Tuseme tu ukweli, ujenzi unahitaji kujinyima sana

Kimsingi akuwekee quotation,
Nenda kwenye maduka kazunguke uulize bei zao!
Kama ni vifaa waweza pata kwa ma agent nenda kwa hayo maduka,
Utapunguza kwa kiasi fulani upigaji

Pole ndugu

Wenye maduka wakiona tajiri wanamtajia bei juu 95%
 
Nimetumia kichuguu cha nchwa kujazia kifusi kwenye nyumba.. hapa naambiwa nahitaji kuikinga saana iyo nyumba kuhusiana na nchwa...

Napagawa tu hapa sielew hata napiga dawa gani .
Msaada wadau

Heee kuna ubaya?

Mi nilijaza kifusi cha kichuguu. Na fundi alinishauri
 
Heee kuna ubaya?

Mi nilijaza kifusi cha kichuguu. Na fundi alinishauri
Aah aah aaah.... Ubaya upo bro. Inatakiwa upige dawa pale chini nyumba nzima.. then upige zege floor inch kama moja upana hivi... Afu dawa teena then tiles zifate.. na kech zipige hata oil chafu.

Nchwa wasee saaana utakaa miaka kadhaaa utaona wanatokeza..

Labda pengine una bahati walisepa wenyewe aaah aah

Mi natafuta aina ya dawa tu
 
Hakika changamoto ni nyingi.

Tunaendelea kujifunza na tuko tayari kutoa ushauri wa kitaalamu katika eneo tunalolimudu.

Poleni wadau. Tupo pamoja.
 
Fundi kaniambia et kuta atainua wa million tatu!!!!

Vyumba vipo vi5
Nkaona ujinga hu ngoj nili pozi njichange
Wakat naendelea kawaza kuna mwingine kaomba kazi atajenga kwa laki9
Nae bado nnamfikilia hapa

Hapa pana shida,huyu wa laki9 hiyo dificit 2.1 mill ataitoa wapi?

Unapochuja mafundi uchuje kwa akili utakuja kukutana na mafundi wa bei rahisi wakupige materials mpaka uchanganyikiwe,binafsi naamini (kama ni Dar) huyu wa mill tatu yupo kwenye nafasi nzuri ya kufanya kazi yenye ubora maana anaonekana anajua anachokifanya.
 
Nimetumia kichuguu cha nchwa kujazia kifusi kwenye nyumba.. hapa naambiwa nahitaji kuikinga saana iyo nyumba kuhusiana na nchwa...

Napagawa tu hapa sielew hata napiga dawa gani .
Msaada wadau
Ulikosea mkuu wenzako wanakimbia vichuguu wewe unahamishia ndani?

Hata mimi nilikutana na changamoto ya mchwa sasa namna ya kuwathibiti fanya hivi,nunua sumu ya mchwa tafuta watu wanaohusika na fumigation kabla hujamwaga jamvi (ile zege ya kupokelea tiles) wamwagie nyumba nzima kisha jamvi lije juu.

Kisha kila baada ya muda fulani let say mwaka ½ unanunua tena sumu ita mtu achimbe pembeni ya ukuta kwa nje nyumba nzima kiasi cha fut 1 kwenda chini amwage mchanga (huu wa kujengea) kisha amwage sumu juu yake then udogo kufunika.

Ni mazingira yameshakuwa hivyo huna namna ya kufanya.
 
Tukiona vijana wanajinyima starehe, anasa, matumizi holela tunafurahi sana.

Leo ni siku ya vijana kufunguka: Ni changamoto gani ulikutana nayo au unakutana nayo wakati unajenga nyumba yako? Umekwama wapi?

Shea nasi uzoefu tujifunze kwa pamoja.
Nimejenga nyumba kwa gharama kubwa kwa uwezo wangu then naona crack ukutani kutokana na jua hili miaka yote sijaona crack isipokuwa mwaka huu
 
Mi bado kupaua ila mh!!!! Bati tu nimeambiwa Milioni 4 na Jua hili linavyochoma hadi Mifuko nipo hoi!!!!
Unfortunately kila siku bati zinapanda,tuseme ukijikusanya ukapata hela ya kununua bati disemba mwishoni ukaingia dukani kununua unakuta tena pesa haitoshi.

Ni wakati mgumu mno!
 
Back
Top Bottom