Tusaidie Serikali kubuni na kutoa mapendekezo mapya ya Kodi ili kuimarisha mpango wa kujitegemea

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,513
2,000
Nilizaliwa Tanzania na nitakufa na kuzikwa Tanzania.

Watanzania wengi sana tunapenda vitu vizuri, lakini kanuni ya vitu vizuri ni Lazima uumie Kwanza wakati unaelekea vitu vizuri, hii ndiyo kanuni ya maisha.

Katika nchi yetu kumekuwepo na kauli mbiu ya Tanzania Lazima tujitegemee.

Ni Jambo Jema sana lakini linamaumivu yake kabla hatujafikia huko.

Tumekuwa na vyanzo karibu vilevile vinavyoingiza pato la Serikali Kwa Maana ya Kodi Kwa miaka mingi SASA, wakati huu tunapoelekea kwenye azima ya serikali ya kujitegemea ni vema kila mtanzania aweze kulipa japo Kodi hata ya sh. 1000 Tu Kwa mwaka.

Ili kila mtu alipe Kodi Kwa ajili ya ustawi wa nchi yake basi ni vema kukatafutwa namna ya kila mtu kulipa hiyo Kodi.

Binafsi ningependekeza kwamba, umefika wakati sasa Kwa kila mtu anayesafiri kwenda mikoani alipe kodi,na Kwa kila tiketi anagalau iwepo Kodi ya 1000 Itakayoingia serikalini.

Lakini Kodi hiyo itamhakikishia msafiri huyo, pindi kunapotokea ajali, iwe bima ya matibabu yake.

Kwa kukadiria tu, pengine kila siku huwa zinauzwa tiketi zaidi ya Elfu 50,000/ tu kwa siku, Maana yake kila siku serikali itakuwa ikpata Kodi ya m.500.

Na utaratibu huo uwe wa moja Kwa moja pindi msafiri anapokata tiketi yake, mf, kama nauli ya kwenda Mwanza ni Tsh 40,000, basi itambidi alipe Tsh 41,000 Kwa Maana ya hiyo elf 1 inayozidi ndio Kodi ya serikali.

Nawasilisha
 

concordile 101

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
1,249
2,000
Kwangu Mimi sion mantiki ya kupunguza mpaka buku, ila wangeachia kukawa Kuna free market tu. Namaanisha badala ya kuwapanga nauli waache Bei iendane na soko. Pia wakatoa tozo zote Kama latra,Kodi za vituoni tukabaki na vat na lesen ya biashara. Vat ikabakia pale pale asilimia 18.

Zaidi ya hapo ili kuzidi kuvutia biashara tungeruhusu hata hayo mabasi ya 15mt yafanye kazi kwetu tukaongezea na vitela nyuma visivyozid tan 10.

Sasa tukija kimahesabu Basi la abiria 50 kwenda mwanza kwa nauli ya juu kabisa ya 67000tsh
67000*0.18=12060

Kwa kila siti vat itakuwa 12060*50=603000
Kwa Basi moja vat 603000

Kukiwa na mabasi letsay 50 kwa ruti ya mwanza serikali itakula Mil30. Kwa mwezi 900 kwa route ya mwanza tu.

Tukija kwenye mazao serikali ingeachana na masuala ya kuzuia uuzaji nje wa mazao badala yake ili kujiongezea kipato ingeweka kikodi kidogo Cha kuexport mazao.

Tuchukulie mfano Mahindi Kodi ya kuvusha kwa kilo ikiwa ni 10tsh/kg

Kwa kila semi itayovuka boda baada ya Kodi nyingine zote Basi serikali itajipatia karibia 300000tsh. Kukiwa na semi 2000 kwa mwezi kwenda boda mbali mbali kwa mazao mbalimbali hiyo ni 600mil si ndogo

Ili Kodi iweze patikana kwa wingi ni serikali kuachana na Sera mbovu waje na Sera za kuvutia watu.

Walau hata Kama hawajaendelea lakini Zambia Wana Sera nzuri sana laiti zingekuwa ziko tanzania tungekuwa tunaongea mengine. Ntaamini watanzania wanajituma Sana ukilinganisha na wanaotuzunguka ila Sera zetu si nzuri.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,513
2,000
Kwangu Mimi sion mantiki ya kupunguza mpaka buku, ila wangeachia kukawa Kuna free market tu. Namaanisha badala ya kuwapanga nauli waache Bei iendane na soko. Pia wakatoa tozo zote Kama latra,Kodi za vituoni tukabaki na vat na lesen ya biashara. Vat ikabakia pale pale asilimia 18....
Mawazo mazuri Sana chief
 

Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
493
1,000
Inaelekea unaishi nchi nyingine kabisa, tatizo la nchi sio watu hawalipi kodi, Tatitizo ni kodi zimekua Kubwa na nyingi hazilipiki. na ndio sababu Serikali inakosa pesa. utaratibu wa kuongeza mapatao haujawahi badilika punguza kodi, punguza idadi ya kodi, ruhusu watu walete pesa,tekinolojia na uzoefu nchi na kura Rafiki kwenye kushughulikia makosa ya kibiashara. hivyo ndivyo China, Singapore, Europe,na nchi zingine zilizoendelea wanafanya, kama kuna makosa wanakaa mezani na kama ni kulipa company au mtu analipa au anaelekezwa ili asirudie makosa, ktk biashara kuna makosa mengi sana, na yanafanyika bila kukusudia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom