wa kejeli, haya basi tufanye muanzishe uzi hajafika chuo elimu yake ni darasa la 4B ... Endelea kuchangia mjadala sasa wewe uliyefika chuo

Msomi tunasubiri nondo
Kweli mkuu mchane huyo boya, mengne yapo kuangalia makosa tuuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujafanikiwa kupata ajira halafu umeajiriwa sekta binafsi??? Very contradicting story

Shusha nondo kaka, Stori yangu sio ya kutunga.. ndomana unaona ipo ipo tu maana hata mi mwenyewe siielewi ndomana Niko Hapa tupeane mawazo
 
Kama una elimu ya chuo halafu ndo unavyojieleza hv kazi ipo?

Bro Ni Kama umetumwa kuja kuharibu mambo aisee.. Nataman Mods wangetupa mandate za kuwapiga block watu Kama nyie msichangie kwenye thread za watu nahisi hata uraiani unazingua ivoivoo.. Punguza molari kaka
 
Mlango unaweza kuwa ni mmoja lakin sio wote twaweza kupitia hapo,kulingana na maumbo ya miili yetu
 
Back
Top Bottom