Tushirikishane nchi za Afrika zenye mazingira mazuri kwa wawezekaji ukiacha Tanzania

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
Sijawahi kuwaza kwamba itatokea siku moja mfanyabiashara wa kitanzania kuwaza kuwekeza nje ya nchi. Anyway ndivyo ilivyo na itabidi!

Wadau wa biashara ambao pia hua mnakua na updated news za kibiashara katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Naomba tushirikishane nchi zipi barani Afrika ukiacha Tanzania ambayo pana mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wanaotaka kuja kuwekeza katika nchi zao haswa ambao sio wazawa wa hizo nchi.

Nikisema mazingira mazuri ya biashara naamanisha
  • Kutobambikiwa kodi ovyo na tozo kubwa au makadirio makubwa ya kukufanya uache biashara
  • Kutokua na wivu wa mafanikio ya mfanyabiashara
  • Kutochanganya siasa na biashara
  • Kupewa ushirikiano MKUBWA SANA na serikali bila kujali wewe ni wa chama gani na umetokea nchi gani.
  • Kujiskia huru, kupewa usalama, hifadhi, yani KUTUNZWA VIZURI kama mwekezaji na kupewa SPECIAL TREATMENT.
  • Sharia za biashara ambazo sio KANDAMIZI
  • Kua na UHURU wa kuweka PESA zako kiwango chochote hata bilioni 10 alimradi unafanya vitu kwa uwazi, na kama mwekezaji nisiwe na UOGA kua kuna "watu" watakuja kuchungulia akaunti yangu bila "idhini"

Embu tushirikishane hizo nchi tafadhali!
 
Baadhi ya rafiki zangu wamekimbilia Zambia, wanasema kule sheria ni rafiki kidogo kwa biashara. Japo nako siyo Paradiso lakini kuna ahueni kubwa sana ukilinganisha hapa kwetu kwenye utawala wa huyu Economic Vlad The Impaler.
 
Tanzania!
178909098.jpg
 
Malawi na Mozambique kuko vizuri tatizo Mozambique imevamiwa na magaidi ndo naijua inafrisa nyingi sana.

Kwani hata mm nilikuwa na mpango wa kutimkia huko.

Kwa ujumla Nchi zetu nyingi bado mambo ya kufanya yapo ilimradi kufuata sheria za nchi husika na kujuana na balozi wetu ili kujua kuna raia wake yuko hapo na anafanyabiashara flani.

Hii moja ya ngao kubwa kwa kulinda Mali zako
 
Botswana, Rwanda, Namibia, Seychelles ( Hakikisha una vibali vyote), Mauritius , Ivory Coast( Hakikisha una vibali vyote na ujifunze kifaransa), South Africa ( jiandae na gharama za ziada za usalama) .
 
Malawi na Mozambique kuko vizuri tatizo Mozambique imevamiwa na magaidi ndo naijua inafrisa nyingi sana.

Kwani hata mm nilikuwa na mpango wa kutimkia huko.

Kwa ujumla Nchi zetu nyingi bado mambo ya kufanya yapo ilimradi kufuata sheria za nchi husika na kujuana na balozi wetu ili kujua kuna raia wake yuko hapo na anafanyabiashara flani.

Hii moja ya ngao kubwa kwa kulinda Mali zako
Shukrani
 
Back
Top Bottom