Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,516
Niliposoma humu kuwa eti Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi ' ametia aibu' nchi kule Kenya, nikasita kuamini au kutoamini kwakuwa sikuwa nimeiona au kuisikia hotuba yenyewe. Baada ya kuiona na kuisikia hotuba husika, sioni hoja za wasema-hivyo.
Katika hafla hiyo ya Uwasilishaji wa Ripoti ya BBI pale Bomas Kenya, Prof. Kabudi, kama Mwakilishi Maalum wa Rais Magufuli alipata nafasi ya kutoa neno mbele ya halaiki iliyokuwepo pale ikiongozwa na Rais wa Kenya, Makamu wa Rais wa Kenya na Kiongozi wa Upinzani wa Kenya.
Kwanza, Prof. Kabudi alianza kumshukuru Mwenyezi Mungu; kumshukuru Rais wa Kenya na hata Rais Magufuli kwa uwepo wake pale kwenye jambo muhimu kwa Kenya, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Pili, alionyesha kwa mifano uhusiano wa kindugu uliopo kati ya Kenya na Tanzania.
Tatu, Prof. Kabudi aliwafikishia Wakenya salamu za Rais Magufuli hasa kuwaunga mkono Umoja wa Mataifa na kuwafikishia ujumbe wake ambao ulijikita katika kuwataka wajirekebishe na kusonga mbele pamoja wakiwa wamoja. Akawasihi waweke mbele maslahi ya nchi yao badala ya wao mwenyewe kwakuwa nchi huanza.
Prof. Kabudi, pamoja na mambo mengine, alionesha tofauti kati ya Tanzania na Kenya kuhusu makabila na ukabila ambao huathiri pakubwa siasa na utengemano wa kitaifa nchini Kenya. Akawasihi kutoyaweka makabila mbele na juu ya Kenya. Wakati wote wa neno lake, alishangiliwa na meza Kuu pamoja na kaumu mzima iliyokuwepo. Alishangiliwa kwa ukweli wake ambao hakuwa anapepesa kuutoa.
Hafla ile haikuwa ya kuzungumzia mikataba ya kimataifa na hivyo kuzungumzia mikataba hakukuwa mahala pake. Hafla ile haikuwa kuzungumzia uchaguzi na hakufanya hivyo. Sasa amekosea nini na amekosea wapi? Hata mwishoni alifikisha ujumbe wa wazi wa moja kwa moja kwa Rais Kenyatta, Makamu wa Rais Ruto na Mzee Raila Odinga na wote waliukubali na kuufurahia wakichagizwa na shangwe za wananchi wao.
Prof. Kabudi hapaswi kuponzwa na ukweli wake kwa ndugu zetu Wakenya. Hapaswi kuponzwa na uwazi wake wa kuufikisha ukweli. Hafla ile ililenga kupata maridhiano na umoja ili kusonga mbele kama Wakenya. Ndiyo maana kaumu nzima ilishikana mikono na kumfuatilia Prof. Kabudi aliyewaongoza katika kauli na ahadi za kujenga Kenya mpya.
Tabia ya kuona kila kauli ina makosa ni kujenga tabia mbaya na inayotesa. Washika-bango muwe makini na mjiepushe na tabia zisizojenga!
Pia soma

Prof. Kabudi ahudhuria hafla ya uzinduzi ripoti ya BBI nchini Kenya inayopendekeza uwepo wa cheo cha Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Waziri wa mambo ya nje Prof. Kabudi amehudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Building Bridge Initiatives (BBI) nchini Kenya ambayo imehudhuriwa na viongozi wote wakuu wa Jamhuri ya Kenya. Miongoni mwa mapendekezo ya BBI ni haya: 1. Uwepo wa cheo cha Waziri mkuu ambaye ni lazima awe Mbunge wa...
www.jamiiforums.com