Tusaidiane namna kukomesha wizi wa nyaya za umeme baada ya kufanya wiring

Nyakitagara

Member
Feb 7, 2019
49
81
Habari za jioni Jukwaa,

Naomba msaada wa kuzuia wezi wa nyaya za umeme, mwezi mmoja umepita nimefanya wiring kwenye nyumba yangu na sasa inanibidi nirudie tena hii ni baada ya mwizi wa waya kuingia na kukata kata nyaya kwenye main switch na juu kwenye dali, inasikitisha sana pale unapofikiri umemeliza hatua na unarudi tena nyuma hatua kumi. Ni nani wanaonunua nyaya hizi na kufanya wengine tupate hasara kubwa?

Na hii imetokea na kwa jirani yangu week hii.

Nawezaje kupambana na hawa wahuni?
 
Hello Nyakitagara, ushauri wangu kwako, ongea ni fundi wako achore mchoro apeleke tanesco baada ya hapo atafute survey kutoka tanesco kwa ajili ya ukaguzi. Baada ya hapo fuatilia control number ili ufanye malipo utafungiwa umeme ndani ya mwezi mmoja.

Ni muhimu afunge bracket, na awe na cut out fuse baada ya kuwekewa umeme ndio amalizie kufanya wiring na kuruhusu umeme ndani ya nyumba.

Hilo litawezekana kama hutakuwa na mkono mfupi ili kupunguza gharama za wiring. Weka mlinzi wa muda mpaka pale utakapovutiwa Umeme
 
Nimeweka grill.wamepita kwenye sehemu ya grill niliweka kama emergency door kama kuna dharura ya moto.
Ndio tafuta mtu aishi hapo kwa muda,hizo kesi mbona zipo sana huku kwetu Chanika,kila siku watu wanalia mm mwenyewe juzi sijarudi nyumbani jamaa wameingia wamevunja mabanda yangu ya sungura sijakuta hata mmoja,hapa nataka niwasiline na babu nimtoe mtu mgoro
 
Ndio tafuta mtu aishi hapo kwa muda,hizo kesi mbona zipo sana huku kwetu Chanika,kila siku watu wanalia ,mm mwenyewe juzi sijarudi nyumbani jamaa wameingia wamevunja mabanda yangu ya sungura sijakuta hata mmoja,hapa nataka niwasiline na babu nimtoe mtu mgoro
Nakuelewa mkuu. Wizi mbaya Sana,
 
Tatizo mkuu ni value ya hizo nyaya zenyewe...single core moja ya 2.5mm inakwenda laki moja. Copper kilo moja elfu 8. Kwa hesabu za haraka haraka.

Nikija kuiba nyaya zote ndani ya mjengo wako naweza kupata hata Kilo 10 ambayo 80, 000/= kazi ya dakika chache. Nikisema niuze waya kama waya mzigo wote nilioiba naweza kupata hata 200k

Fuata ushauri wa majamaa hapo juu, tatizo vitu vyenye thamani tunavichukulia poa. Mimi wameniibia pikipiki yangu mpya kutokana na uzembe wa kuilaza nje, jamaa wakapita nayo japo kuna uzio na makufuli kibao.
 
Nyaya hizo wanachoma kisha wanauza copper kule gerezani. Wengi wao ni hao hao mafundi.
 
Nimeweka grill.wamepita kwenye sehemu ya grill niliweka kama emergency door kama kuna dharura ya moto.
Kumbe jibu unalo. Hakikisha nyumba iko full secured ndio utandaze nyaya. Kama nyumba imejitenga sana weka mlinzi.
 
Nimeweka grill.wamepita kwenye sehemu ya grill niliweka kama emergency door kama kuna dharura ya moto.
Me walikata grill yangu ya mlango nyumba ilikuwa haijaisha, wakaiba makorokoro kibao mwaka wa juzi

Sijui walitumia Nini kukata, ndiomaana sasaivi nikikamata mwizi Sina huruma nae
 
Back
Top Bottom