Mmasihiya
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 389
- 170
Kwa kuwa viongozi wakuu kitaifa wanaendelea na utumbuaji majipu kwa viongozi wasiofaa hasa wenye madaraka makubwa kitaifa, ni vema tukawasaidia kutambua watendaji wanaostahili motisha katika ngazi za halmashauri kwa utendaji wao uliotukuka lakini pengine hawaonekani na pia tusaidie kutambua wanaostahili kutumbuliwa majipu kwa utendaji wao usiofaa (kujiona miungu watu) ukizingatia ofisi za halmashauri zinahudumia wananchi wengi wa hali ya kawaida na watumishi wa kada mbalimbali walio chini yao kwa ukaribu zaidi na mara nyingi viongozi wa kitaifa wakifanya ziara halmashauri husika huwa kuna utaratibu wa kufunika kombe mwanaharamu apite biashara irudi kama zamani.....