Tuseme wananchi walivunja sheria kujenga eneo la barabarani, iweje serikali/PPF nayo ikaweka jengo la Tanesco?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,141
18,769
Hi Suala la Raisi Magufuli kushikilia msimamo kwamba wananchi waliobomolewa nyumba eneo la Ubungo walivunja sheria kwa kujenga eneo la barabarani halijawahi kuniingia akilini hata siku moja. Siku zote nimeona bomoa bomoa hii imefanywa kwenye misingi ya ubabe na uonevu na sio misingi ya sheria. Watu waliobomolewa wanastahili kulipwa fidia.

Kwanza fikiria, tukisema kwamba wananchi waliobomolewa walivunja sheria, ina maana kwamba nyumba zote zilizobomolewa hazikuwa na kibali cha kujengwa, kibali ambacho hutolewa na serikali. Je hili linawezekana, kibali kutolewa na tasisisi ya serikali ambayo inavunja sheria katika kutoa kibali? Ni sawa na kusema siku moja naweza kupigwa faini na trafiki kwa kuendesha gari nikitumia leseni niliyopewa na TRA! Ukitaka kujua haliwezekani, jaribu kujenga kibanda sehemu ambayo hustahili kujenga, na utaona kwamba watu wa jiji wanakuja kukubomolea kabla hata hujamaliza kujenga msingi!

Pili, tuje kwenye hili jengo la Tanesco, ambalo nasikia lilijengwa na PPF. Tanesco na PPF zote ni taasisi za serikali. Hivi inaweza kuingia akilini kwamba PPF au Tanesco walisimamisha hili jengo kwa kuvunja sheria kimakusudi, na ndio maana leo jengo hili la Tanesco linastahili kubomolewa? Je, jengo hili lilijengwa bila vibali na baraka za Jiji? Na vibali vitatolewaje katika mazingira kwamba utoaji wake unakuwa unakiuka sheria? Inaingia akilini hiyo? Kwa hiyo tumshitaki mkurugenzi wa PPF kwa kufuja fedha (bilioni 51 za hili jengo) kwa kujenga sehemu ambayo alijua ujenzi wake ulivunja sheria? Na vipi taasisi iliyotoa vibali vya ujenzi wa jengo hili?

Kwa hiyo suala ni kwamba, kama wananchi walikiuka sheria kujenga eneo la barabara, ilikuwaje serikali yenyewe (PPF, Tanesco) ikakiuka sheria kwa kujenga jengo ndani ya eneo la barabara?

Na tatu, kisheria, labda wanasheria mtusaidie hapa. Je ikiwa kuna sheria ambayo haisimamiwi (law that is generally not enforced), na imekiukwa kwa miaka mingi bila kuwa enforced, ni halali kuchukua hatua dhidi ya uvunjaji wa hiyo sheria miaka zaidi ya 10 baadaye? Kwa maneno mengine ninachouliza ni kwamba, ikiwa nasimamisha jengo mahali fulani kwa kuvunja sheria, je ni halali kusubiri nikamilishe hilo jengo, nilitumie hilo jengo kwa zaidi ya miaka 10, na ndio uje kuniambia kuwa unajua ulipojenga hili jengo miaka 15 iliyopita ulivunja sheria hivyo leo ndio nimekuja kukuchukulia hatua?

Nitarudia tena. Kwa maoni yangu ni kwamba suala la Raisi Magufuli kushikilia msimamo kwamba waliovunjiwa wasilipwe fidia ni la kiubabe na kiuonevu na siyo kisheria. Na ubabe na uonevu huu ulidhihirika pale ambapo tuliona hata zuio la mahakama la kuzuia zoezi la bomoa bomoa likidharauliwa. Waliobomolewa wanastahili kulipwa fidia, ikiwa ni pamoja na jengo la Tanesco ikiwa litabomolewa. Hata kama kwa namna moja au nyingine walivunja sheria, basi si wao waliovunja sheria bali taaisi za serikali ndizo zilivunja sheria, yaani serikali yenyewe. Na kama ni serikali ilivunja sheria kwa kuruhusu ujenzi wa nyumba za watu na jengo la Tanesco, basi serikali haipaswi kuadhibu watu kwa kosa lililofanywa na serikali yenyewe. Lazima fidia ilipwe, la sivyo itamkwe wazi kwamba kinachofanyika hapa ni ubabe na uonevu.
 
hawa viongozi wetu hasa hawa ma Dr na ma prof wanatakiwa wawe wanapimwa akili.


Dr. luis shika nae ni Dr. angekuwa kiongozi pia angepiga kazi tuu na angekuwa na maamuzi kama Haya.
 
Siku inakuja ambayo mahakama itawapa ushindi wananchi hawa na CCM watatuambia Raisi alishauriwa vibaya.
 
Kwa kweli wakulaumiwa ni PPF kwa kufanya bad investment. Huwezi chukua michango ya watu na kujenga kitega uchumi katika eneo la hifadhi ya barabara???
 
Kwa kweli wakulaumiwa ni PPF kwa kufanya bad investment. Huwezi chukua michango ya watu na kujenga kitega uchumi katika eneo la hifadhi ya barabara???

Serikali na vyombo vyake vyote vinavyohusika walikuwa wapi toka jengo linaanza kujengwa hadi linamalika?!

Serikali haiwezi kukwepa lawama kwenye hili.
 
Serikali na vyombo vyake vyote vinavyohusika walikuwa wapi toka jengo linaanza kujengwa hadi linamalika?!

Serikali haiwezi kukwepa lawama kwenye hili.

Kama serikali ilitoa vibali vya ujenzi, basi fidia inastahili, sawa tu na kwa wnanachi waliobomolewa. Ndio maana nikasema mtu yeyote aliyejenga mahali popote akiwa na kibali kinachotolewa na taasisi ya serikali, akibomolewa jengo anastahili kulipwa fidia.
 
Kama serikali ilitoa vibali vya ujenzi, basi fidia inastahili, sawa tu na kwa wnanachi waliobomolewa. Ndio maana nikasema mtu yeyote aliyejenga mahali popote akiwa na kibali kinachotolewa na taasisi ya serikali, akibomolewa jengo anastahili kulipwa fidia.

Mkuu hoja yako nakubaliana nayo kabisa.

Jibu langu nimem-quote mtu ambaye alielekeza lawama kwa PPF pekee.
 
Back
Top Bottom