Tushauriane: Umuhimu wa kuandika Wosia

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,761
102,110
Marehemu hasa mwanandoa wa kiume anapofariki huacha mtanziko mkubwa sana kwa mkewe na watoto wake wapenzi
Mke na watoto sio tu hulia sana kwa sababu ya kufiwa na kipenzi chao lakini pia ni maumivu ya dhuruma wanayoweza kufanyiwa na ndugu na jamaa wa marehemu.
Kusema ukweli inasikitisha sana ndugu na jamaa from nowhere wanapowekeza fitna na roho mbaya kudhuruma mali za wanafamilia.
Nimeshuhudia wanawake kadhaa wakisota masikini kupigania mali za familia, huku watoto wakiwa na maisha magumu sana.
Waafrika tumekuwa hatua utamaduni wa kuandika wosia. Waafrika hatuna utamaduni wa kuwa wawazi kwa wenzi na familia zetu. Mfano unakuta mtu ana mali nyingi tu mahali mahali, pengine anawadai mamilioni jamaa zake lakini mkewe au watoto hawana taarifa, jambo linalosababisha kupotea kwa mali hizi baada ya marehemu kufariki.

Lakini pia natoa onyo kali kwa ndugu na jamaa wenye shetani la kudhurumu mali za marehemu. Chuma mali zako, za marehemu waachie mke/mume na watoto wa marehemu.

TUELIMISHANE
  • Umuhimu wa kuandika wosia, pamoja na mambo mengine kumilikisha mali mapema.
  • Hasara za kuandika wosia.
  • Taratibu za kuandaa wosia utakaotambulika kisheria.
  • Gharama za kuandaa wosia
  • N.k
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom