Tushirikishane; Matukio ya kikatili kati yetu wanadamu

The August

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
1,089
2,000
Habari wanaJF!

Katika pilikapila za maisha, wanadamu tunakutana na matukio ya aina mbalimbali. Matukio haya yanaweza kuwa ya kufurahisha kama yale ya Dr Shika na Yono, ama ya kusisimua lakini pia yapo ambayo kwa kweli ni ya kikatili sana. Matukio haya ni mwanadamu kuyafanya dhidi ya mwanadamu mwenzake. Ndani ya matukio haya yanatupa mafunzo na kutufanya tuchukue tahadhari fulani fulani.

Uzi huu naomba uwe maalum kwetu kushare matukio haya ili kwa lengo la kujifunza na tahadhari au kinga dhidi ya uhai wetu.


..... NGUDU, KWIMBA, MWANZA, 2015

Mwaka huu rafiki yangu mmoja alikuwa akigombea ubunge katika hilo jimbo. So, kuna wakati nilikuwa nafika kumtembelea as a friend na kupeana msaada wa hali na mali. Siku moja tulikwenda katika kijiji kimoja (sina kumbukumbu hasa na jina lake), lakini kipo takribani km 15 kutoka ngudu mjini kama unaelekea Mwanza kupitia njia ya Ilula.. (nadhani wenyeji watanielewa).

Tukiwa pale, tulikuta kusanyiko la watu wakichimba shimo kama kulifukua ili kutoa kitu ndani ya shimo. Kuuliza walikuwa wakihangaika ili kutoa mwili wa mwanamke aliyefukiwa humo.... Nikataka jua nini kilitokea..!


.... Kama wiki moja nyuma, Bwana mmoja wa kuitwa Masanja alikwenda kwa mganga wa kienyeji kujua chanzo hasa cha vifo vya watoto wake. Alikuwa amefiwa watoto watatu kwa vifo alivyodai havieleweki. Basi, bwana mganga alipopiga Ramli aligundua kuwa chanzo cha vifo ni dada yake masanja ndiye amekuwa akimrogea watoto na kuwaua.

Bwana Masanja sasa akawa amempata 'muuaji wa wanae'.. Naye ni dada yake.. Nyumbani kwake Masanja alikuwa amechimba shimo kwa ajili ya choo.. Siku muafaka, alimkuta dada yake shambani na kisha kumkaba shingo hadi kumuua. Dada yake yule picha yake nilipoiona alikua na ujauzito (wenyeji wanadai ni wa miezi mi3), maumbile yake alikuwa amejaa haswa... Alikua ni Pande la Mama. Katika umri wa kama miaka 40..

Masanja baada ya kumuua, alisubiri hadi usiku kisha akawasha moto na kuanza kumkata kata viungo vyake na kisha kuvichoma moto. Akishachoma anatupia kwenye shimo lile. Alipomaliza akafukia..

Habari za kupotea yule mama zilikuwa kubwa na kuenea kijiji kile chote.... Nadhani wahenga hawakukosea kuwa damu ya mtu haipotei bure... Wakiwa katika mazungumzo ya pombe, masanja alijitapa kuwa yule Mama alimuua yeye kisha akamchoma moto na kumzika. Raia pale, walihamaki na kutoa taarifa kwa mwenyekiti na hatimaye polisi walifika..

Ufukuaji wa shimo lile ulipokamilika,,, viungo vilikusanywa kimoja kimoja.. Shingo ilionyesha alama kama ya shoka... Uti wa mgongo ulionyesha alama kama ya panga... Na vidole vilionyesha alama ya visu.... Kichwa kilikuwa kimepasulia vipande vipande kama anakusudia kutengeneza soup...mtoto aliyekuwa tumboni mabaki yake nayo yalikusanywa... Mwili ule wote kwa ujumla wake ulienea kwenye mfuko wa unga wa azam wa kg 50... Hakika ilikuwa ni unyama na taswira ya kutisha na kuhuzunisha sana.....!!

....

Nilijaribu kudadisi chanzo cha vifo vya watoto, wanakijiji walidai walikua wakiharisha na kutapika... Kwa mazingira ya nyumba ya masanja ilivyokuwa na uchafu, ni dhahiri kipindupindu na typhoid havikukauka pale... (Niliwaza kuwa ndio chanzo cha vifo vya watoto)...


Waganga wa kienyeji.

Matukio mengi ya mauji vijijini ukichunguza mzizi wake uko kwa waganga wa kienyeji.. (Ramli chonganishi). Na sababu ya elimu kuwa ndogo wananchi hawafanya analysis yoyote...Sent using Jamii Forums mobile app
 

STREET SMART

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
769
1,000
Haya mambo huwezi kuyaskia mikoa ya pwani na kusini. Ni mambo ya mikoa ya kanda ya ziwa na Iringa, Rukwa na Mbeya. Mara mmeua mama zenu na bibi zenu kisa wana macho mekundu ya uzee, Mara mmechunana ngozi, Mara mnapigana nondo za kichwa, Mara mmetumiana radi. Kuna tofauti kubwa sana ya ustaarabu.
 

The August

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
1,089
2,000
Haya mambo huwezi kuyaskia mikoa ya pwani na kusini. Ni mambo ya mikoa ya kanda ya ziwa na Iringa, Rukwa na Mbeya. Mara mmeua mama zenu na bibi zenu kisa wana macho mekundu ya uzee, Mara mmechunana ngozi, Mara mnapigana nondo za kichwa, Mara mmetumiana radi. Kuna tofauti kubwa sana ya ustaarabu.
Hiyo ya radi Tabora ni kigoma ndio michezo yao..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom