Tushikeni Mkono nasi tutoke

Finder boy

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
608
150
Wasalamu wanajamvi wenzangu!

Mara baada ya salamu naomba niwasilishe ombi langu kwenu: naomba wale wote wenye kazi zao na ajira zao watushike mkono siye vijana ambao tuko mtaani hatujui kitu cha kufanya. tumejaribu jitihada zetu zote tumeshindwa, hatuna mtu wa kutushika mkono, tuko sisi kama sisi, wazazi, walezi na ndugu zetu hawana uwezo wa kutusaidia.

Tumebahatika kusoma hadi chuo kikuu lakini tupo tu mtaani tunaangaika. Tuliamua kusoma ualimu wetu wa sanaa tukijua mara baada ya kuhitimu tutapata ajira, kumbe tulikuwa ndotoni, ndoto ambayo pengine tulilazimishwa kuiota. Tunaambiwa tujiajiri bila kuoneshwa njia ya kujiajiri, sio kuwa hatupendi kujiajiri, ila tatizo mazingira ya kujiajiri, hatuna mitaji, tukiomba kukopeshwa pesa tunaambiwa hatuna vigezo vya kukopeshwa, tukiomba kwa ndugu na jamaa nao wanakataa kutukopesha kuwa hawana hela, sasa tukimbilie wapi jamani?

Ikumbukwe sisi hatukuchagua kuzaliwa kwenye familia zetu maskini ambazo tumezaliwa na wala hakuna aliyechagua au anayependa kuwa kwenye hali ngumu na mbaya ambayo yuko nayo kwasasa. Yote ni mipango ya Mungu, Mungu aliagiza upendo, tupendane jamani, kwanini wewe huwe na furaha wakati mwenzako ana huzuni na masononeko? Tusaidiane jamani, tushikeni mkono, binadamu tunaishi kwa kutegemeana, pengine wewe uko hapo ulipo maana kuna mtu alikushika mkono, nawe mshike mwingine mkono ili nae aje amshike mwingine huko mbeleni.

Maombi ya kazi tunatuma sana, lakini hatubahatiki kupata, wengine hatupati kwakuwa hakuna mtu wa kutushika mkono, hakuna mtu wa kutuonesha fursa. Ikumbukwe hakuna mtu anayependa kuwa omba omba au kulia shida kila siku, ila ndio maisha yenyewe. Tunafanya vitu tusivyovipenda, tunatukanwa, tunazalilika kwasababu ya shida zetu, kwasababu ya umaskini wetu. Wenye shule zenu tukumbukeni sie walimu ambao hatuna pakwenda, tulijifunza kufundisha sisi, basi tusaidieni jamani. kila mtu na fani yake, hata nje ya fani yake tusaidieni. tupeni izo part time kazi tufanye. kila mtu apate riziki yake na Mungu atawaongezea. kama wahitaji ni wengi basi wagawane hata icho kidogo. kama unalipa mshahara wa laki sita kwa mtu mmoja, sio mbaya kuwa na watu wawili alafu wakagawana laki tatu tatu kwenye hiyo post moja.

Vijana tunahangaika, vitu tulivyojifunza vinakuwa useless, kama ilivyo Imani bila matendo imekufa, basi ni sawa na fani tulizosomea bila kuzifanyia kazi (practice) tutajikuta tunapoteza vyote tulivyojifunza na kungundua kua tulipoteza muda kujifunza vitu vingi ambavyo hatujavifanyia kazi. inayomengi ya kuandika, ila naomba niweke nukta hapa maana majozi yananibubujika.

TUSHIKENI MKONO, NISHIKENI MKONO. ASANTENI.
 
Kijana una umeongea kwa hisia sana ila nje na hiyo taaluma yako ya ualimu nini kingine unaweza kufanya jieleze kwanza mengine ndo yafuate
 
Wasalamu wanajamvi wenzangu!
mara baada ya salamu naomba niwasilishe ombi langu kwenu: naomba wale wote wenye kazi zao na ajira zao watushike mkono siye vijana ambao tuko mtaani hatujui kitu cha kufanya. tumejaribu jitihada zetu zote tumeshindwa, hatuna mtu wa kutushika mkono, tuko sisi kama sisi, wazazi, walezi na ndugu zetu hawana uwezo wa kutusaidia. Tumebahatika kusoma hadi chuo kikuu lakini tupo tu mtaani tunaangaika. Tuliamua kusoma ualimu wetu wa sanaa tukijua mara baada ya kuhitimu tutapata ajira, kumbe tulikuwa ndotoni, ndoto ambayo pengine tulilazimishwa kuiota. Tunaambiwa tujiajiri bila kuoneshwa njia ya kujiajiri, sio kuwa hatupendi kujiajiri, ila tatizo mazingira ya kujiajiri, hatuna mitaji, tukiomba kukopeshwa pesa tunaambiwa hatuna vigezo vya kukopeshwa, tukiomba kwa ndugu na jamaa nao wanakataa kutukopesha kuwa hawana hela, sasa tukimbilie wapi jamani? Ikumbukwe sisi hatukuchagua kuzaliwa kwenye familia zetu maskini ambazo tumezaliwa na wala hakuna aliyechagua au anayependa kuwa kwenye hali ngumu na mbaya ambayo yuko nayo kwasasa. Yote ni mipango ya Mungu, Mungu aliagiza upendo, tupendane jamani, kwanini wewe huwe na furaha wakati mwenzako ana huzuni na masononeko? Tusaidiane jamani, tushikeni mkono, binadamu tunaishi kwa kutegemeana, pengine wewe uko hapo ulipo maana kuna mtu alikushika mkono, nawe mshike mwingine mkono ili nae aje amshike mwingine huko mbeleni. Maombi ya kazi tunatuma sana, lakini hatubahatiki kupata, wengine hatupati kwakuwa hakuna mtu wa kutushika mkono, hakuna mtu wa kutuonesha fursa. Ikumbukwe hakuna mtu anayependa kuwa omba omba au kulia shida kila siku, ila ndio maisha yenyewe. Tunafanya vitu tusivyovipenda, tunatukanwa, tunazalilika kwasababu ya shida zetu, kwasababu ya umaskini wetu. Wenye shule zenu tukumbukeni sie walimu ambao hatuna pakwenda, tulijifunza kufundisha sisi, basi tusaidieni jamani. kila mtu na fani yake, hata nje ya fani yake tusaidieni. tupeni izo part time kazi tufanye. kila mtu apate riziki yake na Mungu atawaongezea. kama wahitaji ni wengi basi wagawane hata icho kidogo. kama unalipa mshahara wa laki sita kwa mtu mmoja, sio mbaya kuwa na watu wawili alafu wakagawana laki tatu tatu kwenye hiyo post moja. Vijana tunahangaika, vitu tulivyojifunza vinakuwa useless, kama ilivyo Imani bila matendo imekufa, basi ni sawa na fani tulizosomea bila kuzifanyia kazi (practice) tutajikuta tunapoteza vyote tulivyojifunza na kungundua kua tulipoteza muda kujifunza vitu vingi ambavyo hatujavifanyia kazi.
ninayomengi ya kuandika, ila naomba niweke nukta hapa maana majozi yananibubujika.
TUSHIKENI MKONO, NISHIKENI MKONO. ASANTENI.
Hili bandiko limtabaruku Waziri wa ajira na utumishi pamoja na Waziri wa Elimu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom