Tusaidiane kujibu maswali haya jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusaidiane kujibu maswali haya jamani!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mpeni sifa Yesu, Dec 18, 2010.

 1. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  UTAFANYEJE YAKIKUKUTA HAYA MAMBO HAPA CHINI?

  1. Umeoa mke, na umezaa naye watoto watano, wengine wako shule ya msingi wengine chekechea

  2. una tabia ya ulevi kila mtu mtaani anakujua.
  3. mara nyingi unarudi umejichafua haja kubwa kenye suruali, harufu inaanzia getini unapoletwa, unakojoaa kitandani ukilala kwasababu umekunywa bia lita kumi zikakwangua chakula tumboni hadi kwenye rectum. ndo maana unaendesha bila kujipendea mbele za watoto.

  4. watoto kila siku wanakuona unarudi umejinyeaa, umeloa mikojo, pengine huletwa na tolori au tax

  5. wakati mwingine ukiwa home umelewa unatoka sebuleni kwa watoto unakojoa sebuleni ukifikiri ni chooni kwasababu ya ulevi. watoto wanayaona maungo yako.

  6. watoto wameyaona maungo yako ya siri, wameshakuona ukiwa uchi, wamekuchoka kuona umejisaidia ovyoovyo..

  7. Mke na watoto wako uncomfortable kwasababu mtaani wanachekwa kuwa wanaishi na baba anayejinyeaa na kujikojolea ovyoovyo. mke anavumilia, watoto wanaona aibu.

  UTAJISIKIAJE KUISHI NA WATOTO wakati wameiona aibu yako namna hii? kama ilivyokuwa kwa Nuhu baba yake kina Ham Jafeti na shemu?


  NB: hii imetokea kabisa kwa mbaba mmoja anakaa kule mbezi ya kimara, na mwingine anakaa kihesa Iringa. nimeshuhudia kwa macho yangu akiwa amejinyea..yule wa iringa ni kwasababu ya ulanzi, huyu wa mbezi hapa dar, ni mapombe tu. watoto wake hawamheshimu kabisa yaani hata wajitahidi kumheshimu hadhi ya baba yao hairudi mioyoni mwao.
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  duhh kwa kweli na mwonea hruma sana huyu mama .......
  kama mimi haya yametokea kwangu itabidi nihame mji..
  kwaajili ya kuondoa aibu na kuwapa amani watoto..
  najua hao watoto watakuwa wameadhirika sana kwa mambo baba yao anafanya...
  na baba itabidi nimatafutie misaada yote kuanzia rehabilitation na maombi....
   
 3. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyo hfaya hivyo kwaabab ya ulevi, sasa dawa yake ni kumpakaa hivyo vinyesi akiwa soba, halaf aone inavyokua then atambue kua hua haina tofauti yoyote na anpokua amelewa.
   
 4. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  lakini kati ya ndoa kumi za walevi/wanywaji, watano wako wa namna hii na wake zao wanaishi katika maisha ya namna hiyo kila siku. hapo kipigo weka pembeni kwasababu hiyo ni kawaida/desturi hata akipigwa hasemi kwa watu kwani kila siku anasubiria kipigo anajua kipo.

  hii story haijapikwa, ipo laivu. watoto wanaishi na mzee wakiwa wameuona utupu wake. na mtaani hamna heshima wala nini. yote katika yote, huwezi jua kama vijana wa kihuni wanaopitiaga walevi mtaani walishamuharibu pasipo yeye kujielewa au la...enyi wenye waume, mwombeni Mungu awasaidie waume zenu waokoke...yatakuja kukukuta mambo makubwa utashindwa hata pa kukiimbilia.

  ninaye babayangu mdogo, ni daktari mzuri sana, na anayo hospitali yake pia. yeye hulewa sana, na mara nyingi mamangu mdogo huwa anawaambia kabisa mabaa medi, ukiona amelewa kodisha taxi nitakuja kukulipia hela, mpakieni mleteni home...baa nyingi wameshamjua na wanamsaidia kwa namna hiyo. hivi karibuni kama mwaka mmoja umepita, huyu daktari amepimwa akaonekana anavyo virusi vya ukimwi...mamangu mdogo (mdogo wa mamangu), ameathirika wakati yeye hanywi pombe, baba kaleta...wanao watoto wawili, sasaivi wanajitahidi kujenga maisha ili watoto wao waje waendelee vizuri pindi watakapoondoka....na wameshaanza kutumia vidonge...hivi pombe unajua inaweza kumpeleka mtu kokote? mabaa medi ndo wanaiba pesa kama nini....inatia uchungu sana, lakini ndivyo ilivyo.
   
 5. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hii scenario inafanana na hali halisi ya jirani yangu ambae mumewe ni msomi mzuri wa uhandisi alikuwa na uwezo mzuri kimaisha lkn hali ikabadilika baada ya kuzidisha pombe aina ya gongo!

  Huyu baba alikuwa anaanza kulewa asbh anaokotwa mjini katikati analetwa na wanaomfahamu either wengine kwa baskeli au mkokoteni akiwa hajitambui,,,kajikojolea na kila kitu! akifika home mkewe anamsafisha,,,anamlisha anamlaza kitandani!baba akawa hawezi tena kazi wakawa wanategemea kodi za wapangaji,,na biashara ndogo.
  Mama ni mrembo watu wakawa wanamwambia acha ujinga wewe,,huyu ndo mme wako??hivi shughuli anaweza tena kweli??mama wa watu akaokoka akawa busy na maombi at least mumewe sasa amepunguza ile hali ya kujichafua imeisha na kazi anafanya.
  Lkn ukweli inahitaji moyo mkuu!!!!
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama kuna mwanamume mwenye akili timamu ana tabia kama hizi
   
 7. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #7
  Dec 18, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si kweli ni uongo mkubwa hakuna mwanamume anayeweza kufanya kazi,mwenye familia na hadhi mtaani anayeweza kunywa pombe mpaka akajinyea hapana nimeona walevi mbwa wa gongo,mbege na ulanzi,wa bia konyagi,wisk,banana na pombe zote kali lakini kujikojolea na kujinyea kwa mlevi wa kweli mwenye kujua maana ya pombe haiwezekani hata siku moja,mlevi anayejinyea na kujikojolea ni yule wa siku moja ambaye hajui ladha na madhara ya pombe.
   
 8. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kosa la huyo mwanamke haiwezekani mwanaume akaanza from nowhere kunywa pombe.tangia wakati wako wa chumba aliona dalili kuwa mwenzake ni alcoholic akazembea kwa kutaka kuolewa au akadhania atambadilisha sasa achume alichopanda,hatuchagui tu mume tunaangalia pia je huyu atakuwa rensponsible father to my children????kisha ndio unaolewa.imekula kwake shauri yake.:teeth::whoo:
   
 9. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  lkn usisahau kuwa tabia ya mtu ni less permanent,,,inawezekana kabisa leo hii ukaolewa na mtu asiyekunywa hata pombe lkn baada ya muda akaanza kunywa na mbaya zaidi akawa mlevi bila hata ya frustration.
   
 10. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  jamani, hata hao wanaokunywa pombe koko ni wanadamu, na wameoa, wana watoto pia, halafu, hata nyie mnaokunywa pombe za kwenye kopo, za kiwandani, mbona ukienda kwenye mabaa mengi tu utakuta mbwa wamefugwa, hata kama hawajafugwa, mbwa koko wengi huwa wanatembelea sana maeneo hayo..kwaajili ya nini? si wanataka kula vinyesi vya walevi?

  asilimia kubwa sana ya madaktari wa binadamu, yaani wale wanaosoma muhimbili etc, nimeshuhudia wakipakiwa kwenye toroli na taxi mara kwa mara hawajielewi kwasababu ya pombe...wasomi wengi sana wanakunywa hadi hawajielewi. tatizo sio usomi, tatizo ni pombe ikikukaa kichwani, kutoka ni ngumu yeye anapoenda bar anaweza akawa anasema..lo, jana nililewa nikamwaga radhi, sasa leo ngoja ninywe kidogo tu...anapokuja kustuka, amekunywa nyingi anashindwa kusimama..miguuu inapigana, magoti yanagongana...anaona nyota...hivi tumbo la aina gani linaweza kunywa bia za nusu lita nusu lita kumi, sawa na lita tano za maji yote unamwagia kwenye tumbo moja hilihili? lazima tumbo likwanguke hapo na aibu utapata.
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Kuwa uyaone...............unafikiri majina kama CHA Pombe yalizuka tu?
   
 12. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  for better or worse walikubali kuishi pamoja kama mume na mke!
  Nawasilisha!
   
 13. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  :pray2::pray2::pray2:
   
 14. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mpaka kifo kitakapo watenganisha!
   
 15. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  na kwa majirani je?
   
 16. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  umefanya utafiti wa kutosha mpk kupinga uliyoyaskia?
  wewe acha ubshi ..tembea uone.izi mambo zipo tena sana.
  nina anko angu alikuwa na tabia izo zote.mlev a to z.
  mkewe alisepa
   
 17. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  mmh mpe pole mwenzako
   
 18. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  ivi jaman kwan hakuna dawa ya kumwachisha pombe mtu?
  achilia mbali rehab senta au counceling hakuna DAWA YA KIENYEJI LABDA YA KUMPA BNADAMU AKAACHA POMBE?
   
 19. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wapo wengi tu my friend, wana akili na wanafanya kazi vizuri tu lakini pombe ndo imewatawala mpaka unamhurumia.
   
 20. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #20
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kila mlevi ana mambo yake akilewa, kuna kaka mmoja mi nilisha wahi kumshudia ni kaka anafanya kazi yake na anajiheshim laki akilewa anaenda mbele ya wanaume wenzie anatoa dola mia anavua nguo anawageuzia makalio wenzie, anaanza kusema haya sasa simnajidai vidume hela hii hapa anaejidai kidume anaweza sana aje anifanye sasa hela hii hapa njooni kama wanaume. Inabidi wanaume wenzie waondoke zao na si mara moja, kwa hiyo ulevi wa aibu upo sana na mtu kama huyo hawezi jiskia aibu mpaka aache pombe. Kuna mbaba mwingine yeye akishalewa anaenda bafuni kuoga anajifunga tower anasahau kuvua anaoga nayo then anaicha bafuni anasahau anatoka uchi ni story za kweli na si uongo yapo sana hayo mambo ya aibu. Wao hawaoni aibu familia yake ndo inakua inatia huruma kwa aibu, pia hawashauriki atakuskiliza then ana acha hapohapo.
   
Loading...