paul sylvester
JF-Expert Member
- Mar 18, 2020
- 3,504
- 3,499
Nilizaliwa Tanzania na nitakufa na kuzikwa Tanzania.
Watanzania wengi sana tunapenda vitu vizuri, lakini kanuni ya vitu vizuri ni Lazima uumie Kwanza wakati unaelekea vitu vizuri, hii ndiyo kanuni ya maisha.
Katika nchi yetu kumekuwepo na kauli mbiu ya Tanzania Lazima tujitegemee.
Ni Jambo Jema sana lakini linamaumivu yake kabla hatujafikia huko.
Tumekuwa na vyanzo karibu vilevile vinavyoingiza pato la Serikali Kwa Maana ya Kodi Kwa miaka mingi SASA, wakati huu tunapoelekea kwenye azima ya serikali ya kujitegemea ni vema kila mtanzania aweze kulipa japo Kodi hata ya sh. 1000 Tu Kwa mwaka.
Ili kila mtu alipe Kodi Kwa ajili ya ustawi wa nchi yake basi ni vema kukatafutwa namna ya kila mtu kulipa hiyo Kodi.
Binafsi ningependekeza kwamba, umefika wakati sasa Kwa kila mtu anayesafiri kwenda mikoani alipe kodi,na Kwa kila tiketi anagalau iwepo Kodi ya 1000 Itakayoingia serikalini.
Lakini Kodi hiyo itamhakikishia msafiri huyo, pindi kunapotokea ajali, iwe bima ya matibabu yake.
Kwa kukadiria tu, pengine kila siku huwa zinauzwa tiketi zaidi ya Elfu 50,000/ tu kwa siku, Maana yake kila siku serikali itakuwa ikpata Kodi ya m.500.
Na utaratibu huo uwe wa moja Kwa moja pindi msafiri anapokata tiketi yake, mf, kama nauli ya kwenda Mwanza ni Tsh 40,000, basi itambidi alipe Tsh 41,000 Kwa Maana ya hiyo elf 1 inayozidi ndio Kodi ya serikali.
Nawasilisha