Tusaidiane kuipatia CHADEMA mikakati ya ushindi 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusaidiane kuipatia CHADEMA mikakati ya ushindi 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by C.K, Nov 7, 2010.

 1. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Uchaguzi umepita..! hatuna namna tena zaidi ya kukubali kubeba zigo letu tena- CCM na JK wake kwa miaka mingine 5. Niliwaza kuhama nchi nikakae huko ... mpaka miaka hiyo ipite, lakini baadae nikajirudi kwamba mzalendo wa kweli hapendi kukaa mbali na nchi na watu wake.

  Ninachozidi kugundua ni kwamba CHADEMA pekee ndicho chama chenye nia dhabiti ya kuleta ukombozi wa kweli dhidi ya UMASKINI wa watanzania kwa kuondoa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu - UFISADI i.e ubadhilifu wa mali za nchi.

  Sambamba na kupambana mpaka tupate tume huru ya uchaguzi- NEC, pia tuwachangie mawazo na mikakati wawakilishi wetu (wabunge) na viongozi wote wa CHADEMA mpaka kieleweke 2015. Let's not get tired, we hv just started. Tunaye kamanda wa ukweli - Dr. Slaa ambaye baada ya Nyerere yeye ndiyo rais wangu wa sasa. Mkombozi wa nchi hii ni wewe.., dont undermine yrself. Tembelea tovuti ya chama chetu - CHADEMA, www.chadema.or.tz kisha toa mchango wako. TOGETHER WE CAN!, PEEEEOPLE'S!!!!!!!
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Naona kuna watu nisiowaelewa elewa humu wanajitia kuifahamu sana CHADEMA.
  kwa taarifa CHADEMA wana mtandao mpana sana. sisi wengine hatuthubutu kugusa hata gidamu ya kamba zao za viatu.
  Msijitie kimbelembele mkataka mchaguliwe makatibu kata wa CHADEMA ilhali mmekuja na lengo lenu.

  Nikisoma mistari yako kuna harufu naipata hapo.
  Tulia kwanza isome JF kisha anza kushiriki kama wengine. Hii siyo TAWI la CHADEMA, hapa ni jukwaa huru dogo. Kunywa maziwa ukue utaota meno utang'ata
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nani amekwambia uchaguzi umepita? Unaongelea habari ya uchaguzi kupita wakati Wanananchi bado wanadai kura zao walizompigia Dr Slaa na Chadema? Hakuna kulala, huo mwaka 2015 unaoongela mikakati yake inaendelea, ndio wananchi wanazitaka kura zao, mkakati ndio huu, ndio ajenda kuu, hakuna nyingine.
   
 4. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It's not over.
   
 5. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapo msanii umeniacha hoi na kicheko!
  Ning'amulie hiyo harufu uliyonusa...mi sijui nina mafua :smile-big:
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Umekosea sana mkuu, what if he is innocent and this post is just because he is excited?

  umejuaje kuwa ana harufu unayoisema?

  what are you? nyie ndio mnaoijua sana JF na chadema? huyo mtu atakuja tena kutuma post baada ya kuosma hii ya kwako? asipotuma unapenda mbaki wale wale na mawazo yale yale, huku ukisema unataka mabadiliko?

  Tabia yako haina tofauti na Kingunge au Makamba

  message sent!!!

  umechemsha mkuu, umeniharibia Jumapili yangu kwa watu kama wewe kutuma post kama hizi ambazo ni reproaching!

  Wewe ndio utulie sasa!!
  [​IMG]


  Webby!
   
 7. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Kweli tunatofautiana akili... hivi huyu anayejiita Msanii na mwenzie Atigi ni short au long sighted?! Im doubting kama kweli wako serious na mambo yanayotusibu wanaharakati wa mabadiliko. Kama kazi yenu ni kubomoa mshindwe na mlegee! Hatutaki utani kwenye mambo serious. Wasanii wakubwa nyie, tena wa CCM. Kajiungeni na wasanii wenzenu kumwimbia baba yenu fisadi.

  Kama mpo humu JF kwa mizaha mhamie mitandao mingine ya wasanii wenzenu. Hamna maana, mmenichefua sana, ebooo!
   
 8. kuti kavu

  kuti kavu Member

  #8
  Nov 7, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  @ MSANII

  Utaniwia radhi kama nitakukwaza kwa maneno yangu machache...Lugha uliyotumia mkuu ni kali kupita kupita kiasi. Kama inavyojulikana JF ni jukwaa huru la watu kutoa maoni yao, nafahamu hata mimi mwenyewe mara kadhaa nimekumbana na hoja ambazo zinakwaza humu JF lakini ni vyema tukajifunza kuvumiliana na kukosoana kwa kiungwana. Mtoa hoja akiwa kama mimi nilivyo ni mpya katika JF, kama ligha kama hizi zitakuwa zinatumika kukosoana ni wazi zitakuwa zinakatisha tamaa watu kujiunga na JF...ni vizuri tukikumbuka kuwa hata SENIOR MEMBERS walianza kama sisi tulio wadogo...hivyo no vyema staha ikatumika...

  Lakini pia Japo JF si jukwaa la kichama bado sioni ubaya uko wapi mtu akiweka bayana chama anachokiona yeye kinafaa, ilimradi tu akileta hoja yake kiungwana. Lakini kama walivyosema wenye hekim "kila kitu hakiwezi kuwa kwa kila mtu"...hivyo kama ikitokea umekwazika na hoja humu JF nionavyo mimi nilie mdogo....lugha ya staha ndo njia muafaka ya kukosoana kwani mwisho wa siku sisi wote tu wa TAIFA MOJA!!!
   
 9. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Msanii, a.k.a Mkongwe wa JF hapo umechemka kaka, but don' mind man.
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Huwa naomba radhi kwa kila kosa nililofanya. Lakini huwa naangalia vitu ama hoja ktk pande mbili za shilingi.
  katikati ya hoja mlizozitoa kuhusu USANII wangu ninazidi kuwanusa tu.
  nyakati hizi za hatari ambapo mbinu nyingi zinatumika kunyong;onyesha upinzani hasa chadema nadhani mnapaswa kuwa extra care.

  Kuna mahala nilisoma kwamba HATA SHETANI ANAWEZA KUJA KAMA MALAIKA WA NURU, NA WATUMISHI WAKE KAMA WATUMISHI WA HAKI.

  hakuna ambaye hajui wajibu wa kila mwana mageuzi na supporter wa CHADEMA kuunga mkono na kusaidia chama kukua. Sidhani kama kulikuwa na shime awali ya kuunga mkono CHADEMA ila tuliifanya na tunaifanya kwa utashi wetu. Sasa anapotokea mtu ambaye anajitia povu la rangi puani kwamba tumuamini kwa kila asemalo ni kosa la kiufundi tena lenye gharama sana.
  Ndo mana nimemwambia CK akae, asome na kujifunza how to.... bila hivyo anakuwa hana tofauti na Nakaaya Sumari, kumdhania tunaye lakini kinafsi hatuko naye.

  CK karibu kundini ila jifunnze
   
Loading...