Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Nimeyasikia na kuyafuatilia matokeo ya Kidato cha Nne waliomaliza mwaka jana 2016. Matokeo hayo yalitangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Walioongoza wameongoza; walioongozwa wameongozwa; waliofaulu wamefaulu na waliofeli wamefeli.
Binafsi, naamini kuwa ustawi wa elimu Tanzania huonekana kupitia Shule za Serikali. Huko ndiko wanapopatikana watanzania asilia. Huko hupatikana watanzania wa kawaida wanaosoma katika mazingira ya kitanzania hasa. Wanaofaulu huko, hufaulu kweli.
Shule za Sekondari za Serikali, hakika, ni kioo cha ustawi wa elimu Tanzania. Kutokana na uiamara wa Serikali, ilitegemewa kuwa angalau Shule za Serikali zingechomoja hapa kumi bora katika matokeo hayo. Hali inakuwa kinyume kila kukicha. Shule binafsi zinaendelea kutamba.
Shule binafsi, kwa maoni yangu, husheheni watoto wa watu wa tabaka fulani. Kufaulu kwao kwa kiwango cha juu kunaongeza nafasi kati ya tabaka lao na tabaka la wale wasomao Shule za Serikali. Hii si dalili nzuri kinchi. Wale wanaofeli kwa maelfu waelekee wapi?
Kutamba kwa shule binafsi na kufanya vibaya kwa shule za Serikali kunaleta picha gani? Kunaleta picha kuwa Serikali ina kazi ya kufanya katika nyanja ya elimu ya Tanzania. Inapaswa kufanya tafiti kupitia wadau wa elimu kujua tatizo. Ipo haja ya kuangalia na maslahi ya walimu.
Hali hii ikiendelea, maskini wa kitanzania watafeli kwa maelfu kidato cha nne na kutengeneza magenge hatari mitaani. Lengo la elimu ya bure si tu mwanafunzi afike kidato cha nne; afike na kusonga mbele zaidi. Anayefeli kidato cha nne hana tofauti yoyote na darasa la saba.
Nimalize kwa kupongeza shule na wanafunzi waliofanya vyema. Nitoe pole kwa shule na wanafunzi waliofanya vibaya. Kubwa zaidi, Serikali naishauri kutafiti na kujua tatizo linalokumba shule zake hadi kufelisha kwa kiasi kinachotokea. Elimu yetu ni roho ya Taifa letu.