Tuseme ukweli: Kukiwa na dharura ya mchango kwa haraka, wewe na ndugu zako mnaweza kukusanya kiasi gani mkichangishana?

Mimi na ndugu zangu tukichanga itakuwa 60,000/mwisho yaani tena hapo mimi nimetoa 20 waliobaki wametoa 10 elf.
 
Katika maisha ya binadam!

Mara zote kimbilio kuu huwa ni ndugu katika kutatua jambo la dharula! Kwa unavyowajua ndugu zako!

Wewe na ndugu zako kukiwa na jambo la dharula na mkaamua kuchangishana hapo kama wana ndugu ndani ya siku moja au mbili mnaweza kupata top top Tsh ngapi ile Maximum kabisa hata tukiwapatia Maiki mseme mlichopata kitakuwa ngapi?

(Wewe na ndugu zako pasipo kuhama ukoo tafadhali)
sisi tukiamua zinafika TSH 222222222222222222222222222222222222222222222222222222222222222222456789000000000
 
inategemea tuachangia nin kama harusi au msiba miliion tano inafika kama ugonjwa million 3
 
Hata sijui, hili swali fikirishi. Yaani Mungu atusimamie. Binafsi sina hela hapa na inayopatikana inasambaratika na kugawanyika kabla hata, sijaitia mikononi. Tukipata 30-50, itakuwa kweli sisi ukoo wa wanaume!

Everyday is Saturday............................... :cool:

Dah
 
Ngoja nimsemee jirani yangu hapa kanituma niwaambie kuwa katika familia yake yeye wana uwezo wa kupata si chini ya milioni 100 kama itahitajika kwa dharura.
Baba anawezatoa 30 ml papo hapo
Mama 20ml
First born 50ml
Last born 50ml bila shuruti
Baada ya nijisemee na mimi mwenyewe sasa- tunaweza pata elfu kumi kwa kubanana sana tena kwa kipindi kisichopungua mwezi
 
Hili swali niliwahi kulisikia kwa Musa Hussein akimuuliza Geah Habib kuwa likitokea la kutokea ghafla pah kila mwanafamilia achange mtapata Bei gani?

Hili liliniumiza Sana moyoni kuanzia mm mwenyewe nlikuwa pu*bu mbaya tena nakumbuka ndo kwenye ajali aisee niliomba Sana nikirud road nipambane MUNGU aweke mkono wake pia jaribu kuwashirikisha mawazo ya kuongeza kipato ndugu zako haijalishi watakukubali au watakataa Ila wewe tayari umelitoa jema sometimes hata ka mtaji sio mbaya.

Hili swali n gumu na fikirishi sana linapima Hali ya kipato cha familia zetu jamani tupambane aisee
 
Ngoja nimsemee jirani yangu hapa kanituma niwaambie kuwa katika familia yake yeye wana uwezo wa kupata si chini ya milioni 100 kama itahitajika kwa dharura.
Baba anawezatoa 30 ml papo hapo
Mama 20ml
First born 50ml
Last born 50ml bila shuruti
Baada ya nijisemee na mimi mwenyewe sasa- tunaweza pata elfu kumi kwa kubanana sana tena kwa kipindi kisichopungua mwezi
30+20+50+50 jumla utapata 100 tangu lini
 
Back
Top Bottom