Tushirikishane Kero mbalimbali za kwenye sherehe

Sote najua tumeshahudhuria sherehe mbali mbali aidha za kualikwa au za kwetu wenyewe.

Kuna vitu hutokea ambavyo hupokelewa tofauti kutegemea na muandaaji.

Kuna vitu hufanyika ambavyo huwa ni kero sana kama sio tatizo kwa baadhi yetu.

Kwa mfano, kuna wapiga picha na watengeza video wanatabia ya kuja na kamera lake usoni kukurekodi na uliamua kukaa meza za ukutani kabisa kule ili usionekane, na hapo unakuta mzee video ikirekodiwa unatokea mdomo unamafuta mafuta mdomoni.... Huwa inanikera sana ile kitu huwa natamani kumlamba kofi mpiga picha.

Nyingine ni wale wapenda sifa wanopenda kuonekana mbele za watu. Wengine hatunaga hizo genes za kumwaga mauno mbele za watu. Unakuta bwege mziki ukipigwa tu ameshatoka mbele halafu baada ya dakika chache anakufuata anaanza kukuvuta na wewe uende mbele mkacheze na unakuta kuna watu sikutaka wajue nipo hapo.....

Pia kuna kero ile ya Mc kukuchoresha kwa kukuita mbele pale na kukupatia mic na haukujipanga kutoa speech siku hiyo....

Hizi ni baadhi ya kero katika sherehe..... Wenzangu huwa mnakerwa na zipi?!
Ndio shamra shamra za sherehe hizo, sharti ushehereshwe!
 
Buffet kukosekana ugali ni kero sana kwa upande wangu nani aliidhinisha pilao,ndugu yke wali na wifi zake biriani kuwa chakula kikuu kwenye shughuli? Imagine mbuzi choma na ugali nikipatamo na balimi nne za moto basi najua binti yangu Salome kapata jembe.
 
Mimi sipendi vile watu wanavyoshindana kuvaa tu,.hivyo nimeamua kuwa nachanga rkn sifiki kwenye shelehe yenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Si wapishi wengi wanaserve vizuri..na kero kweli ni zile foleni muda wa menu,.

ila nishahudhuria sherehe kadhaa kapika Dorka Catering...ndugu msomaji yule mama ni noma kbs...kula ni kwa kusaza
Kwanza ni self service, pili line kama 3, nne kuna vitu fresh wanapika hapo hapoo wewee vitamuu,tano fruits and salads kama zoteee na ice cream juu

na sherehe zngine yuko mtu special wa cocktails muda wowote bila foleni

huwa napenda kuchagua vitu vichache tu ktk buffet ili nienjoy zaidi na sio kuchukua vyote toka point A hadi Z mwishowe tumbo lipate hitilafu buree
Nilimtumia Dorka catering kwenye harusi yangu.

Nimpenda kwasababu ya options nyingi za matunda na salads.

Ila bei zake zimesimama kama una hela ya mawazo.
 
Mi ndo mana tunaendaga shughuli za ndugu ama watu ambao tumezoeana sana ili nifurahie

wengine tunaweza changa ila hatuwezi fika
Bila company hio shughuli siendi naona sitaenjoy

kwakweli sherehe bila company inaboa. itabidi niangalie sherehe zingine nachanga tu siendi.
 
Buffet kukosekana ugali ni kero sana kwa upande wangu nani aliidhinisha pilao,ndugu yke wali na wifi zake biriani kuwa chakula kikuu kwenye shughuli? Imagine mbuzi choma na ugali nikipatamo na balimi nne za moto basi najua binti yangu Salome kapata jembe.
Ha ha ha ha ha ha ha ha. Ndugu, ugali kwenye harusi sijawahi kuona. Labda misibani.
 
Mimi sipendi vile watu wanavyoshindana kuvaa tu,.hivyo nimeamua kuwa nachanga rkn sifiki kwenye shelehe yenyewe.
Mmmmmmhmn sasa ndugu ukishapewa tarehe ya sherehe kinachofuata hapo si ni kuandaa mavazi ya siku hiyo itakapofika
 
Nilimtumia Dorka catering kwenye harusi yangu.

Nimpenda kwasababu ya options nyingi za matunda na salads.

Ila bei zake zimesimama kama una hela ya mawazo.
Kuku na nyama alikuwa anagawa vizuri?!

Kama yupo vema nimuunganishe na rafiki yangu ana shughuli mwenzi kumi.
 
Sherehe yenyewe huwa kero kwangu, hasa Yale maspika wanayofungulia muziki kwa sauti kuubwa ukumbini huwa yanani turn off kabisa. Ukiona nimehudhuria Sherehe yako basi nimekuheshimu sana.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Sherehe yenyewe huwa kero kwangu, hasa Yale maspika wanayofungulia muziki kwa sauti kuubwa ukumbini huwa yanani turn off kabisa. Ukiona nimehudhuria Sherehe yako basi nimekuheshimu sana.
Hapo inatokana na aina ya mtu aliyepewa tenda ya huo mziki.
 
Back
Top Bottom