Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,316
- 24,181
Tulio sekta ya ujenzi bado hatujatengemaa kutokana na vurugu tulizopitia miaka hii mitano.
Kabla ya kupata urais Magufuli na sekta ya ujenzi tulikuwa chanda na pete.
Mikutano yote ya wajenzi alihudhuria tena kwa kujipigia chapuo kubwa kwa Rais iwe Mkapa au Kikwete.
Sasa alipopata Urais tukifikiri sasa tutakula bata!
WACHA!
Kwanza kazi zote za serikali akaamuru wapewe TBA, JKT-SUMA Magereza.
Consultancy zote zikaamriwa zifanyike Chuo cha ARDHI.
Hapo makampuni mengi tu yakafa, iwe ya ujenzi au ya consultancy.
Hatujakaa sawa Mwamba akaamuru kazi zote zifanywe kwa mtindo wa Force Account.
Kuna watendaji serikalini wakaenda mbali na kuwapiga marufuku makandarasi katika kazi zozote za Halmashauri au serikali!
Makampuni mengi yakafa mkupuo wa pili.
Sekta aikadhurika sana.
Sekta hii duniani kote ndio ina sambaza fedha kwa uchumi na umma, iwe vibarua, mama ntilie, mabenki na hata ulipaji wa kodi.
Mpaka sasa sekta haijatengemaa vizuri hata baada ya kuona madudu ya TBA, SUMA-JKT, MAGEREZA na vyombo vingine vya serikali ambavyo kuna sehemu vimefanya kazi chini kabisa ya viwango na havisambazi fedha kwenye uchumi.
Tukubali tu Magufuli aliivuruga sekta ya ujenzi akiwa Rais.